Serikali: Pato la Taifa limekua kwa 6.8% ikilinganishwa na 7.7% ya mwaka jana. Uchumi haujaporomoka!

hakuna wa kujali hata waandike umekuwa 50% watu wanataka kuona uhalisia je kipato cha watu kimekuwa? je Hospital na miundo mbinu muhimu vimeboreka. Ni sawasawa na kusema baba mshahara mwaka kapandishiwa 50% lakini watoto na family hawaoni tofauti wanakula ugali bila mboga kama zamani na wanaishi maisha yaleyale.
Unajua madaraka waliyonayo yamewafanya watuone sisi wote mambwiiiisi !
 
Hii ndio point ya maana katika hiyo taarifa yake. Niliwahi kuangazia huko nyuma kuwa uchumi una tabia ya kubadilika na ni lazima wazalishaji wabadilike kuendana na kasi ya mabadiliko ya uchumi. Huko Detroit nchini Marekani, uchumi wake ulikuwa unategemea sekta ya uzalishaji wa magari. Uchumi ulipobadilika sekta hiyo ilikufa na wazalishaji magari wengi walihama wakitelekeza nyumba zao na mali zao nyingine wakihamia sehemu nyingine ili kuendana na mabadiliko ya tabia za uchumi.
Nampongeza Dr Mpango kwa ku highlight hilo...
Acha kuharibu kiswahili kule Michigan mwaka 2008 sekta ya uzalishaji magari haikufa bali ilidorora magari yakawa hayanunuliwi kutokana na matatizo ya kiuchumi hata Asia haswa Japan Western Europe walikumbwa na kadhia hiyo, serikali ya Obama ikaja na Package ya pesa kuwekeza katika miundombinu na kuyakopesha hayo makampuni kiasi Fulani cha pesa za uendeshaji
 
wali underate performance ya private sector kwenye uchumi, huyu mpango anamdanganya Magu hii model ya uchumi wanayotumia ilishafeli kila mahali duniani
 
Dk Mpango afananisha ukuaji uchumi na mwendo wa gari.

Dar es Salaam. Serikali imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, kuanzia Januari hadi Juni, pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hayo leo Desemba 29,2017 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/18, changamoto na matarajio ya Serikali mpaka Juni.

Amesema tofauti ya mwaka 2016 na huu wa 2017 haina maana kuwa uchumi umeporomoka.

"Ukuaji wa uchumi ni kama mwendo wa gari. Unaweza kwenda Morogoro kwa kasi au taratibu na wote mtafika. Barabarani kuna mambo mengi yanayofanya usiende kasi. Hata kasi ya ukuaji uchumi ni vivyo hivyo," amesema.

Akizungumzia kasi ya ukuaji uchumi ya kitakwimu kutoendana na maisha ya wananchi amesema, "Ili kasi ya uchumi iweze kunufaisha wengi ni lazima watu wafanye kazi katika sekta zinazokua haraka."

"Hapa nchini wengi wapo katika kilimo ambacho kinakua kwa kasi ndogo," amesema.

Akieleza jinsi uchumi wa Tanzania ulivyo tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, amesema mwaka huu utakua kwa asilimia saba.

Chanzo: Mwananchi
Uchumi unakuwa Kwa Watu wachache sana Kwasasa huwezi kufanya kitu cha Maendeleo
 
Mimi Nina Ugonjwa Ambao Hata Waziri Pia Anao Yani Sijui Tofauti Ya Kushuka Na Kupanda....

So Anayeelewa Vizuri Anipe Somo Kidogo Hivi Kutoka 7.7% Mpaka 6.8% Hapo Pato La Taifa Limepanda Au Limeshuka Kwa 0.9%...??????
Uchumi kwa mujibu wa takwimu bado unakua. Kilichoshuka ni kasi ya ukuaji. Kusinyaa uchumi hiyo rate ingekuwa negative sio positive.

Issue kubwa ni ukuaji huo wa uchumi kuweza kuonekana kwa wananchi wa kawaida hasa wenye kipato cha chini. Na jingine ambalo waziri amekwepa kulielezea ni sababu za kasi hiyo ya ukuaji uchumi kupungua. Hapo ndio kuna shida za kisera ambazo kimsingi ndio hasa JPM na timu yake wanapaswa kufanyia kazi.
 
Nadhani watu wameshaanza kufanyia kazi huu ushauri!!!

Sidhani kama kuna sekta inayokuwa kwa kasi hivi sasa kuizidi michezo ya ku-bet! Na kila utakopita, watu ni full ku-bet!
Dah! Unamaanisha kamari? Ni kweli mkuu hata makampuni ya simu yamegundua hilo na kuanzisha vimiradi vya kuwawezesha wananchi ili uchumi wao ukue kwa haraka; mara MSHIKO NJE NJE; mara sijui nini. Ni kamari tu ndio mpango mzima; uchumi wa kamari sio wa vi-wonder tena.
 
Uongo mtupu na hizi namba zao za kupikwa. Uchumi miaka yote unakuwa lakini kitaa ugumu wa maisha unazidi kuongezeka. Juzi tu tumeona wafanyabiashara wa kariakoo wakikalamika jinsi biashara ilivyo ngumu siku chache kabla ya Xmas na hali hii si Kariakoo tu bali ni nchi nzima.

Dk Mpango afananisha ukuaji uchumi na mwendo wa gari.

Dar es Salaam. Serikali imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, kuanzia Januari hadi Juni, pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hayo leo Desemba 29,2017 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/18, changamoto na matarajio ya Serikali mpaka Juni.

Amesema tofauti ya mwaka 2016 na huu wa 2017 haina maana kuwa uchumi umeporomoka.

"Ukuaji wa uchumi ni kama mwendo wa gari. Unaweza kwenda Morogoro kwa kasi au taratibu na wote mtafika. Barabarani kuna mambo mengi yanayofanya usiende kasi. Hata kasi ya ukuaji uchumi ni vivyo hivyo," amesema.

Akizungumzia kasi ya ukuaji uchumi ya kitakwimu kutoendana na maisha ya wananchi amesema, "Ili kasi ya uchumi iweze kunufaisha wengi ni lazima watu wafanye kazi katika sekta zinazokua haraka."

"Hapa nchini wengi wapo katika kilimo ambacho kinakua kwa kasi ndogo," amesema.

Akieleza jinsi uchumi wa Tanzania ulivyo tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, amesema mwaka huu utakua kwa asilimia saba.

Chanzo: Mwananchi
 
Mimi Nina Ugonjwa Ambao Hata Waziri Pia Anao Yani Sijui Tofauti Ya Kushuka Na Kupanda....

So Anayeelewa Vizuri Anipe Somo Kidogo Hivi Kutoka 7.7% Mpaka 6.8% Hapo Pato La Taifa Limepanda Au Limeshuka Kwa 0.9%...??????
Hahaha, anakwambia mwaka jana uchumi ulipanda kwa 7.7%, mwaka huu umepanda tena kwa 6.8%.

Unapanda bado, kwa sababu hiyo 6.8% inajumuisha uchumi wote,hata huo uliopanda kwa 7.7% mwaka jana, ila, kasi ya kupanda imepungua.

Na anasema kuna sababu nyingi zinazofanya kasi ya kupanda ipungue (ingawa hajazitaja), kwa maana ya kwamba, uchumi ukipanda kwa kasi sana bila kuji adjust kupunguza speed, ni kama gari linaloenda kwa kasi sana bila kupunguza spidi, inaweza kutokea ajali.

Kwa hiyo, anaona ni bora uwe unapanda kwa kuongeza na kupunguza kasi bila ajali, maana ukiwa unapanda kwa kuongeza kasi tu, kunaweza kutokea ajali.

I get this dilemma all the time when I drive between 65 and 80 miles per hour. Ukifikisha 80 mph inabidi uanze kufikiria kupunguza speed usisababishe ajali.

Kiuchumi alichosema kinaeleweka kabisa,uchumi hauwezi kupanda tu bila correction.

Lakini hawa sina uhakika sana na namba zao.

Halafu, hata tukikubali namba hizi, kwa sasa hatujui kama kushuka huku kwa kupanda kutoka 7.7% mapak 6.85 ni correction ya kawaida tu (chumi zote zinafanya corrections hizi kuepuka overheating na katika economic cycles as noted above) au ni anguko la uchumi linaloanza polepole kutokana na utawala mbovu.

Ukifuatilia projections za World Bank na IMF, tupo kwenye margin of error ya kuwa na angukola uchumi kuanzia mwaka 2019 kuelekea 2020 na baadaye.
 
Huyo mpango akatubu kwanza toka amepata nafasi hiyo ni uwongo mwanzo mwisho mara uchumi unapaa sijui limekua kombora
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Uchumi utakuwaje sasa wakati umeme unakatika kila siku saa 12 asubuhi na kurudi saa moja jioni. Upuuzi tu....
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Uchumi kwa mujibu wa takwimu bado unakua. Kilichoshuka ni kasi ya ukuaji. Kusinyaa uchumi hiyo rate ingekuwa negative sio positive.

Issue kubwa ni ukuaji huo wa uchumi kuweza kuonekana kwa wananchi wa kawaida hasa wenye kipato cha chini. Na jingine ambalo waziri amekwepa kulielezea ni sababu za kasi hiyo ya ukuaji uchumi kupungua. Hapo ndio kuna shida za kisera ambazo kimsingi ndio hasa JPM na timu yake wanapaswa kufanyia kazi.

we unajua maana ya negative kasome hesabu wacha kudanya watu

check hapo chini

7.7 % +( -0.9%)= 6.8%
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Back
Top Bottom