Serikali: Pato la Taifa limekua kwa 6.8% ikilinganishwa na 7.7% ya mwaka jana. Uchumi haujaporomoka!

real G

JF-Expert Member
Feb 7, 2013
5,227
5,287
Dk Mpango afananisha ukuaji uchumi na mwendo wa gari.

Dar es Salaam. Serikali imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, kuanzia Januari hadi Juni, pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hayo leo Desemba 29,2017 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/18, changamoto na matarajio ya Serikali mpaka Juni.

Amesema tofauti ya mwaka 2016 na huu wa 2017 haina maana kuwa uchumi umeporomoka.

"Ukuaji wa uchumi ni kama mwendo wa gari. Unaweza kwenda Morogoro kwa kasi au taratibu na wote mtafika. Barabarani kuna mambo mengi yanayofanya usiende kasi. Hata kasi ya ukuaji uchumi ni vivyo hivyo," amesema.

Akizungumzia kasi ya ukuaji uchumi ya kitakwimu kutoendana na maisha ya wananchi amesema, "Ili kasi ya uchumi iweze kunufaisha wengi ni lazima watu wafanye kazi katika sekta zinazokua haraka."

"Hapa nchini wengi wapo katika kilimo ambacho kinakua kwa kasi ndogo," amesema.

Akieleza jinsi uchumi wa Tanzania ulivyo tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, amesema mwaka huu utakua kwa asilimia saba.

Chanzo: Mwananchi
 
"Hapa nchini wengi wapo katika kilimo ambacho kinakua kwa kasi ndogo," amesema.
Ndio maana nasema kuanzia rais mpaka huyu mpango wote ni WAJINGA na wasio na akili timamu!!

Yaani wanajua kabisa watanzania wengi wapo kwenye kilimo alafu wanasema kilimo kinakua kwa kasi ndogo! kwanini wasiboreshe kilimo ili kikue kwa kasi kubwa na wengi wanufaike???

Je hizo sekta zinazokua kwa kasi (kama kweli zipo japo siamini) ni zipi? je mwananchi wa aliyepo kijijini sumbawanga anaweza akawekeza kwenye hizo sekta??
 
Mimi Nina Ugonjwa Ambao Hata Waziri Pia Anao Yani Sijui Tofauti Ya Kushuka Na Kupanda....

So Anayeelewa Vizuri Anipe Somo Kidogo Hivi Kutoka 7.7% Mpaka 6.8% Hapo Pato La Taifa Limepanda Au Limeshuka Kwa 0.9%...??????
Hapa anaongelea ukuaji wa uchumi, na kwa data zake ni kwamba ukuaji wa uchumi mwaka huu umeshuka ukilinganisha na mwaka jana!!

Na kama ukuaji umeshuka ina maana hata pato litakua limeshuka pia ukilinganisha na mwaka jana!
 
Akizungumzia kasi ya ukuaji uchumi ya kitakwimu kutoendana na maisha ya wananchi amesema, "Ili kasi ya uchumi iweze kunufaisha wengi ni lazima watu wafanye kazi katika sekta zinazokua haraka."
Nadhani watu wameshaanza kufanyia kazi huu ushauri!!!

Sidhani kama kuna sekta inayokuwa kwa kasi hivi sasa kuizidi michezo ya ku-bet! Na kila utakopita, watu ni full ku-bet!
 
Akizungumzia kasi ya ukuaji uchumi ya kitakwimu kutoendana na maisha ya wananchi amesema, "Ili kasi ya uchumi iweze kunufaisha wengi ni lazima watu wafanye kazi katika sekta zinazokua haraka."

"Hapa nchini wengi wapo katika kilimo ambacho kinakua kwa kasi ndogo," amesema.
Hii ndio point ya maana katika hiyo taarifa yake. Niliwahi kuangazia huko nyuma kuwa uchumi una tabia ya kubadilika na ni lazima wazalishaji wabadilike kuendana na kasi ya mabadiliko ya uchumi. Huko Detroit nchini Marekani, uchumi wake ulikuwa unategemea sekta ya uzalishaji wa magari. Uchumi ulipobadilika sekta hiyo ilikufa na wazalishaji magari wengi walihama wakitelekeza nyumba zao na mali zao nyingine wakihamia sehemu nyingine ili kuendana na mabadiliko ya tabia za uchumi.
Nampongeza Dr Mpango kwa ku highlight hilo...
 
Nadhani watu wameshaanza kufanyia kazi huu ushauri manake kila pahala ni vibanda vya ku-bet na hakuna sekta inayokuwa kwa kasi kama ya kamali
Mkuu, nilikuwa sijaona post yako. Naona mawazo yetu yamefanana maana wote tume highlight iyo ajenda. Kwa kweli hicho ndicho kitu cha muhimu...
 
Kweli namba uwa asijawai mwacha mtu salama kumbe inanza 7 inakuja 6 alaf inakuja 8 alisema bashe kuwa anaheshimu sana academic background ya mpango ila mimi nina mashaka nayo
 
Hizo ndo takwimu ukizipinga mwaka utakupindukia jera.
Uchumi umekuwa na AJIRA zimeongezeka ni takwimu mzuri maana vinaendana
 
kutoka 7.7 hadi 6.8, wenyewe wanakiri uchumi kushuka harafu wanakataza kusema vyuma vimekaza
 
Dk Mpango afananisha ukuaji uchumi na mwendo wa gari.

Dar es Salaam. Serikali imesema katika nusu ya kwanza ya mwaka 2017, kuanzia Januari hadi Juni, pato la Taifa limekua kwa asilimia 6.8 ikilinganishwa na asilimia 7.7 ya kipindi kama hicho mwaka jana.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango amesema hayo leo Desemba 29,2017 alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa uchumi wa Taifa, utekelezaji wa bajeti mwaka 2017/18, changamoto na matarajio ya Serikali mpaka Juni.

Amesema tofauti ya mwaka 2016 na huu wa 2017 haina maana kuwa uchumi umeporomoka.

"Ukuaji wa uchumi ni kama mwendo wa gari. Unaweza kwenda Morogoro kwa kasi au taratibu na wote mtafika. Barabarani kuna mambo mengi yanayofanya usiende kasi. Hata kasi ya ukuaji uchumi ni vivyo hivyo," amesema.

Akizungumzia kasi ya ukuaji uchumi ya kitakwimu kutoendana na maisha ya wananchi amesema, "Ili kasi ya uchumi iweze kunufaisha wengi ni lazima watu wafanye kazi katika sekta zinazokua haraka."

"Hapa nchini wengi wapo katika kilimo ambacho kinakua kwa kasi ndogo," amesema.

Akieleza jinsi uchumi wa Tanzania ulivyo tofauti na nchi nyingine za Afrika Mashariki, amesema mwaka huu utakua kwa asilimia saba.

Chanzo: Mwananchi
huyu dk bogus. au mwandishi amemquote vibaya.
ukuaji wa uchumi

1) 2015/2016= 7.7%
2) 2016/2017= 6.8%
kwa data hizo uchumi umesinyaa,
 
Nimechoka na hizi blah blah zisizo na mbele wala nyuma. To hell!
hakuna wa kujali hata waandike umekuwa 50% watu wanataka kuona uhalisia je kipato cha watu kimekuwa? je Hospital na miundo mbinu muhimu vimeboreka. Ni sawasawa na kusema baba mshahara mwaka kapandishiwa 50% lakini watoto na family hawaoni tofauti wanakula ugali bila mboga kama zamani na wanaishi maisha yaleyale.
 
Back
Top Bottom