Waziri Kijaji: Tanzania ina viwanda vya chuma 28 vyatoa ajira 25,358 kwa Watanzania

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,955
4,967
Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji amesema kuwa Tanzania ina jumla ya viwanda 28 vya kuzalisha chuma na bidhaa za chuma.

Dkt. Kijaji ameyasema hayo Leo mei 21,2024 Bungeni Wakati akiwasilisha Hoja ya Bajeti ya Makadirio ya mapato na matumizi ya mwaka wa fedha 2024/2025 ya Wizara ya Viwanda na Biashara

Dkt. Kijaji amesema kuwa Viwanda hivyo vipo katika makundi mbalimbali yanayojumuisha nondo, mabati, mabomba, misumari, na senyenge na vimeajiri jumla ya wafanyakazi 25,358, kati ya hao wafanyakazi 4,169 ni ajira za moja kwa moja na wafanyakazi 21,189 wa ajira zisizo za moja kwa moja.

Aidha amesema kati ya viwanda hivyo, viwanda 19 vinazalisha nondo na vina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 1,299,240 kwa mwaka. Hadi kufikia Machi 2024 viwanda hivyo vilizalisha nondo tani 900,000 ikilinganishwa na mahitaji ya nondo tani 605,369.6.

Aidha Dkt. Kijaji amesema uzalishaji huo ulitosheleza mahitaji yote ya ndani na ziada kiasi cha tani 294,630.4 kiliuzwa katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (DRC, Burundi na Rwanda).

Viwanda 24 vya Mbolea
Serikali imesema kuwa ili kuondoa utegemezi wa kuagiza mbolea kutoka nje ya nchi, Wizara imeendelea kuhamasisha ujenzi wa viwanda vya mbolea ambapo hadi kufikia mwezi Machi, 2024, Tanzania ina jumla ya
viwanda 24 vya mbolea.

Akiwasilisha Bajeti ya Wizara Leo Mei 21, 2024 Bungeni na Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt. ashatukijaji amesema kuwa kati ya viwanda hivyo, viwili (2) ni vikubwa ambavyo ni Minjingu na Intracom Fertilizer Limited, kimoja ni cha kati; na vilivyosalia (21) ni viwanda vidogo ambavyo hufanya kazi ya kuchanganya mbolea (Blending)

Mchango wa Viwanda katika pato la Taifa
Mchango wa Sekta ya Viwanda katika Pato la Taifa kwa mwaka 2023 ulikuwa asilimia 7.0 ikilinganishwa na asilimia 7.1 mwaka 2022. Aidha, ukuaji wa Sekta ya Viwanda ulikuwa asilimia 4.3 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2022.

Mchango wa Sekta ya Biashara katika Pato la Taifa kwa mwaka 2023 ulikuwa asilimia 8.3 ikilinganishwa na asilimia 8.2 mwaka 2022. Aidha, kasi ya ukuaji wa Sekta ya Biashara ilikuwa asilimia 4.3 mwaka 2023 ikilinganishwa na asilimia 3.9 mwaka 2022. Ukuaji huo umechangiwa na uboreshaji wa mazingira ya ufanyaji biashara.

Pia soma
- Waziri Kijaji: Tanzania ina viwanda 13 vya Magari

- Waziri Kijaji: Mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
 
Ni kweli au mkiambiwa kingereza ndio maelewa ,assembling ya baadhi ya magari inafanyika hapa
 
Aidha amesema kati ya viwanda hivyo, viwanda 19 vinazalisha nondo na vina uwezo uliosimikwa wa kuzalisha tani 1,299,240 kwa mwaka. Hadi kufikia Machi 2024 viwanda hivyo vilizalisha nondo tani 900,000 ikilinganishwa na mahitaji ya nondo tani 605,369.6.
Hizo nondo zinazozalishwa pale Arusha ukiikunja inavunjika. Hazifai/hazina ubora. Wenye akili/uwezo wa fedha wanatumia nondo kutoka Kenya.
 
Ni siasa tupu na hadaa. Hawa watawala wetu wanaishi sayari nyingine kabisa.Na huko viwandani Watanzania wamekua watumwa.Hakuna wa kuwasemea wala wa kuwatetea
 
Back
Top Bottom