Serikali nzima kitanzini!

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,005
Serikali nzima kitanzini
Tuesday, 19 July 2011 21:11

Neville Meena, Dodoma
Mwananchi

WAKATI umma wa Watanzania ukisubiri hatua zitakazochukuliwa na Rais Jakaya Kikwete dhidi ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, David Jairo, Kamati ya Bunge ya Mashirika ya Umma (POAC) inakusudia kuchukua hatua za kufuatilia fedha zote zilizotolewa na mashirika ya umma kwa kigezo cha kusaidia kupitisha bajeti.

Habari ambazo Mwananchi lilizipata jana na kuthibitishwa na Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe zinasema kwamba hatua hiyo inalenga kubaini kiasi cha fedha ambacho Wizara za Serikali zimekuwa zikidai kutoka katika idara na taasisi zilizoko chini yake kwa kigezo kwamba fedha hizo zinatakiwa kusadia kupitisha bajeti.

Akithibitisha taarifa hizo, Zitto alisema; "Tunapaswa kufanya uchunguzi ili kubaini kiasi cha fedha za umma ambazo zimetumika katika kipindi cha miaka mitatu iliyopita, maana kuna uwezekano kwamba huu ndio mchezo ambao umekuwa ukifanywa na wizara zetu hizi".

Tuhuma zinazomkabili Jairo
Jairo anakabiliwa na tuhuma za kuwaandikia barua wakuu wa idara zote zilizoko chini ya wizara yake, ili watoe fedha kwa ajili ya kusaidia kupitishwa kwa bajeti ya wizara hiyo, fedha ambazo zinatafsiriwa kwamba zilikuwa ni kwa lengo la kutoa rushwa.

Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo ndiye aliyemlipua Jairo Bungeni juzi kwamba amekusanya kiasi cha Sh1 bilioni kutoka taasisi 21 zilizopo chini ya Wizara yake na kwamba fedha hizo hazina maelezo.

Shellukindo aliendelea kusema kuwa barua hiyo inaonyesha kuwa kila idara na taasisi hizo ziliagizwa kuingiza kiasi cha Sh50 milioni kila moja kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological
Survey of Tanzania (GST) (Taasisi ya Utafiti wa Jiojia) iliyopo kwenye benki ya NMB, tawi la Dodoma.

Taarifa ambazo Mwananchi ilizipata bungeni juzi zilidai kwamba mara baada ya Shellukindo kurusha kombora hilo, Waziri Mkuu, Mizengo Pinda aliagiza kutafutwa kwa taarifa za akaunti husika, na kwamba katika muda mfupi ilithibika kwamba fedha hizo ziliingizwa kisha kutolewa.

Hata hivyo haikiwekwa bayana kiasi halisi cha fedha zilizoingizwa na idara hizo na siku ambayo zilichukuliwa.

Akizungumza wakati wa kuondoa hotuba ya makadirio ya Wizara ya Nishati na Madini bungeni juzi jioni baada ya bajeti hiyo kukataliwa na wabunge, Pinda alisema alikuwa akifanya utaratibu wa kuwasiliana na Rais Kikwete aliyekuwa safarini Afrika Kusini ili kupata ridhaa ya kuchukua hatua dhidi ya Jairo.

"Kikwazo pekee nilichokipata ni kwa sababu Rais hajatua South Africa (Afrika Kusini) na mwenye mamlaka ya kuteua Makatibu Wakuu ni Rais mwenyewe. Nikatamani sana nije hapa mimi niwaambieni nimeishachukua hatua, nimeamua hivi. Lakini, nikaambiwa utakuwa unaingia katika maeneo ambayo si ya kwako,"alisema Pinda na kuongeza:

"......kwa hiyo, kwa hili, naomba niwaombe Waheshimiwa Wabunge, kwa dhati kabisa, kwamba kwa sababu sina mamlaka juu ya mtu huyu ya kumtimua kazi leo au kumwambia ondoka, mwenye mamlaka ni Rais mwenyewe, kwa hili mnipe baraka zenu, akifika South Africa, jioni ya leo mimi nitawasilisha maelezo haya kwake".

Kwa mujibu wa Pinda, tuhuma dhidi ya Jairo si jambo ambalo halina maelezo kwani liko dokezo lililioloandikwa na kusomwa bungeni ambalo linathibitisha kwamba Katibu huyo wa zamani wa Rais Kikwete ana hatia.

Ngeleja amruka Jairo
Habari zaidi zilizopatikana jana mjini Dodoma zilidai kwamba Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alikanusha vikali kufahamu chochote kuhusu utekelezaji wa mpango huo wa wizara yake kukusanya fedha hizo kwa ajili ya kuwezesha upitishaji wa bajeti.

Habari za uhakika kutoka ndani ya kikao cha Kamati ya Wabunge wa CCM kilichofanyika juzi mchana zinadai kwamba kauli ya Ngeleja kwamba hafahamu chochote, zilifuatia hoja iliyotolewa na Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka akitaka Waziri huyo kujiuzulu.

"Alisema haiwezekani Waziri asifahamu kuhusu mpango huu wa ukusanyaji wa fedha, wala haiingiii akilini kwamba hajui chochote, mimi nadhani wakati tukitaka Katibu Mkuu afukuzwe ifikapo leo saa 11 jioni, basi hata waziri naye aachie ngazi,"chanzo chetu kilimnukuu Ole Sendeka.

Gazeti hili lilipomtafuta mbunge huyo wa Simanjiro kuhusu taarifa hizo, hakukanusha wala kukubali zaidi ya kusema kuwa: "hayo yalikuwa ni mambo ya ndani ya chama na waziri mkuu alishatoa msimamo wa Serikali, mimi sina lolote la kuongeza".

Kwa upande wake Ngeleja aliliambia Mwananchi kuwa hawezi kuzungumza chochote kuhusu suala la Katibu Mkuu wake kwani tayari lilikuwa limechukuliwa na viongozi waandamizi wa Serikali kwa ajili ya kulifanyia kazi.

Habari kutoka ndani ya kikao cha kamati ya wabunge wa CCM zinasema kuwa wabunge hao walikuwa wametoa muda kwa Serikali kwamba hadi saa 11 jioni juzi Jairo awe amefukuzwa kazi.

Kwa mujibu wa habari hizo, wabunge hao pia waliitaka Serikali kuielekeza Taasisi ya Kuzuia na Kupamba na Rushwa (Takukuru) kuaza uchunguzi wa jinsi fedha hizo zilivyotolewa na matumizi yake, ili ikibainika vinginevyo wahusika waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.

Kashfa rushwa Nishati
Wiki mbili zilizopita, gazeti hili liliporipoti kuhusu jaribio la maofisa wa wizara hiyo kutaka kuwahonga baadhi ya wabunge katika Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kile kilichodaiwa kutaka bajeti ya wizara hiyo kupita kwa urahisi.

Jumatatu, Julai 4, 2011 Mwananchi lilinukuu vyanzo vyake mjini Dodoma na Dar es Salaam vikibainisha kuwa taarifa za uovu zilifikishwa mezani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ambaye alinukuliwa akisema kuwa angezishughulikia baada ya kuwa amewasiliana na Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja.

Kwa mujibu wa habari hizo suala hilo pia lilifikishwa kwa Spika wa Bunge, Anne Makinda na kwamba Kamati ya Uongozi ya Bunge anayoiongoza pia iliarifiwa kuhusu suala hilo.

Waziri Mkuu, Pinda alipozungumza na Mwananchi alikiri kupata taarifa za tuhuma hizo japokuwa halikuwa limefikishwa rasmi kwake.
Habari zilizolifikia Mwananchi zilidai kwamba, Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Makamba ndiye aliyewashtaki wajumbe wa kamati yake kwa Spika huku akiwachongea watumishi wa Wizara ya Nishati na Madini kwa Pinda kutokana na kujihusisha na vitendo vya rushwa.

http://reddit.com/

Tulishaongea hadi tukachoka kuwa hii sirikali ya ****** ipo kirushwarushwa, wakatujibu kelele za mlangoni sijui nini vile haziwanyimi usingizi. Yameshaanza kutokea sasa, nafikiri now mnakosa usingizi na kama bado mmelala then huo sio usingizi, mnaweza kuwa mlishakufa zamaniii na kwa sasa wameshaanza kutoa harufu.. ptuuuuu!!
Shennnnzy taipu..:pound: afu ngeja uunasema hujui kitu? hii laana itakuandama wangu..!!!
 
huu mchezo ni wa siku nyingi dana kumbe ndiyo maana wabunge wa CCM huwa wanaunga mkono kila kitu hata kama ni hoja ya ovyo vipi
 
ole sendeka walau umeongea cha maana! na waziri ajiuzulu! wanataka kumtoa kafara jairo, hiyo 1 B inamaana hawakuijua? kuna haja pia ya uchunguzi,hiyo hela ilitolewa kwenye hiyo account ikaelekwa kwenye account gani? otherwise hakuna haja ya kutupa hela kwenye tume afu findings zisifanyiwe kazi!
 
Kwa hili serikali iko matatani. Naipata faraja pale tu nnapoona kuwa wabunge wa vyama vyote waliungana hata kabla ya kuahirishwa kwa hoja ya wizara husika, wabunge walionesha msimamo wao wa dhati wakati walipokuwa wakichangia hoja, hii ilikuwa kwa karibu wabunge wote, walikuwa hawataki kabisa kuunga hoja mkono. Wa CCM ndio walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii hoja.

Nna uhakika, yatavumbuka mengi kutokana na sakata hili na ni wakati muafaka wa kuweka mambo sawa kwa faida ya wananchi.

Sina shaka kabisa kuwa waziri atajiuzulu.

Nishati na madini ni vitu nyeti sana kwa Taifa letu, tuliona lilivyowang'oa mawaziri mpaka waziri mkuu si muda mrefu uliopita.
 
inamaana W.N bado yuko ofisini je D.J nae yupo ofsn? viongozi wetu bwana, yani DJ licha ya kuumbuliwa bungeni bado yupo tu ofisini.
 
Hawa wanaojiita Wapinzani walikuwa wapi siku zote? inaonyesha ni jinsi gani hawapo makini kwenye kufuatilia utendaji wa serikali!
Sikutegemea ishu kama hii iibuliwe na mbunge wa Chama tawala!
Akina Zitto wakae tu kimya, wameshachemsha.
 
Hivi, hili lingesanuliwa na mbunge wa CDM, lingeungwa mkono hivyo na Magamba?
 
Hawa wanaojiita Wapinzani walikuwa wapi siku zote? inaonyesha ni jinsi gani hawapo makini kwenye kufuatilia utendaji wa serikali! Sikutegemea ishu kama hii iibuliwe na mbunge wa Chama tawala! Akina Zitto wakae tu kimya, wameshachemsha.
Mangapi wameyaibua, wabunge wa magamba sijui kwa kuwalobbed wameyapinga na kuunga mikono 101% hoja za serikali yenu!
 
Hawa wanaojiita Wapinzani walikuwa wapi siku zote? inaonyesha ni jinsi gani hawapo makini kwenye kufuatilia utendaji wa serikali!
Sikutegemea ishu kama hii iibuliwe na mbunge wa Chama tawala!
Akina Zitto wakae tu kimya, wameshachemsha.
Kwani kila kitu negative lazima kiibuliwe na wapinzani hapo unakosea mkuu
 
Hawa wanaojiita Wapinzani walikuwa wapi siku zote? inaonyesha ni jinsi gani hawapo makini kwenye kufuatilia utendaji wa serikali! Sikutegemea ishu kama hii iibuliwe na mbunge wa Chama tawala! Akina Zitto wakae tu kimya, wameshachemsha.
Bungeni si sehemu ya porojo, mbunge akiibua kashfa lazima awe na source na evidence, sasa wewe unataka wapinzani wawe watu wa kubwabwaja tu, ishu za huyo katibu mkuu zilikuwa kwenye status ya gossip kwa muda mrefu but kulikuwa hakuna ushahidi, thank God ushahidi umepatikana na jamaa kaanikwa lakini hata hivyo mbona wapinzani wameibua kashfa nyingi very positive, just be honest! kashfa imeibuliwa na mbunge wa ccm lakini wapinzani wameunga mkono licha ya kuwa viceversa huwa ni vigumu!
 
Hivi, hili lingesanuliwa na mbunge wa CDM, lingeungwa mkono hivyo na Magamba?
Mara nyingi inakuwa ni vigumu kwa wabunge wa ccm kuunga mkono hoja za cdm hasa kuhusu masuala ya kashfa zinazowakabili watendaji wa serikali, kumbuka yalomkuta zitto kabwe akasimamishwa kuhudhuria vikao bungeni kwa muda fulani, wabunge wa ccm waliibeza hoja yake lakini baadae ilijulikana kuwa zitto kasema kweli kwa hiyo nadhani kwa tabia ya ccm kama hoja hiyo ingeletwa na mbunge wa upinzani wangeibeza!
 
Kwa hili serikali iko matatani. Naipata faraja pale tu nnapoona kuwa wabunge wa vyama vyote waliungana hata kabla ya kuahirishwa kwa hoja ya wizara husika, wabunge walionesha msimamo wao wa dhati wakati walipokuwa wakichangia hoja, hii ilikuwa kwa karibu wabunge wote, walikuwa hawataki kabisa kuunga hoja mkono. Wa CCM ndio walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii hoja.

Nna uhakika, yatavumbuka mengi kutokana na sakata hili na ni wakati muafaka wa kuweka mambo sawa kwa faida ya wananchi.

Sina shaka kabisa kuwa waziri atajiuzulu.

Nishati na madini ni vitu nyeti sana kwa Taifa letu, tuliona lilivyowang'oa mawaziri mpaka waziri mkuu si muda mrefu uliopita.

Mkuu FaizaFoxy,
Leo imekuwaje unatoa 'comment' ya kumpinga na kumkandamiza W.N.M na serikali yako ya CCM tofauti na 'comment' zako za siku nyingine hapa JF?
Au kwa kuwa kule mjengoni wewe ndiye uliyetoa hadharani barua ya DJ lili asulubiwe hivyo unaiendeleza hoja yako hapa JF?
'Bravo' Mkuu, anyway kwa hili tupo pamoja. kwani tuna uhakika DJ alitekeleza maagizo ya W.N.M. Tunaomba uendelee kusimamia hoja yako.
'My Regrets; Sorry' Usiulize nimekujuaje.

Mie napita tu.......................

Kwa hili serikali iko matatani. Naipata faraja pale tu nnapoona kuwa wabunge wa vyama vyote waliungana hata kabla ya kuahirishwa kwa hoja ya wizara husika, wabunge walionesha msimamo wao wa dhati wakati walipokuwa wakichangia hoja, hii ilikuwa kwa karibu wabunge wote, walikuwa hawataki kabisa kuunga hoja mkono. Wa CCM ndio walikuwa mstari wa mbele kuipinga hii hoja.

Nna uhakika, yatavumbuka mengi kutokana na sakata hili na ni wakati muafaka wa kuweka mambo sawa kwa faida ya wananchi.

Sina shaka kabisa kuwa waziri atajiuzulu.

Nishati na madini ni vitu nyeti sana kwa Taifa letu, tuliona lilivyowang'oa mawaziri mpaka waziri mkuu si muda mrefu uliopita.

Hongera zako FF. Nayafurahia mabadiliko ninayoyaona katika michango yako katika mijadala mbali mbali hapa jamvini. Siku za mwanzo ulikuwa hukosoi chochote ndani ya CCM au Serikali. Siku zote ulikuwa unapigia debe tu au kufagilia mambo mengi tu hata yale ambayo hayakustahili kuyafagilia.
 
Back
Top Bottom