Serikali njoo msome hii hapa tafadhali

stella1975

JF-Expert Member
Nov 25, 2018
870
1,249
Viongozi Wangu wa kiserikali kwanza poleni kwa Vita hiii mnayopigana ya Covid -19 hii ni Vita ya kidunia tunapigana wote hivyo natoa ushauri Wangu huu hapa chini Namna bora ya kupigana vita hiii pasipo kukimbilia kufungia watu ndani kutokana na mataifa mengi kukopi na kupesti

HATUA KWA HATUA KUANZIA HATUA YA KWANZA HADI YA MWISHO

1.KUFUNGA MIPAKA YOTE YA NCHI HAKUNA KUTOKA NJE WALA HAKUNA WA KUINGIA NDANI YA NCHI

hapa unafunga mipaka Yote ya nchi unazuia Ndege zote za kuingia na kutoka na vyombo vyote vya usafiri nje ya nchi, ukishafanya hivyo inapigwa Elimu Kwa wananchi Juu Ya corona namna ya kujikinga na Namna Ya kuchukua tahadhali na Namna ugonjwa unavyoambukiza Dalili na kusihi jamiii kusaidia kutoa taarifa pale wanapomhisi mtu ,ukishindwa hiii unachukua hatua nyingne Kama ifuatavyo

2.UNAFUNGA SHULE ZOTE NA KUPIGA MARUFUKU MIKUTANO MIKUBWA

hapa utafunga vyuo na shule na mikutano mikubwa hiii mikutano mikubwa unaiorodhesha Kama vile Ya hadhara, makongamano na sherehe, masoko makubwa yooote Kama kariakooo, usifunge shule halafu ukaiacha kariakooo ile kariakooo ni zaid ya shule kariakoo ni zaid ya mikutano ya hadhara Kama hujui matokeo ya kariakoo ngoja nikungate sikio kariakoo ni sehemu inayoweza kuwa chanzo cha maaambukizi ndani ya dar na nje ya dar, mtu aliyoko Mbinga anaweza kuupata ugonjwa chanzo kikawa ni kariakooo, Wakati huuu ile Elimu inaendelea kwa kuongeza kasi, ukishindwa unachukua hatua inayofuata

3.UNAFUNGA MIKUSANYIKO YA KATI
hapa unafunga mikusanyiko yooote ya Kati ,unaiorodhesha hiii mikusanyiko ya Kati nikama vile, makanisa, masoko makubwa, Harusi, mazishi, happybaday na mingne miingi ya Kati tu, Wakati huuu Elimu imeongezeka na kuhusisha wadau weeengi na kuwasaka wooote wanaoshukiwa kwa kuwapima, kupima kunaanzia hapa sasa ila Kwa wale washukiwa tu, ukishindwa unachukua hatua nyingne Kama ifuatavyo

4.UNAFUNGA MIKUSANYIKO MIDOGO YOOTE
Hapa unapiga marufuku mikusanyiko yooote midogo na lazima uiorodheshe, unapoiorodhesha unaepusha mgogoro kwa jamiii na polisi, unaepusha madhara ya kupigana watu Au kunyanyaswa na polisi, hiii ni ile mikusanyiko midogo Kama vile mabaaar Yote yanafungwa, minada yoote inafungwa, masoko yooote yanafungwa hapa kuna masoko makubwa yalisha fungwa kule kwenye mikusanyiko mikubwa na masoko makubwa nikama kariakooo na mengne ila madogo ni haya ya mitaaani ndio madogo yooote, unafunga usafiri wote wa umma, unafunga Hakuna wa kutoka Mkoa kuingia Mkoa mwingne na hakuna watu kusimama zaid ya watano, na Hakuna gari private Ya kubeba watu zaid ya watatu, na Hakuna Duka linaloruhusiwa kufunguliwa ila unaacha maduka ya vyakula, Bucha, Famacy na hospital, pia unafunga maduka Yote ya mjini Kama kariakoo, Posta na miji mingne hapa unaaanza kutangaza ratiba ya upimaji nyumba hadi nyumba na kila Mtaa Au kata inapewa Siku mbili au Tatu kukutwa ndani, hapa inakuwa umefungiwa watu Kwa Siku chache Tatu Au mbili Kwa kuwapima na unawafungia kwa kimaeneo, ukikamilisha hapa walai nakuambia baada ya two months utakuwa huna maaambukizi hata ya mtu mmoja
Hapa utakuwa umepambana kisomi na kumaliza kisomi

USHAURI WANGU KWA WASOMI
nyie wasomi mnakula mshahara mko huko juuu mambo Kama haya yanawashindaje? Kwa nini mnashindwa kushauri na kuchukua hatua Kama hiii

Cha kuskitisha unaweza kukuta nchi hata haijafuata huuu utaratibu unasikia wanatoa tamko watu wote wabaki ndani hivi viongozi wa nchi hiyo tukiwata mashtole watakasirika? Kuna viongozi wasiojitambua Kabisa fuata hatua kwa hatua, huwezi kwenda la Saba kwa kuruka la sita na tano

UTEKELEZAJI WA ZOEZI HILI UTAFUATA MUONGOZO HUUU

kwanzaa ili ufanikishe vizuri Jambo hilo unapaswa kuwa na mfumo wa utekelezaji Kama ifuatavyo

Unaandaaa Kamati tano tofauti ambazo kila Kamati itakuwa na Kazi yake ambayo haitaingilia Kamati nyingne, Kamati hizo zitakuwa Kama ifuatavyo :

1.KAMATI YA KUZUIA NA KUDHIBITI

hiii Kamati Kazi yake itakuwa ni kuzuia na kudhibiti kwa kuhakikisha kuwa hakuna anaeingia nchini au mkoani au wilayani au katani Au Kijijini pasipo kuhakikiwa hali ya Afya yake, Kamati hiii inaweza kuzuia mtu yoyote kuingia eneo hilo pale inapobidi yani kuingia nchini Au Mkoa Au wilaya Au Kata Au Kijijini, hiii Kamati ndio itakuwa mwamvuli kwa mwananchi ambae hana corona ndio itakayochukua jukumu la kuwakinga wasio na maambukizi kwa kuhakikisha kuwa huyu ambae hana anabaki Salama, Kamati hiii itakuwepo ya kitaifa, kimkoa, kiwilaya, kikata na Kijijini na kila Kamati itawajibika kwa ngazi ya Juu yake

2.KAMATI YA ELIMU
hii Kamati Kazi yake itakuwa ni kutoa Elimu Ya kujikinga na Elimu yoooote inayohusiana na ugonjwa huuuu, Kamati hiii ndio itakayokuwa na mamlaka ya kutoa muongozo Juu Ya Namna Ya sisi kukutana, kusimama kusafiri, kusalimiana na miongozo mingne inayohusiana na uelewa, Kamati hiii itakuwepo katika ngazi zote za kitaifa, kimkoa, kiwilaya, kikata na kijiji na kila Kamati itawajibika kwa ngazi ya Juu

3.KAMATI YA KUTIBU NA KURATIBU WAGONJWA

Him Kamati itahusika na wagonjwa tu pamoja na washukiwa tu, hiii itasimamia ukusanyaji wa wagonjwa na kuwapeleka sehemu zilizoandaliwa kwa kuwatunza na kuwatibu, hiii Kamati ndio itakayoaandaa sehemu za kuwaweka wagonjwa na waliofariki, ndio Kamati itakayosimamia mazishi ya waliofariki na kutoa muongozo we mazishi, Kamati hiii itakuwa na jukumu la kuhakikisha kuwa yoyote Yule anaeshukiwa anakuwa mikononi mwao fasta, anachukuliwa fasta, waweke utaratibu wa wao kupata taarifa na kuandaa mazingira ya kupewa taarifa Mara tu mgonjwa atakapokuws amehisiwa, pia hiii itakuwa na jukumu la kuwafuatilia wale ambao wamepona na kurhuhusiwa, watawafuatilia kwa ukaribu hata kwa miezi Tatu,

4.KAMATI YA KUKUSANYA RASILIMALI
hiii ndio Kamati iyakayokuwa inakusanya rasilimali na kuzigawa kwenye Kamati, hiii itawasiliana na serikali Kwa ajiri ya kutoa bajeti nchi nxima na ndio itakayoratibu kila sent inayotumika kwenye zoez na ndio itakayotoa taaarifa ya matumiz ya fedha hiii itasaidia kupunguza matumiz mabaya ya fedha pasipo hiii Kamati kila idara Au uongozi wa maeneo mbali mbali utatumia hela vibaya kwa kujificha kwenye mgongo wa covid -19 Kamati hiii ndio itakayokuwa inanunua vifaaa vyote na Kama kutahitajika Msaada wa serikali Kwa wananchi hiii Kamati ndio itakayohusika katika tathimini na ushauri na kusimamia

5.KAMATI YA TAARIFA NA UENEXI

hii ndio Kamati Ya kutoa taarifa tu, Kamati hiii itakuwa inatoa taarifa toka kwenye zile Kamati nne, kukiwa na taarifa inayotakiwa kutolewa na Kamati namba moja watapeleka taarifa yao huku, Kamati hiii ijumuishe wasemaji wa vyama vya siasa Kama vile pole Pole na Yule wa chadema

Mipango ni kuchagua, Serikali ikiamua kufuata hiii Kwa njia ya kisomi njoooni inbox Kama hamtaki ushauri basi fanyeni hivyo hivyo Kwa kuchanganya sukari na chumvi Kama tutafika
 
tabora kuna barabara mpya mkuu wa mkoa ameiita toronto mwaka jana aliita wamachinga wamejipanga hapo katikati ya mji kila jumamosi na jpili watu kujazana mpk huruma wameweka maji ya kunawa leo yapo kesho hakuna wangefikiria jinsi ya kutatuwa hili aisee hata kuwapa eneo kubwa wasikaribiane ...
 
Waliogopa kuwazuia wavhina wazungu wasiingie ndani ya nchi, sasa tuidome namba.Mwexi was Tano-Sita hall itakuwa tete sana.Serikali haina mbinu zoxote za maana.Makonda anasema watu waendelee tu na maisha yao.
 
Safi sana! Hivyo ndivyo ilitakiwa serikali ifanye tangu mwanzoni kabisa maambukizi yalipoanza.
 
Back
Top Bottom