Ili kuondokana na umasikini tunapaswa kupata viongozi wenye maono makubwa na uthubutu

mwanamichakato

JF-Expert Member
Mar 20, 2015
897
715
Nchi yetu bado ni maskini sana licha ya utajiri mkubwa sana wa rasilimali asilia (Madini, misitu, Ardhi, Maliasiri,n.k).

Hivyo ili kuondoka kwenye dimbwi na Korongo la umaskini tunapaswa kupata viongozi wenye maono makubwa sana na uthubutu ktk nyanja zote zinazohusu maamuzi yenye kubeba hatima ya wapi nchi itakuwa miaka 50 na 150 ijayo.

Mataifa yote yaliondelea haikuwa rahisi, lelemama, mdebwedo kufika walipofika..a lot of sacrifice has been taken. China, Singapore, Japan, Germany, UAE,etc. Tuache masihara ya kuchagua vyama, Marafiki, Ndugu, Jamaa, Marafiki. Vitengo vya nchi viwe imara. Vifanye comprehensive vetting/Scouting/Grooming/Diligence ya future leaders kwenye levels zote Kwa faida ya taifa. Usalama wa Taifa-Kielimu, Kisiasa, Kiuchumi, Kisayansi, Kiutamaduni..Inawezekana

Katiba ya nchi imeruhusu wenye Elimu ndogo kuweza kugombania na hatimae kuwa wabunge. Tuna wabunge wenye Elimu kubwa na maarifa mengi Lakini pia tuna Wabunge wenye Elimu Za chini, Uelewa Mdogo wa mambo ya dunia ya leo..

Vigezo vya michakato ya Chaguzi Za kisiasa ngazi ya vyama, Tume ya uchaguzi vina mapungufu mengi Kwa nafasi Za Serikali Za Mtaa, Udiwani hata ubunge.

Ni rahisi sana mtu kuwa au kushinda uchaguzi sababu ya umaarufu wake pekee pasipo kujali Mchango wake ktk fikra kubwa ya maendeleo chanya Kwa jamii husika,Kata,jimbo..etc.Michakato ya maendeleo inapatikana si Kwa kupiga domo,Wingi wa maneno,Siasa Za vitimbi na vioja.

Wawakirishi wa wananchi wanapaswa kuwa na maono makubwa sana juu ya utatuzi wa changamoto/Vigingi vya umaskini (Elimu,Afya,Miundombinu-Maji,Umeme,Barabara,Gesi;..Biashara,Uwekezaji,Viwanda,Kilimo,Uvuvi,Madini..

Maono ya wabunge hayapaswi kuwa kushinda uchaguzi kisha kupata ukwasi…Maono ya wabunge hayapaswi kuwa kupata uteuzi (Natamani Katiba ibadirishwe Mawaziri wasiwe Wabunge),Maono ya wabunge hayapaswi kuwa kuondokana na umaskini (Kuukata) sababu ya posho,marupurupu na viinua mgongo (Natamani vifutwe)..Maono ya wabunge hayapaswi kuwa kuwekwa kwenye kamati zenye ulaji..etc
KAMATI ZA BUNGE..
🦋Nini Majukumu ya kamati?
Nini faida ya kamati?

🦋Zimesaidia nini ktk kuondoa ufisadi/Unadhirifu/Uozo/Matumizi mabaya ya madaraka?

🦋Wanakamati ktk kamati husika wana weredi/Uzoefu/Ubunifu?

🦋Taifa linefaidika nini so far kupitia kamati husika?

🦋Wanakamati wa hizi kamati ni waadirifu?..Kipimo cha uadirifu kipo?

🦋Kuna vitengo vya ushauri wa wataalamu nyuma ya Hizi kamati?

🦋Nini umuhimu wa ziara ya kamati kwenye mashirika ya Umma,Mamlaka,Taasisi Za Umma?

🦋Ni kweli kwamba Kamati Za BUNGE Zinatumia mabilioni ya kodi mbali na posho,Marupurupu,Mishahara,nk wanayopata..?
 
utajiri una maana gani haumiliki? misitu yote imeshagawiwa wala siyo kuuzwa kugawiwa kwa waarabu na wizi na uporaji wa carbon credit, mbuga za wanyama ndiyo hizo wamasai wanafukuzwa kupisha emir wa emirat kuwinda, sasa utajiri gani huo unaouongelea? bandari ndiyo hizo zimeshakwenda kwa foreigners huko kwenye gesi ndiyo wala usiseme, visiwa vimekwenda, vitalu vya kuwinda vyote foreigners wanamiliki …
 
Hakuna mataifa yameendelea bila kuuana huyu ni ukweli mchungu, Kuna mzungu aliniambia usione kwao wanaheshimiana watu washauana sana mpaka heshima ikawepo.... Huko china,Singapore ambapo wamefanya revolution kubwa ukichaguliwa kua kiongozi wa serikali lazima tumbo licheze kidogo maana ukizingua kidogo tu watu wanakula kichwa

Hizi siasa za kubembelezana hatuwezi kufika mahali.... Serikali inatakiwa ipate watu watano wa juu kaliba la magu yaani hakuna kucheka na mtu
 
Nchi inapaswa kuwa na mwendelezo wa maraisi kama Hayat Magufulì kama miaka 20 tu, inatosha kabisa kuibadiri hii nchi na kuwa kama Singapore
 
Back
Top Bottom