Serikali Njombe wapiga marufuku shughuli zote za waganga wa kienyeji!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
34,116
2,000
Mkuu wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri pamoja na baraza la madiwani wamepiga marufuku shughuli zote za waganga wa kienyeji wenye leseni na wasio na leseni wakiwemo lambalamba na wapiga ramli.

Mkuu wa wilaya amesema mganga yeyote atakayekiuka agizo hilo hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Chanzo: ITV
 

Getstart

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
6,657
2,000
Hii ingefanyika mapema na nchi nzima. Lakini isiwe kwa waganga wa kienyeji kwa ujumla bali iwahusu wapiga ramli na wale wabajifanya kutambua wachai au kufufua mtu. Pamoja na utetezi wao kuwa kupiga ramli ni sawa na utafiti wa kimahabara, huu ni upuuzi.
 

S.Liondo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,400
2,000
Wapigwe marufuku Tanzania nzima. Hatuwahitaji hata kidogo. wabaki wataalam wa mitishamba tu.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,220
2,000
Tatizo sheria zetu huwa ni za kujionyesha tu mbele ya tv na kesho wao ndio wa kwanza kwenda kuzunguka mbuyu uchi
Huwa wanahuzunisha sana hawa so called wasomi
Ni wiki au mwezi halafu wanarudi tena kama zamani


Sent from my SM-G570F using Tapatalk
 

Uttarra

JF-Expert Member
Jan 5, 2019
397
1,000
Kupiga marufuku hii huko Njombe kutamaliza tatizo lililopo?

Waganga wa kuenyeji wakihamia Makete, Ikungi, Kibondo au Kongwa tatizo la mauaji litakua limehamia sehemu nyingine.

Hebu watafute suluhisho endelevu.
 

S.Liondo

JF-Expert Member
Apr 20, 2011
3,400
2,000
Hivi kuna tofauti kati ya wataalamu wa miti shamba na waganga wa kienyeji.
Kwangu mimi ninaposema waganga wa kienyeji ninamaanisha wale wanaotumia nguvu za giza kufanya mambo yao. Na wataalam wa miti shamba ni wale wajuzi wa tiba mbadala itokanayo na aina mbalimbali za mimea. Hicho ndicho nilichotaka kumaanisha.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom