Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,475
- 39,991
Tunaitaka ifanye hivi na ifanye vile; tunaitaka isifanye hivi au isifanye vile; tunataka viongozi wake wawe hivi au vile na tumefikia mahali pa kuibebesha mizigo ya kila aina; tunailaumu kwa ufisadi, tunailaumu kwa kushindwa kuchukua hatua mbalimbali. Wakati huo huo wapo wengine ambao wanataka tuimbe nyimbo za kuisifia serikali kuwa hatuoni kile ambacho "serikali imefanya" n.k
Serikali inatazamwa kama chombo cha aina fulani ambacho pasipo hicho mambo fulani hayafanyika au hayawezi kufanyika kwa ufanisi; hivyo serikali inatarajiwa kuhakikisha elimu ya juu iko nzuri, barabara nzuri, usalama wa raia, haki za wananchi, n.k n.k
Nimebaki kujiuliza hata hivyo serikali ni ya nini hasa?
Ni mambo gani ambayo serikali inatakiwa iyafanye na ambayo pasipo serikali hayawezi kufanyika? Ni mambo gani jukumu la sekta binafsi au vikundi binafsi vya watu na ni yapi ambayo ni jukumu la mtu mwenyewe?
Je tunaweza kutengeneza njia nzuri ya mafanikio na neema bila kuingiliwa sana na serikali au ni lazima tuihusishe serikali katika kila kitu?
Je serikali ni chachu ya maendeleo au ni kizuizi cha maendeleo hayo? Ni serikali ya namna gani ambayo inachochea maendeleo na ni ya namna gani inayazuia au kuyakwaza?
Tulipojiuliza wakati ule kuhusu vitu tunavyovihitaji ili tuendelee tulisema vitu vinne tu Watu, Ardhi, Siasa Safi na Uongozi bora; Katika maendeleo hayo hatukuksema tunamhitaji Mungu, Dini, Sayansi, Serikali, au kitu kingine. Je serikali ni kile kikolombwezo kinachonogesha mambo hayo mengine?
Bado sijapata majibu na ndio nimeanza kuyatafuta...