Serikali ni bora mfukuze watumishi wote kisha muanze upya kuajiri wale mnao wataka

Wakifukuza na kuanza kuajiri upya wataajiri kwa kadi za chama. Maana mkuu asivyopenda chadema anaweza kusema ajira serikalini kwa ajiri ya maccm tu.
 
Hadi 2020 hakutakuwa na waajiriwa wapya,ila kutakuwa na WASTAAFU WAPYA,bado kuna uhakiki wa NIDA,mishahara na takataka kibao,kwenye hiyo performance walim ndo watatolewa Kafara
 
Kila mwaka tunafanyiwa tathmini kwa kutumia OPRAS, bado hiyo haitoshi?
Mkikuta performance yangu ni 200% mtanilipa shilingi ngapi?
Acheni UKUDA huo...
Naona hata OPRAS imezingua wanashindwa kuitekeleza
 
Hao wanaofanyia wenzao tathimini wao wamejitathimini?wanaandaa njia za kulipana posho ilhali hao wanaotaka kuwatathimini wanamaisha ya aibu sana,hawa viongozi sijui wanawazaje Sielewi,sijaona hata anaekuja na wazo la kuboresha mazingira ya watumishi kila siku wanawaza kuwakomoa tu.
Kuna jamaa manispaa ya kinondoni ndo alikuwa akihakiki vyeti na matokeo yake amesombwa na Vyeti fake
 
Ana chosha.
Ongeza mshahara kwanza ndo uanzekunyanyasa wafanyakazi.
 
Huyo mwanamke ana roho mbaya
Huyu mama ni jinamizi!Ni kama wanataka mtumishi awe kama mfanyakazi wa kanjibhai.Niliona sehemu mtu kaajiriwa nesi duka LA dawa,walikosekana wateja anapewa kufua nguo za watoto.Anaambiwa huwezi kaa tu.Na dukani ukweli kiti ni cha bosi tu.Hutakiwi kukaa kuanzia asubuhi hadi saa 12 jioni.
 
unaogopa nini kufanyiwa tathmini? kwani wewe hutimizi wajibu wako? kwanini usifanyiwe tathmini? unaogopa nini? mbona private sector ni swala la kawaida? punguza deko
Huko serikalini wanapopanga jambo huwa hawafikirii kwa upana wake.Mf. OPRAS,kwa idara ya afya kuna shida sana kwa baadhi ya kada.Mf. mtu yuko famasi,kila Siku dawa hakuna,na serikali ndiyo haijaleta dawa,sasa hawa watu unawapimaje performance yao?Sana sana ninachokiona ni watu kupandishwa kindugu na aidha utoe rushwa.Wanaopanda kirahisi ni wale wanaotoa chanjo mfano.Yeye atasema niliweka lengo la kutoa chanjo kwa watu kadhaa,na nimevuka lengo kwa asilimia kadhaa.Ukweli mipango mingi inaongeza mianya ya uonevu tu na kufaidisha watu wachache.Mungu yupo lakini
 
Lakini, ukitizama kwa undani, hili jambo linaukweli, watumishi wengine hawafanyi kazi, wengine hawakai hata vituoni , akiguswa anadai anamiradi yake!, sasa kwa namna hiyo inakuwa kero sana kwa wengine, na wasimamizi wa kituo, sasa hivi ni mtu kwa mtu, safu. Napongeza hilo, ila sasa waweke maslahi mazuri wasilete mbwembwe
 
unaogopa nini kufanyiwa tathmini? kwani wewe hutimizi wajibu wako? kwanini usifanyiwe tathmini? unaogopa nini? mbona private sector ni swala la kawaida? punguza deko
Private sekta unaifahamu au umesimuliwa? Yaani huko tathimini inaenda na malipo ya fedha sasa huko government malipo yanachekesha
 
Back
Top Bottom