Serikali na CCM acheni kumpa Tundu Lissu umaarufu wa bure!

lakini kwa vile hakuna mwenye akili kwa sasa serikalini na Chamani Bali nguvu ndo dira waliacha njia hii na wakaweka katazo la kumtembelea Lissu. Acha wavune matunda ya upumbavu wao maana ushauri wako kwa sasa hauwasaidii zaidi ya kuwafanya waonekane wahusika zaidi. Chochote wanachokifanya kwa sasa kinawadidimiza zaidi kwenye shimo la uhisika. Waliyakoroga ni wajibu wao kuyanywa.
Akili wanazo, wanaangalia Mkubwa anataka nini , wanaangalia midomo ya Dictator inacheza vipi, short of that "hawatakwenda chooni". Akili wanayo sana tena sana! Ila waliopanga shambulio, hao akili ziliwatoka! Lisu is smart, atayaanika yote mpaka ICC, na i can assure you, watakuja hapa, it is amatter of time!
 
Mkuu umefanya uchambuzi mzuri sana ila nguvu uliyotumia kufanya uchambuzi juu ya shambulio la Lissu ungeuelekeza kushauri Serekali nini kifanyike juu ya shiling yetu kuanguka kwa dolla au Kushauri Serekali nini cha kufanya kufufua uchumi wa nchi yetu ningefurahi sana kwasabubu wananchi tunaumia sana mtaani maisha ni magumu sana matatizo yamefika kiwangu cha juu sana kupita maelezo na haya matatizo niyakupanga sio bahati mbaya tuliambwia mapema kua jero itaitwa miatano, Malumba ya Lissu na Serekali hana tija kwetu sisi wajasiriamali
 
Msikilize tena Lissu, amesema ccm siyo chama cha siasa bali ni chama dola na uhai wake unategemea dola, yaani viongozi wake ni raisi, wanajeshi, polisi, etc. In simple plain language, ccm= raisi, polisi, jeshi, tbc, yaani hivyo vyombo sijui vya kiuchunguzi na ccm ni kitu moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Spika ameshaweka bayana, watajibu kila tuhuma au maneno ya TL.

Wanaanzaje kunyamaza wakati wanajua walichokifanya? Wakiusikiliza ushauri wako watapunguza kiwango cha uharibifu lakini sio kufuta kabisa doa la serikali kuhusu TL.

Yesu alinyamaza mbele ya washtaki wake kwakuwa hakua na hatia.
Serikali kuyuhumuwa sio jambo geni lakini majibu ya serikali huwa ndio mageni.

Hakuna serikali hapa duniani haijawahi kutuhumuwa kuua au kutaka kuua.

Nimesema hata kukaa kimya nalo ni jibu.
 
Msikilize tena Lissu, amesema ccm siyo chama cha siasa bali ni chama dola na uhai wake unategemea dola, yaani viongozi wake ni raisi, wanajeshi, polisi, etc. In simple plain language, ccm= raisi, polisi, jeshi, tbc, yaani hivyo vyombo sijui vya kiuchunguzi na ccm ni kitu moja

Sent using Jamii Forums mobile app
Yeye ubunge alishindaje katika mfumo huo na kama nchi haina demokrasia na haiheshimu.sheria aliwezaje kuwa mbunge?
 
Ukishaanza kukiogopa kimvuli chako mwenyewe hakuna kitu utaacha kukiogopa.

Lakini pia kukaa kimya ni kiashirio kikubwa kuwa kile kinachosemwa ni kweli. Na utakapojibu ndipo itajulikana ukweli zaidi kutokana na majibu utakayojibu.

Mpaka wao wameamua kumjibu sidhani kama walikurupuka tu, ila naamini walishakaa chini wakajadiliana na wakaafikiana wafanye hivyo.

Ila mwisho wa siku, siku zote daima milele panapo ukweli uongo hukaa pembeni.

Ahsante.
Kuliko kujibu upuuzi ni bora kukaa kimya

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa kimya na mtazamaji kuhusiana na suala hili la Tundu Lissu lakini baada ya kuangalia kwa muda nimegundua madhaifu mengi sana kwa upande wa serikali katika kukabiliana na yanayojiri kwenye suala hili.

Serikali na CCM wamekuwa reactive badala ya kuwa proactive ambapo matokeo yake wanafanya makosa mengi ya msingi hasa mahusiano ya umma.

Serikali na viongozi wa juu wa CCM kukimbizana na Lissu kwenye vyombo vya habari ili kujibu hoja zake ni ujinga wa kiwango cha juu kwa sababu kufanya hivyo ni kujiweka wazi kwenye maswali ambayo hanaya majibu ya kisiasa bali kiuchunguzi. Kimantiki taasisi ya kiuchunguzi wa makosa ya jinai haiwezi kutoa majibu ya uchunguzi kama uchunguzi haujakamilika lakini pia hata yakitolewa huwa yanatolewa kitaalam na kwa uangalifu mkubwa sana bila kujali mwathirika/waathirika wanafikra zipi.

Lissu akiwa anahojiwa na waandishi wa habari bila kuwepo maafisa wa serikali ni faida kwa serikali na CCM kuliko ofisa wa serikali na CCM kuwepo pia katika mahojiano hayo. Mahojiano yake katika kipindi cha HARDtalk bila uwepo wa ofisa wa serikali yaliinufaisha zaidi serikali kuliko muhojiwa. Hata pale alipotoa shutuma, mtangazaji alimwambia aache kutoa shutuma ambazo anaowatuhumu hawapo ili wazijibu.

Ni ujinga kwa serikali kudhani kuwa kinachofanyika hapa Tanzania hakijulikani katika makorido ya watawala wa Ulaya na Marekani na kwa maana hiyo wanakwenda kujibu tuhuma za upotoshaji. In fact, watawala wa Ulaya na Marekani wanajua hata yale yanayosemwa ndani ya Ikulu ya Magogoni nchini achilia mbali anayoyasema Lissu. Kwa maana hii, kama Lissu anayosema ni kweli au uwongo watakuwa wanajua.

Kwa mfano, juzi Gazeti la The New York Times la Marekani ambalo lina mahusiano ya karibu sana na majasusi wa Marekani lilipewa audio yenye maongezi ya mwana mfalme, Mohammed bin Salman akiwaambia watu wake wa karibu kuwa atatumia risasi kama Jamal Khashoggi hatarudi Saudi Arabia na kuachana na ukosoaji wa serikali. Hii inaonyesha kuwa kila anachokisema na kukifanya ndani ya nyumba yake kinajulikana kwa majasusi wa nchi ya Marekani.

Hii ina maana kuwa serikali inapoteza muda kujitetea kwenye suala la Tundu Lissu na demokrasia kwa sababu watawala wa Ulaya na Marekani wanajua kama ni kweli au uwongo.

Serikali lazima waelewe kuwa anachokitaka Tundu Lissu ni reaction ambayo ni reactive kutoka serikalini ili aendeleze marumbano na mijadala kwenye vyombo vya habari ya ndani na nje.

Ninakumbuka kwa mara yangu ya kwanza kusafiri katika nchi za Ulaya nilipewa ushauri kuwa ukimuona mtu anakuchokoza au kukuchochea unachotakiwa ni kutoonyesha hisia au kujibu. Kutoonyesha hisia au kujibu kutamfanya akose sababu ya kuendelea kukuchochea au kukuchokoza lakini kikubwa zaidi ataona anachofanya ni ujinga na kuachana na uchochezi au uchokozi.

Serikali ikikaa kimya hata wale wanaomuhoji Lissu watachoka kwa sababu kutakuwa hakuna reaction kutoka serikalini. Kukosa reaction kutoka serikalini ina maana hata mahojiano yanakuwa hayahitajiki (redundant). Serikali lazima waelewe dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction lakini kikubwa zaidi uendeshaji wa serikali ni sawa na mbio za masafa marefu(marathon). Kuna wapiga kelele wataibuka na baadaye watapotea.

Watu wenye fikra pana wanaomfahamu Lissu hawashangai na kile anachokisema bali wanachoshangaa ni jinsi ambavyo viongozi wa juu wa CCM na serikali wanavyojibishana naye kwenye vyombo vya habari.

Kwa mtu mwenye fikra pana na anamfahamu vizuri Lissu atajua hupenda sana kujionyesha mbele ya watu/hadhara (limelight) lakini pia hufurahia sana (relish) kama kuna reaction bila kujali kama ni nzuri au mbaya. Waingereza huita Attention seeking behaviour. Lissu anachokitafuta kwa CCM na serikali ni kukimbizana au kujibishana naye kwenye media akiwa ndiye focal point.

Mpaka sasa malengo yake kwa kiwango kikubwa yamefanikiwa kutokana na ujinga wa viongozi wa juu wa serikali na CCM ambao wengi wao hawajui ukubwa na umuhimu wa vyeo vyao. Eti Katibu Mkuu wa chama tawala CCM anajibishana na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu? This is beyond stupidity.

Lissu anatakiwa arumbane na wanachama wa kawaida wa CCM na sio viongozi wa juu wa chama. Majibu ya hoja za Lissu kuhusu shambulio lazima yajibiwe na taasisi rasmi za uchunguzi na sio kila kiongozi wa serikali.

Hawa viongozi wa CCM na serikali hawakujifunza makosa waliyoyafanya kwa Mange Kimambi baada ya kumkuza na kupata followers wengi kutokana na kujibishana naye. Makosa yaleyale wanayarudia kwa Tundu Lissu.

Katika dhana ile ile ya Attention seeking behaviour, Ninajua pia Lissu atapenda sana akirudi nchini akamatwe akiwa uwanja wa ndege ili kutimiza Newton's third law of motion ambapo matokeo yake yatakuwa kumpa umaarufu wa bure lakini kikubwa zaidi hata waliokuwa hawaamini aliyokuwa anayasema nwataamini niya kweli. Ninawaomba sana serikali wasimkamate siku akiingia nchini bali wamuache tu. No force, no rection.

Ninakumbuka mwaka 1995 wakati Augustino Mrema akiwa mpinzani maarufu nchini, kila alipobebwa waliombeba walipigwa mabomu na vitendo hivyo vilizidi kumfanya maarufu mpaka Mwalimu Nyerere alipotumia busara na kuwambia polisi, “Kwa kuwa wanaotaka kumbeba Mrema wapo, waacheni wambebe. Wambebe hata kama watakuwa wanapokezana kama machela (jeneza), waacheni.” Polisi walipotii agizo la Baba wa Taifa, la kuacha kuwapiga mabomu, Mrema naye kama shani hakubebwa tena. Mwl. Nyerere alitumia dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction.

Tuliona pia huko Kenya, baada ya wapinzani kuamua kumuapisha Raila Odinga kuongoza Kenya baada kutangaza kwamba hamtambui Uhuru Kenyatta kama kiongozi aliyechaguliwa kwa njia halali, polisi waliwaacha wafanye hivyo na matokeo yake kitendo hicho kikaonekana nicha kijinga.

Huko Venezuela tumeona kiongozi wa upinzani akifanya kama alivyofanya Raila Odinga lakini dhumuni lake lilikuwa ni kutaka polisi wawazuie ili mapigano yatokee ambayo yangekuwa ni sababu ya Marekani kuingia kimabavu katika nchi hiyo kwa kisingizio cha kuzuia mauwaji. Serikali ya Rais Madulo ikajua janja yao na ikamuacha Juan Guaidó ajiapishe bila kumuingilia kwa kutumia nguvu ya polisi/jeshi. No force, no reaction. Uamuzi wa polisi/jeshi kumuacha ajiapishe kumeua malengo ya Marekani ya kuingiza majeshi Venezuela.

CCM na Serikali lazima waelewe kuwa hoja sio Lissu anatumiwa na ''mabeberu'' bali hoja ni jinsi gani wataweza kuzuia njama za ''Mabeberu'' kwa sababu ''mabeberu'' kuwatumia watu sio jambo jimpya.

Kuna Mzee mmoja aliwahi kunipa ushauri kwa maneno haya, Ukimya hukuvisha nguo ya utulivu na hukukinga na haja ya kutoa visingizio lakini pia jawabu fasihi kabisa kwa mpumbavu ni kutomjibu.

Nimalizie kwa kusema, Serikali na viongozi wa juu wa CCM lazima watambue kuwa hata kukaa kimya ni jibu kwa sababu hakuna serikali hapa duniani ambayo haijawahi kutuhumiwa kutaka kuua au kuua raia.

Ushauri mzuri kwa watu waelewa. Lakini uliowaambia ni waelewa? Wangekuwa waelewa wasingefanya hayo waliyoyafanya hadi leo wawe wanajaribu kuzima moto kwa petroli. Ila umekosea kidogo jambo moja; attention seeker anaejulikana namba moja nchi hii sio Lissu, ni Magufuli. Au umesahau kuwa plan yake ni kuwa "kiongozi wa malaika"? Unadhani ni kwa nini kila mteule husema "serikali hii inayoongozwa na mpendwa wetu Rais Dr John Joseph Pombe Magufuli" with no variations or exceptions?

Na ushukuru Mungu wewe sio verified user la sivyo ungekiona cha moto kutokana na bandiko lako hili.
 
Hoja yangu sio kumjibu bali kumjibu nini na kwa faida ya nani?

Labda nikuulize kama wanaomjibu ndio waliomshambulia, wanamjibu ili iweje? Kwamba Marekani na Ulaya watajua kuwa sio wao waliomshambulia?

Wanajitetea kuua soo ili ukweli usizidi kuenda maana wanajua raia wanawaogopa na hakuna mwenye uthubutu wa kuhoji, na ukihoji wanakubambikizia kesi na kipigo juu.
 
Yeye ubunge alishindaje katika mfumo huo na kama nchi haina demokrasia na haiheshimu.sheria aliwezaje kuwa mbunge?

Are you so dumb to understand the concept of time? Aliposhinda ubunge Rais alikuwa Magufuli? Ina maana circumstances zilizopo leo zilikuwepo wakati uchaguzi unafanyika na Lissu akashinda?
 
Vyombo vya kiuchunguzi vitajibu nini wakati mmevizuia kufanya uchunguzi?

Serikali ndio inapaswa kujitetea kwani ndio yenye dhamana ya kulinda uhai na mali za watu kupitia Jeshi la Polisi.

Isotoshe hamna majibu wala hoja za kujibu hoja za Lissu na ndio maana mnaumbuka.

Na huyo Katibu Mkuu wa chama chako kimataifa anafunikiwa vibaya sana na Lissu na hata hapa ndani ya nchi Lissu ni maarufuku kuliko Bushiru.

Eleweni Jiwe ni zero kichwani kwani anatumia nguvu, ubabe na zaidi anaongozwa na chuki kuliko busara na maarifa katika maamuzi yake na matokeo yake ndio haya ya yeye kuaibika na kuumbuka.
 
Leo msema kweli umepandisha uzi kama mwana CCM na muunga mkono serikali ila alie na fikra huru, hongera sana tungekuwa siku zote tunajadili vitu kwa ujuzi kama hivi taifa lingesonga tu.
 
Umeandika mengi lakini umesukumwa zaidi na mapenzi kwa chama tawala, unaweza kupuuza au kutomjibu mtu kama anachosema ni uongo, lakini kama mambo mengi yanayodaiwa ni ya kweli utajitahidi kukanusha kwa kuwa hata kama ni uongo ukisemwa kwa muda mrefu unakuwa ukweli na hili serikali inalijua.
Pili mimi nataka msikae kimya mkanushe kwa kujibu hoja, kwa mfano anasema Magufuli anaminya demokrasia, sasa nyinyi mnatakiwa mtuonyeshe ni kwa kiwango gani Magufuli ametanua demokrasia kwa watu. Anasema anafanya manunuzi bila kufuata sheria ya manunuzi, tuonyesheni ni kwa namna gani mchakato wa manunuzi ulifanyika na bunge kushiriki. Anasema mlikula pesa za tetemeko Bukoba, tuonyeshe ni namna gani waathirika walipata pesa. Mambo yako mengi sana. Wewe unashauri wakae kimya huo ni ushauri wa ovyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom