Serikali na CCM acheni kumpa Tundu Lissu umaarufu wa bure!

Ni ushauri wenye mantiki kwa serikali, kosa kubwa lililofanyika toka mwanzo ni kujiangaisha na mpuuzi kama Tundu Lissu, ni mtu anayetafuta sifa binafsi kwa masllahi yake, anaungwa mkono na wapiuuzi wachache wasioipend serikali. Serikali iachane kujishughulisha naye.

Sent using Jamii Forums mobile app

Kwa tafsiri yako mtu asipoipenda serikali ni mpuuzi!?
 
Ukishaanza kukiogopa kimvuli chako mwenyewe hakuna kitu utaacha kukiogopa.

Lakini pia kukaa kimya ni kiashirio kikubwa kuwa kile kinachosemwa ni kweli. Na utakapojibu ndipo itajulikana ukweli zaidi kutokana na majibu utakayojibu.

Mpaka wao wameamua kumjibu sidhani kama walikurupuka tu, ila naamini walishakaa chini wakajadiliana na wakaafikiana wafanye hivyo.

Ila mwisho wa siku, siku zote daima milele panapo ukweli uongo hukaa pembeni.

Ahsante.
Ninachosema majibu kuhusu hoja za Lissu za shambulio yanatakiwa yatolewe na wataalam wa taasisi ya kiuchunguzi ambayo ina msemaji wake.

Ni ujinga kumuona Waziri wa mambo ya ndani akijibu hoja za kiuchunguzi wakati yeye wala sio msemaji rasmi wa taasisi hiyo.

Ni upumbavu kumuona Katibu Mkuu wa CCM akijibishana na Tundu Lissu wakati yeye msimamizi wa shughuri za chama. Anachotakiwa ni kuimiza serikali kutoa majibu kuhusu suala la Tundu Lissu na sio kuwa msemaji wa serikali.
 
Mkuu mwenyewe juzi nimeliongea hili, NI UPUMBAVU KIWANGO CHA SGR kwa viongoz wa serikali kujibishana na Lisu. Lisu hatafuti majibu nani kampiga Risasi coz kila siku anawataja na kutoa kejeli na dhihaka kibao. Lisu nao anataka MAJIBISHANO aendelee kupata KIKI.Hakuna jibu lolote Lisu atapewa ye na wafuasi wake wakakubali bila ya suspects wake kutajwa. Yaani tayari wana majibu yote ya uchunguz mfukoni. Ni mambo ya kipumbavu kwa kiongoz wa serikali asiye ma taaluma yyt ya kipelelezi na hausiki na jeshi la polisi kumjibu lisu. Nafikiri jpm kazungukwa na VILAZA wengi kiasi kushindwa kumsaidia pale panapohitajika msaada wa maana na kazungukwa na watu ambao nao wanapenda kiki za kisiasa na sio weledi. Swala la lisu kila kiongoz anataka kujionesha naye kasaidia serikali ili Mwisho kama ni cheo au favour flani apate kutoka kwa mkulu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Kabisa! Na hapo ndio mnadhibitisha ya kuwa JPM ni kilaza kwa kuwa kazungukwa na VILAZA !

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ninachosema majibu kuhusu hoja za Lissu za shambulio yanatakiwa yatolewe na wataalam wa taasisi ya kiuchunguzi ambayo ina msemaji wake.

Ni ujinga kumuona Waziri wa mambo ya ndani akijibu hoja za kiuchunguzi wakati yeye wala sio msemaji rasmi wa taasisi hiyo.

Ni upumbavu kumuona Katibu Mkuu wa CCM akijibishana na Tundu Lissu wakati yeye msimamizi wa shughuri za chama. Anachotakiwa ni kuimiza serikali kutoa majibu kuhusu suala la Tundu Lissu na sio kuwa msemaji wa serikali.

Jibu lako lipo paragraph ya 3 kwenye hiyo post uliyoi-quote.

Soma tu kwa utulivu utaelewa.

Ahsante.
 
Mkuu mwenyewe juzi nimeliongea hili, NI UPUMBAVU KIWANGO CHA SGR kwa viongoz wa serikali kujibishana na Lisu. Lisu hatafuti majibu nani kampiga Risasi coz kila siku anawataja na kutoa kejeli na dhihaka kibao. Lisu nao anataka MAJIBISHANO aendelee kupata KIKI.Hakuna jibu lolote Lisu atapewa ye na wafuasi wake wakakubali bila ya suspects wake kutajwa. Yaani tayari wana majibu yote ya uchunguz mfukoni. Ni mambo ya kipumbavu kwa kiongoz wa serikali asiye ma taaluma yyt ya kipelelezi na hausiki na jeshi la polisi kumjibu lisu. Nafikiri jpm kazungukwa na VILAZA wengi kiasi kushindwa kumsaidia pale panapohitajika msaada wa maana na kazungukwa na watu ambao nao wanapenda kiki za kisiasa na sio weledi. Swala la lisu kila kiongoz anataka kujionesha naye kasaidia serikali ili Mwisho kama ni cheo au favour flani apate kutoka kwa mkulu.

The problem with the world is that the intelligent people are full of doubts, while the stupid ones are full ofconfidence.
Ninashukuru Mkuu kama uliwaza kama mimi.

Mimi nimekuwa msomaji katika sakata hili ambapo nimegundua tatizo kubwa sana ndani ya chama na serikali kuhusu mahusiano ya umma.
 
Nimekuwa kimya na mtazamaji kuhusiana na suala hili la Tundu Lissu lakini baada ya kuangalia kwa muda nimegundua madhaifu mengi sana kwa upande wa serikali katika kukabiliana na yanayojiri kwenye suala hili.

Serikali na CCM wamekuwa reactive badala ya kuwa proactive ambapo matokeo yake wanafanya makosa mengi ya msingi hasa mahusiano ya umma.

Serikali na viongozi wa juu wa CCM kukimbizana na Lissu kwenye vyombo vya habari ili kujibu hoja zake ni ujinga wa kiwango cha juu kwa sababu kufanya hivyo ni kujiweka wazi kwenye maswali ambayo hanaya majibu ya kisiasa bali kiuchunguzi. Kimantiki taasisi ya kiuchunguzi wa makosa ya jinai haiwezi kutoa majibu ya uchunguzi kama uchunguzi haujakamilika lakini pia hata yakitolewa huwa yanatolewa kitaalam na kwa uangalifu mkubwa sana bila kujali mwathirika/waathirika wanafikra zipi.

Lissu akiwa anahojiwa na waandishi wa habari bila kuwepo maafisa wa serikali ni faida kwa serikali na CCM kuliko ofisa wa serikali na CCM kuwepo pia katika mahojiano hayo. Mahojiano yake katika kipindi cha HARDtalk bila uwepo wa ofisa wa serikali yaliinufaisha zaidi serikali kuliko muhojiwa. Hata pale alipotoa shutuma, mtangazaji alimwambia aache kutoa shutuma ambazo anaowatuhumu hawapo ili wazijibu.

Ni ujinga kwa serikali kudhani kuwa kinachofanyika hapa Tanzania hakijulikani katika makorido ya watawala wa Ulaya na Marekani na kwa maana hiyo wanakwenda kujibu tuhuma za upotoshaji. In fact, watawala wa Ulaya na Marekani wanajua hata yale yanayosemwa ndani ya Ikulu ya Magogoni nchini achilia mbali anayoyasema Lissu. Kwa maana hii, kama Lissu anayosema ni kweli au uwongo watakuwa wanajua.

Kwa mfano, juzi Gazeti la The New York Times la Marekani ambalo lina mahusiano ya karibu sana na majasusi wa Marekani lilipewa audio yenye maongezi ya mwana mfalme, Mohammed bin Salman akiwaambia watu wake wa karibu kuwa atatumia risasi kama Jamal Khashoggi hatarudi Saudi Arabia na kuachana na ukosoaji wa serikali. Hii inaonyesha kuwa kila anachokisema na kukifanya ndani ya nyumba yake kinajulikana kwa majasusi wa nchi ya Marekani.

Hii ina maana kuwa serikali inapoteza muda kujitetea kwenye suala la Tundu Lissu na demokrasia kwa sababu watawala wa Ulaya na Marekani wanajua kama ni kweli au uwongo.

Serikali lazima waelewe kuwa anachokitaka Tundu Lissu ni reaction ambayo ni reactive kutoka serikalini ili aendeleze marumbano na mijadala kwenye vyombo vya habari ya ndani na nje.

Ninakumbuka kwa mara yangu ya kwanza kusafiri katika nchi za Ulaya nilipewa ushauri kuwa ukimuona mtu anakuchokoza au kukuchochea unachotakiwa ni kutoonyesha hisia au kujibu. Kutoonyesha hisia au kujibu kutamfanya akose sababu ya kuendelea kukuchochea au kukuchokoza lakini kikubwa zaidi ataona anachofanya ni ujinga na kuachana na uchochezi au uchokozi.

Serikali ikikaa kimya hata wale wanaomuhoji Lissu watachoka kwa sababu kutakuwa hakuna reaction kutoka serikalini. Kukosa reaction kutoka serikalini ina maana hata mahojiano yanakuwa hayahitajiki (redundant). Serikali lazima waelewe dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction lakini kikubwa zaidi uendeshaji wa serikali ni sawa na mbio za masafa marefu(marathon). Kuna wapiga kelele wataibuka na baadaye watapotea.

Watu wenye fikra pana wanaomfahamu Lissu hawashangai na kile anachokisema bali wanachoshangaa ni jinsi ambavyo viongozi wa juu wa CCM na serikali wanavyojibishana naye kwenye vyombo vya habari.

Kwa mtu mwenye fikra pana na anamfahamu vizuri Lissu atajua hupenda sana kujionyesha mbele ya watu/hadhara (limelight) lakini pia hufurahia sana (relish) kama kuna reaction bila kujali kama ni nzuri au mbaya. Waingereza huita Attention seeking behaviour. Lissu anachokitafuta kwa CCM na serikali ni kukimbizana au kujibishana naye kwenye media akiwa ndiye focal point.

Mpaka sasa malengo yake kwa kiwango kikubwa yamefanikiwa kutokana na ujinga wa viongozi wa juu wa serikali na CCM ambao wengi wao hawajui ukubwa na umuhimu wa vyeo vyao. Eti Katibu Mkuu wa chama tawala CCM anajibishana na Mjumbe wa Kamati Kuu wa chama cha upinzani CHADEMA, Tundu Lissu? This is beyond stupidity.

Lissu anatakiwa arumbane na wanachama wa kawaida wa CCM na sio viongozi wa juu wa chama. Majibu ya hoja za Lissu kuhusu shambulio lazima yajibiwe na taasisi rasmi za uchunguzi na sio kila kiongozi wa serikali.

Hawa viongozi wa CCM na serikali hawakujifunza makosa waliyoyafanya kwa Mange Kimambi baada ya kumkuza na kupata followers wengi kutokana na kujibishana naye. Makosa yaleyale wanayarudia kwa Tundu Lissu.

Katika dhana ile ile ya Attention seeking behaviour, Ninajua pia Lissu atapenda sana akirudi nchini akamatwe akiwa uwanja wa ndege ili kutimiza Newton's third law of motion ambapo matokeo yake yatakuwa kumpa umaarufu wa bure lakini kikubwa zaidi hata waliokuwa hawaamini aliyokuwa anayasema nwataamini niya kweli. Ninawaomba sana serikali wasimkamate siku akiingia nchini bali wamuache tu. No force, no rection.

Ninakumbuka mwaka 1995 wakati Augustino Mrema akiwa mpinzani maarufu nchini, kila alipobebwa waliombeba walipigwa mabomu na vitendo hivyo vilizidi kumfanya maarufu mpaka Mwalimu Nyerere alipotumia busara na kuwambia polisi, “Kwa kuwa wanaotaka kumbeba Mrema wapo, waacheni wambebe. Wambebe hata kama watakuwa wanapokezana kama machela (jeneza), waacheni.” Polisi walipotii agizo la Baba wa Taifa, la kuacha kuwapiga mabomu, Mrema naye kama shani hakubebwa tena. Mwl. Nyerere alitumia dhana ya Newton's third law of motion. No force, no reaction.

Tuliona pia huko Kenya, baada ya wapinzani kuamua kumuapisha Raila Odinga kuongoza Kenya baada kutangaza kwamba hamtambui Uhuru Kenyatta kama kiongozi aliyechaguliwa kwa njia halali, polisi waliwaacha wafanye hivyo na matokeo yake kitendo hicho kikaonekana nicha kijinga.

Huko Venezuela tumeona kiongozi wa upinzani akifanya kama alivyofanya Raila Odinga lakini dhumuni lake lilikuwa ni kutaka polisi wawazuie ili mapigano yatokee ambayo yangekuwa ni sababu ya Marekani kuingia kimabavu katika nchi hiyo kwa kisingizio cha kuzuia mauwaji. Serikali ya Rais Madulo ikajua janja yao na ikamuacha Juan Guaidó ajiapishe bila kumuingilia kwa kutumia nguvu ya polisi/jeshi. No force, no reaction. Uamuzi wa polisi/jeshi kumuacha ajiapishe kumeua malengo ya Marekani ya kuingiza majeshi Venezuela.

CCM na Serikali lazima waelewe kuwa hoja sio Lissu anatumiwa na ''mabeberu'' bali hoja ni jinsi gani wataweza kuzuia njama za ''Mabeberu'' kwa sababu ''mabeberu'' kuwatumia watu sio jambo jimpya.

Kuna Mzee mmoja aliwahi kunipa ushauri kwa maneno haya, Ukimya hukuvisha nguo ya utulivu na hukukinga na haja ya kutoa visingizio lakini pia jawabu fasihi kabisa kwa mpumbavu ni kutomjibu.

Nimalizie kwa kusema, Serikali na viongozi wa juu wa CCM lazima watambue kuwa hata kukaa kimya ni jibu.
Well said Mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jaribu kufanya jambo, kisha uliyemfanyia awe anakutangaza uone kama utakaa kimya. Unasema hivyo maana hukushirikishwa kwenye ye shambulio lake. Hao wanaomjibu ndio waliomshambulia.
Hoja yangu sio kumjibu bali kumjibu nini na kwa faida ya nani?

Labda nikuulize kama wanaomjibu ndio waliomshambulia, wanamjibu ili iweje? Kwamba Marekani na Ulaya watajua kuwa sio wao waliomshambulia?
 
Umeandika vizuri lakini kuna usemi wa kizungu unaosema "Silence means Yes" (kukaa kimya maana yake unakubali kinachosemwa,tafsiri isiyo rasmi) sasa wewe unasemaje "kuwa hata kukaa kimya ni jibu"unamaanisha jibu la ndiyo?:Lazima Serikali ijibu mapigo sisi back benchers tutaamua.
Alisema kwanini serikali ikae kimya sababu,ametoa sababu kuwa hao alikoenda kushitiki Lisu hao mabeberu wanajua kila kitu katika korido zetu
 
Spika ameshaweka bayana, watajibu kila tuhuma au maneno ya TL.

Wanaanzaje kunyamaza wakati wanajua walichokifanya? Wakiusikiliza ushauri wako watapunguza kiwango cha uharibifu lakini sio kufuta kabisa doa la serikali kuhusu TL.

Yesu alinyamaza mbele ya washtaki wake kwakuwa hakua na hatia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom