Serikali: Marufuku kufukuza wanafunzi shule binafsi wanaofeli wastani

Malisa leo nimekudharau kabisa, unaandika ujumbe mreeefu lakin unashundwa kutambua mantiki nzima ya waraka wa serikali kuwazuia shule binafsi kukaririsha, kuhamisha au kufukuza wanafunzi walioshindwa kufikia wastan waliouweka wao kama shule.

Mchujo utakuwepo darasa la nne, na form two, na ni kwa wastan uliopangwa na serikali. sio kama wewe unayepotosha eti wamewaruhusu wenye wastan wa 12% kuendelea na masomo. unajua kuwa hata huo wastan wa serikali ni zaidi ya 12% kwa form two na darasa na nne, lakin umeamua kupotosha tu kwa sababu zako za kisiasa. Wanafunzi wasiofikia wastan uliopangwa na serikali, iwe darasa la nne au form two, watakariri darasa. Na hii ni kwa shule zote, serikali na binafsi.

kumekuwepo na kasumba kwa hizi shule binafsi kuwafukuza au kuwakaririsha madarasa wanafunzi wasiofikia wastani wa shule zao, let say 60%. Hii imezua malalamiko miongoni mwa wazazi na walezi kuwaongezea gharama na usumbufu. unakuta mwanafunzi kafikisha 55%, anakaririshwa darasa, wakati kama angeendelea na form three na wastan huo huo angepata div two au three. sasa tujiulize, kwa jamii yetu div three na four hazitakiwi kabisa??? mbona hawa wameendelea na vyuo na kuwa waalimu, manesi, maskali, mafundi mchundo na wanasaidia sana jamii zetu??

Huu ulikuwa ni ujanja wa shule binafsi kujiona wao wanafundisha sana, kumbe wanachojua ni kuchuja tu wabaki na vipanga ili kwenye mitihani ya kitaifa wapate div one na two ili kujipandishia ada . lets have a fair ground.. hapo tutajua mbichi na mbivu. kama mnajua kweli kufundisha, mfundisheni aliyepata wastani wa 35% naye apate div one au two. hapo ndo tutajua ninyi si watu wa mchezo mchezo. pandisheni ada mtakavyo.... lakin si kuwafukuza waliopata zaidi ya 35%.

Ukweli ndio huo.
Kuna wapinzani uchwara wanaotaka kupinga na kupotosha hata mambo mazuri yanayofanywa na serikali.

Kuna shule moja wastani wake ni 85 ili mtoto ahamie pale.
Hawa hawana lolote zaidi ya kuwachuja wanafunzi na kubakiwa na wale wenye akili zao za kuzaliwa.

Hebu tufikiri kido kama Serikali nayo ingewachuja wanafunzi wake kwa namna hiyo hiyo ingekuwaje na ni wangapi wangepata elimu?

Ukiangalia hizi shule zinaandaa watu tegemezi tu wa kuajiiriwa ndio maana huwezi kuwaona huko kwenye ajira binafsi wakiwa na makampuni yao kama akina Mengi ,Anthony Dialo na Mo. Wanaandaa watu wa aina moja tu wa kukariri Darasani wakati Taifa linajengwa na watu wenye vipaji mbali mbali.

Kazi ya serikali ni kuweka wastani wa chini wa mwanafunzi kufaulu.

Ni wajibu wa shule kuzingatia wastani wa serikali.

Zamani shule za private ndizo zilizokuwa zinachukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu.

Shule za binafsi zimelenga biashara.

Ila nailamu zaidi serikali ya Chama chetu cha mapinduzi kwa kupelekwa na wapinzani kama upepo na hofu ya kushindwa uchaguzi hali inayopelekea kukurupuka kwenye kila sekta. Wapinzani walianza kusema kuwa watatoa elimu bure kwenye kampeni za mwaka 2005 na 2010. CCM kwa woga wa kushindwa japo hata kama wangeshindwa wasingeachia madaraka nao wakaiga na kuja na sera hii inayodidimiza elimu yetu na kuua shule za serikali.

Elimu ni kitu cha msingi kwa binadamu hivyo ni lazima kila mtu agharamikie Elimu ya watoto wake. Hata kwa kiwango kidogo kulingana na uwezo na mazingira ya watu.

Leo hii kuna watu wa daraja la kati ambao wanaumizwa sana na hawa watu wa shule binafsi kwa ada kubwa wakati serikali ingeweza kuweka shule za msingi kila kata kwa ajili zinazofundisha masomo kwa kingereza na hawa wazazi wakalipia gharama kidogo ,say 500,000 /- kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi na mishahara ikalipwa na serikali.
Mzazi mwenye uwezo aruhusiwe kuhamishia watoto wao huko asiyeweza abakie kule kwenye ada ya sh. 20,000/ kwa nwaka. Pasiwe na kitu cha bure kabisa.
Kama tuna maanisha kuwa tunatoa bure kwa kuwasaidia watu basi hata hospitalini tungefanya bure mana kule ndio wanaenda wagonjwa wanaoweza hata kupoteza maisha kwa kukosa pesa.

Ningekua mie ndio waziri ningetenga shule moja ya Msingi kila kata iwe ni English Medium.
Na kila Tarafa Shule moja ya Sekondari iwe ya kulipia ada kubwa lakini iwe na mahitaji muhimu kwa mwanafunzi na idadi ndogo ya wanafunzi darasani na maabara, mabweni na walimu wa kutosha. Tupate wataalam wa kutosha.
 
Nakwambia serikali hii ina magenius! Ni jambo jema hili msiishie hapo, ilikuleta usawa na shule za serikali kuwa na ushindani na private schools inabidi shule zote za binafsi ziwe za kutwa kama shule zetu za kayumba. Hapo shule za serikali zitakuwa juu kwa ufaulu. Goli la mkono sio kwenye uchaguzi tu hata kwenye ushindani wa kielimu laweza tumiwa tu!
 
Ukweli ndio huo.
Kuna wapinzani uchwara wanaotaka kupinga na kupotosha hata mambo mazuri yanayofanywa na serikali.

Kuna shule moja wastani wake ni 85 ili mtoto ahamie pale.
Hawa hawana lolote zaidi ya kuwachuja wanafunzi na kubakiwa na wale wenye akili zao za kuzaliwa.

Hebu tufikiri kido kama Serikali nayo ingewachuja wanafunzi wake kwa namna hiyo hiyo ingekuwaje na ni wangapi wangepata elimu?

Ukiangalia hizi shule zinaandaa watu tegemezi tu wa kuajiiriwa ndio maana huwezi kuwaona huko kwenye ajira binafsi wakiwa na makampuni yao kama akina Mengi ,Anthony Dialo na Mo. Wanaandaa watu wa aina moja tu wa kukariri Darasani wakati Taifa linajengwa na watu wenye vipaji mbali mbali.

Kazi ya serikali ni kuweka wastani wa chini wa mwanafunzi kufaulu.

Ni wajibu wa shule kuzingatia wastani wa serikali.

Zamani shule za private ndizo zilizokuwa zinachukua wanafunzi wenye ufaulu wa juu.

Shule za binafsi zimelenga biashara.

Ila nailamu zaidi serikali ya Chama chetu cha mapinduzi kwa kupelekwa na wapinzani kama upepo na hofu ya kushindwa uchaguzi hali inayopelekea kukurupuka kwenye kila sekta. Wapinzani walianza kusema kuwa watatoa elimu bure kwenye kampeni za mwaka 2005 na 2010. CCM kwa woga wa kushindwa japo hata kama wangeshindwa wasingeachia madaraka nao wakaiga na kuja na sera hii inayodidimiza elimu yetu na kuua shule za serikali.

Elimu ni kitu cha msingi kwa binadamu hivyo ni lazima kila mtu agharamikie Elimu ya watoto wake. Hata kwa kiwango kidogo kulingana na uwezo na mazingira ya watu.

Leo hii kuna watu wa daraja la kati ambao wanaumizwa sana na hawa watu wa shule binafsi kwa ada kubwa wakati serikali ingeweza kuweka shule za msingi kila kata kwa ajili zinazofundisha masomo kwa kingereza na hawa wazazi wakalipia gharama kidogo ,say 500,000 /- kwa ajili ya mahitaji ya wanafunzi na mishahara ikalipwa na serikali.
Mzazi mwenye uwezo aruhusiwe kuhamishia watoto wao huko asiyeweza abakie kule kwenye ada ya sh. 20,000/ kwa nwaka. Pasiwe na kitu cha bure kabisa.
Kama tuna maanisha kuwa tunatoa bure kwa kuwasaidia watu basi hata hospitalini tungefanya bure mana kule ndio wanaenda wagonjwa wanaoweza hata kupoteza maisha kwa kukosa pesa.

Ningekua mie ndio waziri ningetenga shule moja ya Msingi kila kata iwe ni English Medium.
Na kila Tarafa Shule moja ya Sekondari iwe ya kulipia ada kubwa lakini iwe na mahitaji muhimu kwa mwanafunzi na idadi ndogo ya wanafunzi darasani na maabara, mabweni na walimu wa kutosha. Tupate wataalam wa kutosha.
Very very correct!
Kinachoonekana shule hizi sasa wanadhani elimu ni kufaulu mtihani. Wahitimu wa shule hizi wengi sasa ni wale wenye ubunifu wa chini kabisa ktk jamii.
 
Wazazi tujitaidi watoto wetu wapate lishe bora nutrition wanapozaliwa hasa kuwakazania breast feeding siku 1,000 hili wasiwe na udumavu (Stunted children) mtoto wa aina hii hata ukimpeleka shule za private kama English Medium udumavu wa watoto wa aina hii ni irreversible.Wazazi wachangie lishe bora mashuleni hili watoto wao wapate matokeo mazuri katika shule zetu za umma.Elimu bure hatakuwa na maana kama wazazi watakwepa kuwalisha watoto wao vizuri.
 
Unamfahamu mgunduzi yeyote ktk dunia hii aliyekuwa anashinda mitihani akiwa shuleni? Nakuuliza hivi ili kuondokana na wazo kwamba elimu ni kushinda mitihani ya shuleni.

Mzazi ukianza kuhangaika au shule ikihangikia divisheni wani na two badala ya elimu, ni upuuzi wa wazi. Kuna shule wanatumia hata viboko ili wapate divisheni wani, bila kujali kwamba watu hao wakiwa juu itabidi tuwatafutie Magufuli wa miaka hiyo ili awasimamie. Mitihani isiwe ndiyo elimu.
 
Back
Top Bottom