Serikali: Marufuku kufukuza wanafunzi shule binafsi wanaofeli wastani

Waache private schools waendelee na utaratibu wao

Waboreshe huku kwao ili tusiwe na sababu ya kuwapeleka watoto huko private
 
Nani kakuambia shule za binafsi hazitii bidii kwenye kufundisha? Karibia 60% ya shule za sekondari za binafsi zina maabara na maktaba.
Pili,shule za binafsi zinahakikisha mwanafunzu kuwa anasoma kwa bidii ndio maana wameweka wastani. Ukishindwa kufikisha unaondoka,unaacha wanaotaka kusoma wasome.
Acheni ujinga wakutaka kuharibu elimu inayotolewa na shule za binafsi.

Ujinga tena basi kagome msifate walilosema, eti watoto hawataki kusoma kituko umetoa. Lia kama unataka kulia habari ndio hiyo, ukitaka toa tamko
 
Hapa,naiona jinsi serikali itakavo pigwa chenga ya mwili.

Shule binafsi,hazitapokea kabisa mwanafunzi wanaedhani hataweza kuperform,yaani INTERVIEW itakuwa ya kukata na shoka.

Na nnahisi katika interview,wataset questions ambazo ndio zitakuwa determining factor,ukitoboa hayo umepita na lazima ufaulu.
Swadaktaaaaa!!umemaliza mkuu hicho ndicho kitakacho tokea shule binafsi hazita kubali ujinga huo,kwani utashusha ufaulu wao na sifa kwa shule husika.hakuna anaelazimishwa kwenda kwenye shule hizo,mtu ampeleke mwanae shule kulingana na urefu wa kamba yake,serikali inajiingiza kwenye mambo yasiyo na maana badala ya kusumbuka na majanga yanayoinyemelea nchi.
 
Nadhani kuna kuto kufahamu nini dhumuni la sera hii. Kwa miaka mingi elimu yetu imekuwa inamsukumia lawama mwanafunzi pale anapofanya vibaya au anapopata alama zisizo tosheleza. Mfumo huu umemdidimiza mwanafunzi bila kuangalia chimbuko la tatizo la kufeli, tunasahau kuangalia mchango wa mwalimu na shule kwa ujumla katika kuchangia kufeli kwa huyu mwanafunzi. Sera inayopendekezwa ni sera inayo tumika katika nchi zilizo endelea kama Marekani, Uingereza, Ujerumani na zingine nyingi. Unasikia neno "Under Performing School" na sio Under Performing Student". Kumekuwa na mtindo wa mashule kupanga alama za ufaulu za juu ili tuu mwanafunzi atakapo rudia, shule nayo inapojipatia kipato. Sasa msalaba inabidi uhame kutoka kwa mwanafunzi na kwanda kwa mwalimu au shule kwa ujumla, wote wanatakiwa watoe kipaumbele kwa wanafunzi wasio fanya vizuri madarasani mwao, kuliko kumweka mwanafunzi kwenye mzunguko wa kurudia madarasa mwisho wa siku yule mwanafunzi anaedea kutofanya vizuri huku wazazi wanaendelea kutoa ada na kuamini kuwa mtoto wao ndio anafanya vibaya.
Kwa upande wa pili, elimu yetu imekuwa haitoi nafasi kwa wanafunzi kusoma kwa nafasi, nikimaanisha mwanafunzi hapewi muda wa kujirekebisha pale anapofanya vibaya. Michujo imekuwa mingi, darasa la nne, la saba, kdt cha pili, kdt cha nne, kdt cha sita, chuoni. Tofauti na nchi kama Uingereza, mchujo ni kitato cha nne, kidato cha sita na chuo. Na huoni wao wakiwa na shida ya kutoa wanafunzi wanaofaulu mitihani yao. Hii ni kama tuwaambie wanasiasa wafanye uchaguzi kila baada ya miaka miwili, muda gani watatumia kufanya mageuzi mbadala.
 
Duuh na hainaga kukariri darasa hata akifeli. Basi tunapoelekea haitakuwa ajabu kuona mwanafunzi kamalize darasa la 7 au kidato cha 4 hajui hata kusoma, kuandika na kuhesabu kwa ufasaha. Sasa sijui malengo ni nini ya mambo hayo. Masikini elimu yetu
Wamesema anekosa wastani sio asiyejua kusoma, mtu unalipa ada ya ghali halafu wanasema wastani wetu ni 70 kapata 68 anarudia. Hilo ni mfano hai na limetokea. Unadhani ni sawa,?
 
Nadhani kuna kuto kufahamu nini dhumuni la sera hii. Kwa miaka mingi elimu yetu imekuwa inamsukumia lawama mwanafunzi pale anapofanya vibaya au anapopata alama zisizo tosheleza. Mfumo huu umemdidimiza mwanafunzi bila kuangalia chimbuko la tatizo la kufeli, tunasahau kuangalia mchango wa mwalimu na shule kwa ujumla katika kuchangia kufeli kwa huyu mwanafunzi. Sera inayopendekezwa ni sera inayo tumika katika nchi zilizo endelea kama Marekani, Uingereza, Ujerumani na zingine nyingi. Unasikia neno "Under Performing School" na sio Under Performing Student". Kumekuwa na mtindo wa mashule kupanga alama za ufaulu za juu ili tuu mwanafunzi atakapo rudia, shule nayo inapojipatia kipato. Sasa msalaba inabidi uhame kutoka kwa mwanafunzi na kwanda kwa mwalimu au shule kwa ujumla, wote wanatakiwa watoe kipaumbele kwa wanafunzi wasio fanya vizuri madarasani mwao, kuliko kumweka mwanafunzi kwenye mzunguko wa kurudia madarasa mwisho wa siku yule mwanafunzi anaedea kutofanya vizuri huku wazazi wanaendelea kutoa ada na kuamini kuwa mtoto wao ndio anafanya vibaya.
Kwa upande wa pili, elimu yetu imekuwa haitoi nafasi kwa wanafunzi kusoma kwa nafasi, nikimaanisha mwanafunzi hapewi muda wa kujirekebisha pale anapofanya vibaya. Michujo imekuwa mingi, darasa la nne, la saba, kdt cha pili, kdt cha nne, kdt cha sita, chuoni. Tofauti na nchi kama Uingereza, mchujo ni kitato cha nne, kidato cha sita na chuo. Na huoni wao wakiwa na shida ya kutoa wanafunzi wanaofaulu mitihani yao. Hii ni kama tuwaambie wanasiasa wafanye uchaguzi kila baada ya miaka miwili, muda gani watatumia kufanya mageuzi mbadala.
Umesha sema wenzetu marekani, kwani na hapa tz ni marekani?
 
Serikali haina ubavu wa kuzipangia shule binafsi zifanye nn. kuna shule ziliwahi kuburuzwa mahakamani na kushinda kesi baada ya kuwafukuza watt wa vigogo kwasabb walipata alama ambazo ni chini ya wastani waliojipangia, japo kwa vigezo vya kitaifa watt wale walikuwa wamefaulu

shule binafsi huwa zina wasainisha wazazi makubaliano maalumu (mkataba) ambao hukubalika mahakamani.

shule binafs hz zina ada binafsi, mihula binafsi, taratibu binafsi na haya yote wazazi wanayakubali. serikali isimamie shule zake tu.
Kama kinachokubabaisha ni mkataba serikali pia inao uwezo wa kuziandalia shule hizo mikataba ya kisheria kuzilazimisha kukubaliana na utaratibu ambao serikali inaona unafaa ambapo atakayekiuka mkataba atafutiwa usajili....ni ngumu sana kushindana na serikali mkuu pale inapokuwa na dhamira ya dhati kwenye jambo nyeti,sidhani kama kwenye hili serikali inabahatisha,kama nawe unakishule chako kina mtindo huo kaa mkao wa kula.
 
Msem,

Siongei kwa kubahatisha, shule binafsi hazijaanza leo kufanyiwa figisu, lkn mara zote zimeibwaga serikali.

figisu ya mwisho kupanguliwa ni ile ya ada elekezi, imekufa kifo cha mende licha ya serikali kuingia gharama kubwa. maana ilikuwa tayari imeunda chombo maalumu cha kuratibu na ilishafanya mikutano mingi tu na wadau.

iliandaa na hiyo ambayo ww unaita mikataba lkn wadau huita waraka maalumu kuzitisha na kuzishinikiza shule zitekeleze lkn yako wapi?

usidanganyike, wanafunzi watachujwa maana ndicho wazazi wao wanataka.
 
me nimekubaliana na swala la mchujo kwa shule za private sec na primary. lengo lao ni nzurikuwa jengea uwezo wanafunzi ili waweze kukompete na accademic issues. waacheni kama mlivyoaawacha kwenye ada.
 
Umesha sema wenzetu marekani, kwani na hapa tz ni marekani?
Sasa, mkiona wenzenu wanakwenda kwenye sayari nyingine na nyinyi mnatamani siku moja na nyinyi muende. Kama ukishindwa kuazima mazuri ya jirani usishangae pale unapopitwa na kuachwa nyuma.
 
Kama mmeshindwa kudhibiti ada za private schools na hili litapita kwa sababu shule hizo huendeshwa kwa makubaliano kati ya mzazi na shule.mbona hamzuii INTERVIEW Kabla ya kujiunga acheni kutafuta mnashindwa makubwa mnatafuta madogo yasio na athari
Good saying mkuu
 
Back
Top Bottom