Kwa hiyo ccm kupitia serikali yake, wamefanya fujo kwenye mdahalo wa amani ili wajenge hoja ya kufuta midahalo ya kujadili katiba.
Midahalo inayofutwa ni ya ITV kwa ajili ya usalama. Usalama unaimarishwa kwa kufuta majadiliano?
Vipi kuhusu mikutano ya ccm na mahojiano yanayoendeshwa kupitia Star TV, ITV, ya akina kikwete na wengine wanaoshawishi wananchi wapige kura na ndiyo kwenye katiba ? Bila shaka hii haina tatizo la kiusalama kwa kuwa inaendeshwa na wavuruga usalama wenyewe.
Na ni kwa ajili ya nini wanazuia watu wasijadili katiba ila wanalazimisha tu ipigiwe kura ya ndio? Hapa ni naona ni utunzaji na matumizi ya wazi ya mtaji wa ccm ambao ni ujinga wa watanzania. Ccm haitaki watanzania wapate elimu ya katiba, wabaki katika ujinga, halafu kwa ujinga huo huo, wawe manipulated kupiga kura ya ndio ili kuhalalisha uzandiki, ufisadi na ugaidi wa ccm.
Sasa wananchi wanaambiwa katiba ni yakwao kwa maana ya utengenezwaji wakati imetengenezwa na mafisadi.
Halau wanatakiwa wapige kura ya kuikubali na watakao ikataa kukiona;
Tatu ni
marufuku kujadiliana na kuielewa katiba lakini ni
lazima waikubali na kuitii vyovyote ilivyo;
Tutakufa ndiyo lakini watoto wetu wataishi kwa uhuru ndani ya nchi yao. Hakuna thamani ya maisha tena hapa Tanzania. Nisipokufa katika kutetea familia na uzao wangu kwenye katiba na haki zao za kiraia, nitakufa kwa kukosa huduma za afya, nitauawa na jambazi, nitakufa kwa ajali ambazo zinaongezeka kila siku ingawa ccm inadanganya watu zimepungua,. Nadhani nitakuwa shujaa nikuawa na ccm kwa kuwa ninatetea ustawi wa watoto na vizazi vyangu.
Kwa hali ilivyo sasa, misimamo ya serikali ya ccm kutokutofautisha chama na seriakli, namna wanavyotaka kutubana kwenye kona ili turidhie walipotuikisha na wanakotupeleka, sasa lazima kisanuke!.
Waratibu wa mipango, pangeni mtushirikishe, tuko tayari kutetea Utaifa wetu!.
Serikali inajipanga kuzuia midahalo yote na hasa inayorushwa kwenye TV kwa kile wanachokiita "sababu za kiusalama"
Kama vile ambavyo mara nyingi vyama pinzani wamekuwa wakizuiwa kufanya mikutano kwasababu za "kiusalama" ndivyo hivyo midahalo hiyo itakavyozuiliwa.
Kwahiyo wanajamii tujiandae kupokea barua hiyo muda wowote ule itakayozuia midahalo "KWASABABU ZA KIUSALAMA"
Wageni wote karibuni Tanzania.