Serikali kuwajadili waliokataa Ukuu wa Wilaya

2025DG

JF-Expert Member
Jan 30, 2023
508
1,425
Wateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.

Viongozi walioshindwa kuapa ni Rais wa CWT, Leah Ulaya ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mbogwe mkoani Geita na Katibu Mkuu wa chama hicho, Japheth Maganga aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Wilaya ya Mkoani Kagera

Katika kile kinachoonekana kutokuwepo kwa taarifa rasmi juu ya udhuru wao, Waziri Mhagama amesema yeye pia ameona kwenye vyombo vya habari kuwa wateule hao hawajaripoti katika viapo vyao kama walivyofanya wateule wengine katika maeneo yao ya kazi.

Amesema wateule hao walitakiwa kutii uteuzi huo kwa sababu katiba inamruhusu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Sululu Hassan kufanya hivyo.

Kumekuwa na mijadala katika mitandao ya kijamii kwa vigogo wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutofika katika vituo vyao vya kazi kwa uapisho.

Amesema wanachosubiri ni taarifa rasmi kutoka wizara zinazohusika wao yaani Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, Vijana na Watu wenye Ulemavu.
 
Sio lazima kukubaki uteuzi/ cheo, ndio maana mhusika aliyeteuliwa huwa anatakiwa kukiri kukikubali cheo. Kwahiyo unaweza tu kumshukuru aliyekuteua kwa kuonesha imani kwako kisha ukasema haupo tayari kwa majukumu hayo mapya na kwamba hutoweza kuyatekeleza kwa ufasaha, hivyo usije ukamuangusha aliyekuteua.

Kwahiyo unatakiwa kutoa sababu tu za kukakataa uteuzi inaruhusiwa.
 
Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Jenista Mhagama amesema wanasubiri taarifa kutoka kwa wizara zinazohusika ili waangalie taratibu na sheria zinasema nini juu ya viongozi wa Chama cha Walimu Nchini (CWT) kutotokea kula kiapo cha ukuu wa wilaya katika mikoa husika.
...wastage of time and resources, kwwani hii ni vita ya mtukula kwamba mtu asipokwenda anachukuliwa hatua? Au walitaka wakaripoti, wasitimize wajibu wafukuzwe kwa aibu?
 
Sio lazima kukubaki uteuzi/ cheo, ndio maana mhusika aliyeteuliwa huwa anatakiwa kukiri kukikubali cheo. Kwahiyo unaweza tu kumshukuru aliyekuteua kwa kuonesha imani kwako kisha ukasema haupo tayari kwa majukumu hayo mapya na kwamba hutoweza kuyatekeleza kwa ufasaha, hivyo usije ukamuangusha aliyekuteua.

Kwahiyo unatakiwa kutoa sababu tu za kukakataa uteuzi inaruhusiwa.
Inaelekea due diligence kabla ya uteuzi hakuna kabisa.

Hilo ni tatizo kubwa kwa serikali kushindwa kuwatafuta wateuliwa kabla na kufanya vetting.

Hii kazi ya vetting miaka yote ndiyo kazi ya TISS.

Wizara husika ya yule mama Jenista Mhagama imeshindwa kazi.

Kuteuliwa si adhabu na kukubali uteuzi si lazima.
 
Mh Rais imulikeni CWT!!! Kikichotokea nimrejesho kuwa ndani ya CWT Kuna ujujaji wa kutisha, pia napendekeza walimu wakatwe tsh 8000 kama CWT contribution!! Wasikatwe kulingana na ukubwa wa mshahara kama ilivyo sasa
Ni za Nini hizi??
 
Wateule wa nafasi za Ukuu wa Wilaya ambao inasemekana wamekataa uteuzi huo watatakiwa kutoa maelezo ya kwa nini wameshindwa kuripoti katika vituo vyao vya kazi kwa ajili ya uapisho...
Nadhani Kwa nchi za kidemokrasia hili lisingebebe vichwa cha habari.

Hutaki uteuzi anapewa mwingine anayehitaji hakuna haja kuwekeana vinyongo.

Sana sana wahusika walitakiwa washukuru na kukataa kwa heshima
 
Yaani kama wewe ni mtumishi wa Serikali huwezi kugomea uteuzi wa Mh Rais kirahisi rahisi tu! Kumbuka hata hapo ulipo yeue ndio Mwajiri Mkuu! Kwahiyo hawa ndg zetu kifupi wameyakanyaga!

Kibaya zaidiwatu wanahusisha kukataa kwao uteuzi kunatokana na maslahi makubwa wanayoyapata kutoka kwenye pesa za walalahoi na watu wasiofaidika chochote na uwepo wa Chama hicho cha Waalimu!!!

Lichama lipolipo tu linakusanya pesa nyingi kutoma kwa Waalimu badala yawe na ubunifu wa kuwasaidia walimu hata kuwapa mikopo ya riba nafuu hawawezi! Ujinga mwingi sana na badala yale wahuni wanazipiga tu na kulipana mishahara ya kutisha huku wachangiaji wakizidi kuchoka tu!!

Hata Mwalimu akistaafu hapati chochote cha maana hata shukrani tu ya kuwachangia!
 
Nashangaa sana jambo moja. Mtu kabla hujampa uteuzi wowote busara ni kumpigia simu na kumtaarifu. Sasa hiina hili wala lile unapangiwa Geita. Ukumbuke

1. Unatoka Dar es salaam wewe mke wa mtu na una watoto na makazi Dar. Sasa unampa mtu week aache ndoa na vingine akatumikie serikali mbali huko ukute hajawahi kufika

2. Inamtoa mtu kwenye cheo kisicho na maehaka unampa uDC anajua mda wowote anatumbuliwa pia labda hana uwezo wa kuwa DC. Kipimo gani umempima kuonyesha kuwa Anaqualify?

3. Mtu Ana kazi yenye marupurup na mshahara mzuri. Unamuamisha kwenye kazi yenye mshahara mdogo. Hata kama ni mimi nisingeweza kukubali. Unajuaje kama Ana mikopo tele na mshahara anaoufata hauendani na kima cha chini cha marejesho ya mikopo. .
 
Back
Top Bottom