Serikali kuufunga Uwanja wa Benjamin Mkapa kupisha ukarabati kuelekea AFCON 2027

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Kwani ukarabati wa Lupaso utaisha lini? Tangu mwaka 2023 Serikali iliposaini mkataba wa Bilioni 30 mpaka leo bado mambo hayaeleweki.

Serikali imetangaza kuwa Uwanja wa Benjamin Mkapa utafungwa kwa ajili ya ukarabati wa mwisho kuanzia mwezi huu (Machi, 2026) ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya kuelekea mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027.

Taarifa hiyo imetolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa, wakati wa mahojiano na gazeti la The Citizen.

Msigwa amesema hatua ya mwisho ya ukarabati itahusisha maboresho ya nyasi za uwanja pamoja na maeneo mengine muhimu, na inatarajiwa kuchukua kati ya miezi sita hadi mwaka mmoja.

Amesema ukarabati huo ukianza, uwanja hautapatikana kwa michezo yoyote, hivyo kama ratiba za mechi zitakamilika kabla ya kuanza kwa ukarabati zitaendelea kama ilivyopangwa, lakini vinginevyo timu zitalazimika kutafuta viwanja mbadala.

Kufungwa kwa uwanja huo ni hatua muhimu kwa soka la ndani, kwani Uwanja wa Benjamin Mkapa umekuwa ukitumika kama kituo kikuu cha michezo ya ligi na mashindano makubwa nchini.

Soma zaidi;
 
Miaka 3 wana karabati nini, Vipi Ingekua ujenzi wangetumia miaka mingapi?
 
Ndio wanatumia ile 30B au mzigo mwingine unalambwa?
 
Hela zinazopigwa kwenye uwanja huu ni kufuru!

K ila anayepewa Cheo anajipigia kibwege sana
 
Lupaso ingekuwa inaumwa basi ni UKIMWI kila siku dozi ya matengenezošŸ˜‚
 
Ukarabati haujawahi kuisha tu tangu 2023
 
B30 ukawa rejected wana mambo ya kisenge sana.
Then Tena unarekebishwa.
Takataka kabisa.
 
Kwa bahati mbaya sana bunge ambalo lingehoji ufisadi unaofanyika halipo hivyo ni kila mbuzi na urefu wa kamba yake.
 
uwanja unatumika zaidi kidini kuliko malengo yake ya uwanja wa mpira.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…