George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 147
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza kuhusu ni nini watanzania watachokiamua watakapopitisha katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan suala la muundo wa serikali.
Nimetamani sana uwepo mdahalo uhusuo jambo hili, ili hoja zijengwe na kusikika kuhusu tuwe na serikali kuu ya namna gani. Tuendelee na mfumo wa sasa (serikali mbili)?, Tanganyika ifufuke (serikali tatu), au Serikali kuu moja? Natumia maneo serikali kuu maana natambua zipo serikali za mitaa (halmashauri za wilaya na vijiji/mitaa/sheia)
Kama ningeulizwa iwapo muundo wa serikali kuu moja wawezafaa, nisingekurupukia kusema ndio bila kutaja yafuatayo;

- Tanzania ni dola moja, linahitaji serikali kuu moja, na bunge moja la JMT.
- Watanzania (mf. kwa mujibu wa wimbo wa taifa, na nembo ya Taifa) tunaamini katika uhuru na umoja.
- Serikali kuu moja ni umbo jembamba la vyombo vya utendaji, licha ya kuleta unafuu wa gharama za uendeshaji, itaruhusu zaidi nguvu za kiutawala zipelekwe ngazi za chini kwa wananchi kuliko kuwa na kuwa na vyombo vikubwa ngazi za juu.
- Ipo hatari ya mparaganyiko endapo kutaendelea kuwepo muundo wa serikali zaidi ya moja, harafu itokee serikali hizo tofauti zikaundwa na vyama vya siasa tofauti.
- Yamkini serikali moja yaweza kuwa sehemu ya suluhu ya kero za muungano.
- Kimahesabu serikali mbili ni yaleyale, serikali tatu ni hatua moja kurudi nyuma, serikali moja (yaweza kuwa) ni hatua moja kwenda mbele.