Serikali kuu moja, mbili, au tatu?

George Kahangwa

JF-Expert Member
Oct 18, 2007
547
147
Mara nyingi nimekuwa nikiwaza kuhusu ni nini watanzania watachokiamua watakapopitisha katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hususan suala la muundo wa serikali.

Nimetamani sana uwepo mdahalo uhusuo jambo hili, ili hoja zijengwe na kusikika kuhusu tuwe na serikali kuu ya namna gani. Tuendelee na mfumo wa sasa (serikali mbili)?, Tanganyika ifufuke (serikali tatu), au Serikali kuu moja? Natumia maneo serikali kuu maana natambua zipo serikali za mitaa (halmashauri za wilaya na vijiji/mitaa/sheia)

Kama ningeulizwa iwapo muundo wa serikali kuu moja wawezafaa, nisingekurupukia kusema ndio bila kutaja yafuatayo;
  • Tanzania ni dola moja, linahitaji serikali kuu moja, na bunge moja la JMT.
  • Watanzania (mf. kwa mujibu wa wimbo wa taifa, na nembo ya Taifa) tunaamini katika uhuru na umoja.
  • Serikali kuu moja ni umbo jembamba la vyombo vya utendaji, licha ya kuleta unafuu wa gharama za uendeshaji, itaruhusu zaidi nguvu za kiutawala zipelekwe ngazi za chini kwa wananchi kuliko kuwa na kuwa na vyombo vikubwa ngazi za juu.
  • Ipo hatari ya mparaganyiko endapo kutaendelea kuwepo muundo wa serikali zaidi ya moja, harafu itokee serikali hizo tofauti zikaundwa na vyama vya siasa tofauti.
  • Yamkini serikali moja yaweza kuwa sehemu ya suluhu ya kero za muungano.
  • Kimahesabu serikali mbili ni yaleyale, serikali tatu ni hatua moja kurudi nyuma, serikali moja (yaweza kuwa) ni hatua moja kwenda mbele.
WanaJF mnasemaje?
 
Naamini Tanzania itakua na umoja zaidi endapo kama tutakua na serikali moja (serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania), na sio kuwa na serikali mbili kama ilivyosasa au kuwa na serikali tatu kama wanavyopendelea baadhi ya wazalendo wa nchi hii.
- Haiingii akilini kwa nchi moja kuwa na serikali zaidi ya moja.
- Tutapunguza chokonozi zinazoichokonoa serikali kupitia sababu zinazoitwa kero za muungano.
- Itatusaidia kusahau kama kulikua na nchi inaitwa zanzibar, kama tanganyika inavyosahaulika na hili litaongeza mshikamano Tanzania.
- Tutapunguza gharama nyingi zinazotumika kuwalipa wawakilishi katika bunge la zanzibar, raisi wa zanzibar pamoja na serikali yake yote, Zanzibar kubakie na wakuu wa mikoa, wilaya, madiwani na wabunge watakao wawakilisha wananchi wao katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania - Dodoma.
 
Hebu soma tena,,,serikali ya jamuhuri ya muungano wa tanzania,,,it means ni serikali ya shirikisho wa nchi,zaidi ya moja,iwe mbili au tatu ndio ikaitwa muungano,sasa sisi tuna serikali mbili ambazo zilijipatia uhuru mwaka 1961 ambayo tanganyika na zanzbar 1964,na ndipo zikaungana,baada ya muungano ilikuwa tunaita hivi Jamuhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar.

Baada ya hapo ilitumika technic ya kuimeza zanzbar ndani ya muungano na kuiyuwa tanganyika na kuita tanzania tukapakiwa na serikali ya muungano ambayo ni tanganyika kuita tanzania na ikabakia zanzbar, Ni sawa zaire kiuta congo, tanganyika/tanzania.

sasa watanganyika ikiwa nyinyi munataka kuwa serikali moja hilo haliwezikani kwa upande wa zanzibar,kwani sisi ni taifa kamili tuna serikali yetu,na kila kitu chetu,haya ni maamuzi yetu,na hatuko tayari kuuza utaifa wetu kwa kujimbambika jina la ubatizo la tanganyika ambalo ni tanzania,sisi ni wazanzbari sasa inafika miaka 500 zanzibar ipo.

Sasa ikiwa wewe umependezewa na jina la tanzania jite mtanzania,lakini sisi wazanzbari tunafahamu kuwa tanzania ni ile tanganyika kilichobadilika ni jina tu,kwanza muungano hatuna,kwani mshiki wa muungano amekufa,ni sawa na ndoa mke kufa kubakia mume,hakuna ndoa tena.

Pia katika makubaliano ya muungano,rais wa zanzbar ndio anatakiwa awe makamo wa rais wa muungano kwa sababu yeye amechaguliwa na wanachi wa zanzibar kwa hiyo naweza kuwakilisha wazanzbari katika muungano,sasa jiulize Doctor Bilal amechaguliwa kichama ndio kawa makamo wa rais wa muungano vipi anaiwakilisha zanzibar ? Wakati hakuchaguliwa na wanachi ?

Kwa kweli vile vizingiti vya muungano ambavyo vilivyofanya muungano uwepo havipo na muungano umekufa,sasa muungano hakuna,uliokuwepo ni muungano wa chama tu,ASP na TANU ambayo ni ccm.

Nembo ya Taifa.jpg hii symbol ukiangalia ni ile ile ambayo ikitumika kwa serikali ya tanganyika leo tunaambiwa tanzania,sasa jiulize tanganyika sio hii tanzania ? 972872-2089765673-b.jpg 1613330.jpg Nembo hii ndio ilikuwa ikitumika kwa tanganyika sasa inatumika kama ni ya tanzania,ni sawa zaire kuita congo,utapeli tu,nani alosema tanganyika haipo ? Ipo tanganyika,rasilimali kama migodi,almasi,mafuta na gasi,sio ya muungano sasa jiulizeni yanasimamiwa na serikali ipi ? Na pesa hizo za umma zinakwenda wapi au wanagawana viongozi ? Amkeni nyinyi.

9440474.png hii nembo sasa imekuwa ya tanzania,jiulize huu sio usanii ?
View attachment 32914 na hii ndio ilivyokuwa baada tu ya muungano tukitambulika kimataifa angalia hiyo ramani ...Balozi zetu zilikuwa zikiandikwa jamhuri ya muungano wa tanganyika na zanzibar.

Sisi wazanzibar tunasema tena hatutaki hatutaki muungano,kwa sababu hauna jema kwetu,hauna fadhila,unatudhulumu sisi,na nyinyi watanganyika kama munaona ni mzigo kwenu basi bora iwe end.
 
Ndugu yangu sijui hii mada yako inaeleza nini? Kwani Tanzania ina Serikali mbili zaidi ya ile ya Kikwete? Au unafikiri Zanzibar ni Tanzania ya pili? Kuna Tanzania na kuna Zanzibar na kila sehemu ina Serikali moja tu.
 
Nataraji kuona misimamo ya hivi ikiibuka wazi wakati wa kutafuta maoni ya kuandikwa kwa katiba mpya
 
Habari zenu wadau poleni na mihangaiko.

Leo tuna serikali mbili ya Muungano na ya Zanzibar. Je utaratibu huu mzuri wa kuwa na Rais wa muungano akifika Zanzibar anakuwa hana nguvu rejea siku ya mapinduzi Rais Shein huingia mwisho baada ya Rais wa Muungano kuingia. Je utaratibu huu ukoje.

Ardhi:
Suala la Rasimali na ajira. Ni vigumu kwa Mbara kumiliki ardhi Zanzibar, na ni rahisi sana kwa mzanzibar kumiliki ardhi bara. Je suala la rasimali ardhi likoje? Leo kuna bidhaa zinatengenezwa Zanzibar ni ngumu kuingia bara au za bar ni ngumu kuingia Zanzibar.

Ajira:
Wazanzibar wapo kwa maelefu bara wakifanya kazi private na serikalini wakati ni nadra sana kwa mbara kupata kazi Zanzibar.

Rasimali ya mafuta na madini:
Leo Zanzibar na bara inasemekena kuna mafuta. Je itakuwaje hapa. Wazanzibar watakubali mafuta yao yafaidishe wote.

Bungeni pia mfano jambo likipitishwa na bunge la jamhuri ya muungano haliwi sheria hadi lipishwe na baraza la wakilishi. Yaani hapa ni kwamba baba anapitisha jambo lakini mtoto hafanyi mpaka na yeye apitishe.

Tafadhali piga kura kwa Tanzania imara.

1. Je unahitaji serikali ngapi? Iwe serikali moja na Rais mmoja mwenye nguvu pote.

Au

2. Tuendelee na hizi serikali mbili ambazo kuna Rais Muungano na Rais wa Zanzibar.

Tafadhali huu mjadala sio wa vyama vya siasa. Changia bila kufata ushabiki wa chama au mihemko ya utanganyika na uzanzibar.
 
Wazanzibar wameenea maeneo mengi ya dunia kujitafutia kipato kutokana na kutawaliwa na mkoloni mweusi hivyo mirija yote ya shughuli za kiuchumi kufungwa. Hakuna namna nyengine ni kujichanganya huko huko Tanganyika mpaka pale mnapoiruhusu Zanzibar kuwa huru kiuchumi. Ardhi ya Zanzibar ni ndogo sana hivyo lazima ilindwe kwa namna yoyote ile kwa vizazi vijavyo, itakuwa ni upunguani kumuuzia ardhi adui wako, Watanganyika ni maadui wakubwa wa kisiasa na kiuchumi wa Zanzibar hivyo wazanzibar wapo makini sana. Suala la mafuta bado ni porojo tu hatuna uhakika wa uepo wake mpaka hapo yakapochimbwa (kama yapo) na kuhusu madini hayo ni Tanganyika haito kaa itokee kuwa mali ya Muungano maana adhma yenu yenu kwa Zanzibar ipo wazi. Ama kuhusu serikali ngapi? Suluhisho zuri ni kuuvunja huu Muungano wa kihuni kila nchi iendelee na shughuli zake. Hakuna faida hata moja kwa Zanzibar zaidi ya madhila tu.
 
Kafie mbelee lete referendum leo uone UKOLONI WENU UTAKAVYOAIBIKA
 
Ndio maana nikasema kwamba umefika wakati Wazanzibar popote walipo kuungalisha nguvu dhidi ya uovu huu wanaouanda Watanganyika dhidi ya Visiwa vyet pendwa
 
Wanataka kuiga ya Mod wa India na Kashmir?!

Mnatafuta sifa za ajabu, hawa Wazanzibari mnataka kuwaua bure bila sababu ya msingi.

Kama mnataka Tanzania moja mbona mnaendelea kupima viwanja/ardhi kila mtu na kipande chake?!

Muwaache Wazanzibari na nchi yao.
 
1 ndio jibu mkuu,Makonda atolewe Dar aende akasimamie Mkoa uliozungukwa na maji.
 
Tafadhali piga kura kwa Tanzania imara.

1. Je unahitaji serikali ngapi? Iwe serikali moja na Rais mmoja mwenye nguvu pote.

Au

2. Tuendelee na hizi serikali mbili ambazo kuna Rais Muungano na Rais wa Zanzibar.

Tafadhali huu mjadala sio wa vyama vya siasa. Changia bila kufata ushabiki wa chama au mihemko ya utanganyika na uzanzibar.
Blindspot kweli wewe ni blind, labda uwaulize wana CCM peke yao wapige hii kura kwani wao ndio wanaobishana kuhusu iwe 1 au mbili. Sisi wenye mawazo tofauti hatutagusa hapa.
 
Habari zenu wadau poleni na mihangaiko.

Leo tuna serikali mbili ya Muungano na ya Zanzibar. Je utaratibu huu mzuri wa kuwa na Rais wa muungano akifika Zanzibar anakuwa hana nguvu rejea siku ya mapinduzi Rais Shein huingia mwisho baada ya Rais wa Muungano kuingia. Je utaratibu huu ukoje.

Ardhi:
Suala la Rasimali na ajira. Ni vigumu kwa Mbara kumiliki ardhi Zanzibar, na ni rahisi sana kwa mzanzibar kumiliki ardhi bara. Je suala la rasimali ardhi likoje? Leo kuna bidhaa zinatengenezwa Zanzibar ni ngumu kuingia bara au za bar ni ngumu kuingia Zanzibar.

Ajira:
Wazanzibar wapo kwa maelefu bara wakifanya kazi private na serikalini wakati ni nadra sana kwa mbara kupata kazi Zanzibar.

Rasimali ya mafuta na madini:
Leo Zanzibar na bara inasemekena kuna mafuta. Je itakuwaje hapa. Wazanzibar watakubali mafuta yao yafaidishe wote.

Bungeni pia mfano jambo likipitishwa na bunge la jamhuri ya muungano haliwi sheria hadi lipishwe na baraza la wakilishi. Yaani hapa ni kwamba baba anapitisha jambo lakini mtoto hafanyi mpaka na yeye apitishe.

Tafadhali piga kura kwa Tanzania imara.

1. Je unahitaji serikali ngapi? Iwe serikali moja na Rais mmoja mwenye nguvu pote.

Au

2. Tuendelee na hizi serikali mbili ambazo kuna Rais Muungano na Rais wa Zanzibar.

Tafadhali huu mjadala sio wa vyama vya siasa. Changia bila kufata ushabiki wa chama au mihemko ya utanganyika na uzanzibar.

Ilibidi uweke na sehemu ya serikali tatu. Unapoweka mbili au moja na wale wanaotaka serikali tatu inakuwaje?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom