Serikali kuondoa maduka ya dawa karibu na hospitali ni kufufua gari bovu kwa spea kutoka gari zima

Kuhamisha maduka ya dawa karibu na hospital ni kusumbuwa watu,,

Kila la siku napiga Kelele humu,
Dawa ya watu kuwa waadilifu ni kuweka adhabu Kali kwa wale wote wanaofuja Mali za umma.

Na atakayekamatwa na dawa za serikali basi adhabu yake ni Sawa na kesi ya mauaji.

Uone kama dawa zitakosekana mahospitalini..

Watu wanaiba dawa mnafanya kuwabembeleza wasiibe,,


Ajabu Sana..mwizi anabembelezwa asiibe.
 
Hizi fujo za kiutendaji ni ishara ya kukosa weledi. Mnada wa Tanzania alioutaja Mjuzulu JYN naona unakaribia sana!
Haya ni maandalizi rasmi ya kuwahangaisha wagonjwa na relatives kusafiri miles kufuata dawa na vifaatiba vinavyokosekana kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati, usumbufu kwa wapiga kura. Karuhusu nani na Sasa anakataza nani
 
Haya ni maandalizi rasmi ya kuwahangaisha wagonjwa na relatives kusafiri miles kufuata dawa na vifaatiba vinavyokosekana kwenye hospitali, vituo vya afya na zahanati, usumbufu kwa wapiga kura. Karuhusu nani na Sasa anakataza nani
Hao wanatudhihirishia wazi kwamba wameshindwa kazi kabisa! Hii haina tofauti sana na fukuzafukuza iliyowakumba wamachinga hivi juzi kati. Serikali iweke udhibiti mzuri wa mali zake, na wala siyo kuwanyanyasa wafanyabiashara na walipa-kodi halali.
 
Wananchi wetu wataonja raha lini? Tangu nchi ipate uhuru nchi yetu imetawaliwa na chama kimoja tu hicho hicho kwa awamu zote, lakini kila ikija awamu mpya na kila Waziri, Mkuu wa Mkoa na mkuu wa wilaya mpya ni kama kwamba nchi inatoka kwenye uongozi wa chama kingine. Watanzania kila kukicha hawana uhakika kutatokea nini kesho kwemye maisha yao. Kila kiongozi mpya atakosoa uongozi uliomtangulia kwa kuwahangaisha wananchi.

Waziri wa Afya anataka maduka yote ya dawa yakae umbali wa mita 500 kutoka zilipo hospitali zote nchini, eti kuzuia dawa za hospitali zisiende kwenye maduka hayo kwa njia ya wizi na kuzuia mashaka kwa wananchi kuwa dawa kwenye maduka hayo zinatoka hospitali, jamani. Kufanya hivyo ni kuwaingiza hasara wafanyabiashara waliowekeza mitaji yao kwenye maduka hayo, lakini ni kusababisha msumbufu mkubwa sana kwa wagonjwa na ndugu za wagonjwa wanaolazimika kwenda kutafuta dawa na vifaatiba kwenye maduka haya baada ya dawa na vifaatiba hivyo kukosekana hospitali. Sasa itawalazimu wapige safari kwenda mbali kutafuta dawa kwenye maduka hayo.

Waziri angefanya yafuatayo ili kutatua tatizo hili:
1. Kuhakikisha kuwa hospitali zote zina dawa zote na vifaatiba vyote muda wote kwa mwaka mzima
2. bei ya dawa kwenye hospitali ni bora na bei nafuu kuliko kwa watu binafsi.
3. Watumishi wasio waaminifu kwa dawa za umma wanaondolewa na kushtakiwa mara moja
4. Wananchi wanaodhani kuwa maduka ya watu binafsi yanauza dawa za hospitali waelimishwe.
5. Mfumo wa udhibiti wa dawa kuingia na kutoka uimarishwe kuziba mianya ya wizi.

Waziri anapewa taarifa totofu kuhusu uhaba wa dawa mahospitalini, ukweli ni kwamba, hakuna dawa na vifaa toshelevu kwenye hospitali zetu za serikali sawa na ilivyo kwa madawati, vitabu, maabara na vyumba vya madara kwenye shule zetu.

Tuzijaribu kufufua vibovu kwa kuharibu vile vizima, hapo tunatengezeza vibovu viwili kwa wakati mmoja, watakaoumia ni wananchi.


Swali ni moja tu kama dawa zote zinaingizwa nchini kwa kupitia MSD ni kwanini kuna upungufu kwenye hospitali wakati maduka binafsi yana dawa hizohizo?
 
Mku hata ikiwa 500M ni nusu kilometer, kwani nani kakwambia dawa za serikali haziwezi kuvushwa zaidi ya nusu kilometer? Watu wenyewe unakuta mfanyakazi wa Muhimbili anaishi Temeke au Tandika kwani unafikiria nini?

Labda na wafanyakazi wote wajengewe nyumba za kuishi ndani ya meter 500. Wasivuke hata kutembelea ndugu zao wa mbali isipokuwa kwa kibali maalumu.
Kamjibu aliyesema mita500 ni sawa kutoka muhimbili Hadi manzese. Hajasema wezi hawawezi kuiba na kupeleka umbali wa mita 500.
 
Waache uvivu wawalipe MSD pesa zao Ili madawa yajae mahospitalini.
Sekta binafsi hauepukiki
 
Waziri angefanya yafuatayo ili kutatua tatizo hili:
1. Kuhakikisha kuwa hospitali zote zina dawa zote na vifaatiba vyote muda wote kwa mwaka mzima
2. bei ya dawa kwenye hospitali ni bora na bei nafuu kuliko kwa watu binafsi.
3. Watumishi wasio waaminifu kwa dawa za umma wanaondolewa na kushtakiwa mara moja
4. Wananchi wanaodhani kuwa maduka ya watu binafsi yanauza dawa za hospitali waelimishwe.
5. Mfumo wa udhibiti wa dawa kuingia na kutoka uimarishwe kuziba mianya ya wizi.
Naafikiana nawe
6. Maeneo yote ya hospitali yafungwe CCTV cameras
 
Nikwamba hiyo sheria ilitungwa idadi ya watu nchini ikiwa bado ndogo. Ipelekwe Bungeni ibadilishwe haiendani na hali halisi ya maisha ya watu.
Sheria ni ya 2020.

Sio jambo geni hilo.
 
Mita 500 , ina maana kutoka Muhimbili duka liwe Manzese .
Sababu zinazotajwa kuyaondoa maduka ya dawa karibu na hospitali hazilingani na gharama na nguvu ya kuyahamisha maduka hayo, yaani kubomoa mashelfu na partitions, kuhamisha AC, dawa zote kwenda kwenye nyumba nyingine iliyoko 500m kutoka hospital. Gharama za Hiyo nyumba nyingine kuitengeneza hadi ikidhi vigezo vya pharmacy ni kubwa sana. Wafanyakazi lazima wapoteze ajira kwanza wakati boss anatafuta na kuitengeneza hiyo sehemu ingine.
 
Hii nchi imejaa viongozi wanaotaka muda wote waonekane ni wachapakazi hodari! Ummy Mwalimu, Dorothy Gwajima, Hamis Kigwangala na Juma Aweso, ni mifano hai!

Zamani pia tulikuwa na akina Daudi Albert Bashite! Yaani wakipewa mamlaka, ni kusumbua tu watu na pia kutoa matamko tatanishi muda wote!

Huyu Ummy wakati akiwa Tamisemi, eti alipiga marufuku walimu kuhama kutoka Vijijini na kwenda Mjini! (Na Wakati ni haki ya mfanyakazi iwapo ametimiza vigezo na masharti! Mfano kuhama kwa gharama zake mwenyewe, iwapo amekaa kituo kimoja miaka mingi na hivyo anataka kubadili mazingira, nk.)


Badala yake wakitaka kuhama kutoka Mjini kwenda Vijijini, eti waruhusiwe! Akili ndogo kabisa hii.
Sasa unajiuliza; alitumia Sheria/kanuni gani? Utakuta hakuna majibu. Na ingekuwa yeye aambiwe aishi Kijijini maisha yake yote atakubali? Jibu utakuta ni hapana!

Na ukimuuliza ni kwa nini watumishi wa umma wengi wanahama kutoka Vijijini na kukimbilia Mjini? Unaweza ukakuta kwa akili zake nyingi kichwani, hajui!! Nadhani ifikie wakati apunguze mihemko na kutafuta attention kwa Bosi wake muda wote.
Yeye anafahamu kuwa vijijini hakuna English medium chekechea na primary kwa watumishi ambao wangependa watoto wao wasome shule za hivyo, anafahamu kuwa vijijini hakuna nyumba za watumishi, Kuna matembe TU, anafahamu kuwa vijijini hakuna maji Wala umeme, anafahamu kuwa vijijini hakuna Bank Wala saccos. Kwanini iwe marufuku kwa mtumishi kuhamia mjini. Lazima kuwe na policy ya watumishi wa vijijini.

Hizi ni dalili kuwa Iko siku watu watakataa kwenda kupiga kura kiboyaboya kama zamani, watajitambua.
 
No kweli kwenye radius ya 500m unaweza kufuna maduka zaidi ya matano nikitumia mfano was Mawenzi Hospital Moshi.

Ina maana Hawa wafanyabiashara wanfungiwa biasharara zao kwa kosa gani? Kwa mini serikali inakwepa udhibiti was dawa kwenye hospitali zake?

Isitoshe huo umbali wa meta 500 ametumia kigezo gani kuupata,? Kwa Nini siyo meta 400 au 800?!
Hii ni sawa na kiongozi mwanamke kuacha kuwaambia wanawake wenzie waache ukahaba na kuvaa nguo fupi badala yake anawalalamikia wanaume wanaotembea na makahaba waache kutembea nao ili makahaba wasipe wateja.

Hakuna magonjwa mpumbavu atakwenda duka binafsi kununua dawa wakati hospitali zipo
 
Back
Top Bottom