Serikali kukopa Stanbic ni sahihi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Serikali kukopa Stanbic ni sahihi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BONGOLALA, May 21, 2010.

 1. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #1
  May 21, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,392
  Trophy Points: 280
  Waziri wa fedha Mustafa Mkulo katangaza serikali kukopa $200mil kutoka benki ya Stanbic kupunguza nakisi ya bajeti ya bil 200 kutokana na wafadhili kupunguza kiwango cha msaada ktk bajeti.

  Swali: Kwa sasa TRA inakusanya bil 400 Tsh kwa mwezi, ina maana Mkulo haoni kuwa kama mianya ya ukwepaji kodi ikidhibitiwa huo upungufu wa bil 200 unaweza zibwa na TRA? Je, kukopa benki ndio suluhisho la nakisi ya bajeti? Pia hajaeleza jinsi gani mkopo utakavyorejeshwa kwa vianzo vipi? JE, mkopo kwa serikali hua hausishi bunge kuidhinisha?

  Isije ikawa kama ununuzi wa rada. Kwa nini waziri hakufikiria kubana matumizi yasiyo ya lazima kuziba pengo?

  Katika mdororo wa uchumi nchi za wenzetu serikali huzipa mikopo mabenki hapa tz benki ndiyo husaidia serikali hapo naomba ufafanuzi
   
 2. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #2
  May 21, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Hata kama TRA watakusanya trition 400 kwa mwezi, serikali hii haina displine ya matumizi ya fedha za walipa kodi.

  Angalia jinsi wakubwa wanavyosafiri nje na misururu mirefu ya watu wasio na lolote la kuongeza kwa nchi kwa hela za walipa kodi. Without having discipline in public expenditure, based on approved budget what should we expect?

  Maisha bora kwa kila mtanzania yamekuwa maisha bora kwa viongozi na wateule wao. Hii serikali ni serikali mbovu kuliko serikali yoyote maana inakwenda kwa kubahatisha bahatisha tu.
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  May 21, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  Wameambiwa wafanye hivyo na IMF na World Bank ukimhukumu Waziri wa fedha unamuonea, yeye kaambiwa suluhisho ni mkope na pa kukopa waambiwa ni Stanbic.

  Maamuzi yote makubwa Tanzania wanaamua IMF na WB hata Rais hana maamuzi. Hiyo ndo hali halisi, na katika historia ya IMF na WB hawana mfano wa nchi hapa duniani ambayo wameshaisaidia ikaendelea kama hata unao huo mfano tupe hapa

   
 4. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #4
  May 21, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Sawaaa, lakini hata kama ukiambiwa ukope kwani na wewe ndio huna akili ya kupambanua?

  Kwanini tusitumie rasilimali zetu kibao kwa ajili ya bajeti na matumizi yetu? Sijui tunaenda wapi na ni nani atatuongoza
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  May 21, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,181
  Trophy Points: 280
  Unapoliza "ni sahihi" unamaanisha kisheria, kiuchumi, kijamii, kwa kuyumkinika au vipi?

  Kisheria, kiuchumi, kijamii, kwa kuyumkinika inawezekana bila tatizo. Ingawa si kitu kizuri.
   
 6. Mvina

  Mvina JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2010
  Joined: Aug 2, 2009
  Messages: 1,000
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Tatizo letu tumelala sana na yaonesha tumeridhika sana na hali ya umasiki tuliyo nayo mi nadhani hata hawa tunaowaita wahisani na nchi marafiki inabidi wakate kabisa kuchangia bajeti yetu ila viongozi na sisi wananchi tupate akili ya kujitegemea.

  Rasilimali tunazo ila vichwa bado vimelala tunapenda sana starehe kuliko kazi ni kama vile tunakula zaidi kuliko tunavyozalisha sasa katika hali kama hiyo unategemea nini kifuate?

  Serikali inatakiwa itafute namna ya kuongeza uzalishaji wa bidhaa na si kutegemea kuagiza kila kitu toka nje na pili ibane matumiza yake ikiwezekana hata kupunguza mishahara ya mawaziri na wabunge kama si marupurupu.

  Safari bado ni ndefu, Mungu ibariki Tanzania.
   
 7. S

  Subira Senior Member

  #7
  May 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Haonewi huyo waziri, ila kama kiongozi anapaswa kuangalia nini cha kufanya chenye faida siyo kupokea amri ya imf na wb tu kama zuzu.

  Na tulishaambiwa ni kihiyo what do you expect, kwa nchi hii there are many solutions many many many! Kitu hapa ni uongozi bora ndio unaogomba, nchi yenye vyanzo vingi vya kipato na ndiyo nchi maskini ktk maskini huoni kuwa shida ni uongozi, magari ya kifahari, wake watatu watatu kwa viongozi.,

  Hizo safari za nje zisizo na hesabu kwa misafara iliyojaa wajumbe, kupeana tender za kifisadi we unaongea nini usitukasirishe zaidi!
   
 8. S

  Subira Senior Member

  #8
  May 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 162
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Tabu yetu iko kwenye uongozi na kushauka kwa wanaotuongoza, baada ya mwalimu kubana viongozi waliochukua nafasi baada yake walishauka na nafasi hizo wakaamua kutureep of, sie wajinga wajinga tunaowachagua tukiamini watatusaidia kumbe wote wanabadilika na kuwa aina moja wakishapata uongozi.

  Kama Rwanda mawaziri wanatumia suzuki na nchi inapanda kuliko kawaida sie tunashauka na mashangingi
   
 9. Liz Senior

  Liz Senior JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2010
  Joined: Apr 19, 2007
  Messages: 485
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Sina hakika sana na hili lakini hata hivi majuzi nilipokuwa napitia vitabu vya mwanangu vya civics form 2 niliona mahali wanataja vyanzo ambavyo serikali inaweza kutumia kwa matumizi, hii ni pamoja na mikopo toka taasisi za ndani na nje
   
 10. m

  mbarbaig Senior Member

  #10
  May 22, 2010
  Joined: Feb 10, 2009
  Messages: 151
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Bro, kukopa mabenki ya ndani mara nyingi kunaongeza interest rate ya mikopo kwa raia wa kawaida...cut down spending...na govt haiwezi kukopa bila IMF na world bank kuiruhusu so it is a vice versa from what you are saying...don't blame IMF or world bank here this is your own shit...cut spending and balance your budget..sidhan kama world bank ndio tuna kuambia nunua luxury cars etc...wake up!!!
   
 11. m

  mapambano JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2010
  Joined: Mar 14, 2008
  Messages: 535
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Miaka iliyopita budget ilipitishwa ikiwa na sehemu mbili. 1) Budget ya kujitegemea, incase donors hawata toa mchango wao. 2) Budget tegemezi, inayojumlisha donors na mapato ya serekali. Wasiwasi wangu, huyu Mkullo, utendaji wake na historia yake. Je ni mtu anayeweza kutilia ngumu mambo ya pesa? Kwa mfano zile safari za JK, sasa haya ndio matunda ya hizo safari?

  Najua tuko kwenye mambo ya uchanguzi, lakini haya mambo ya kukopa, wajukuu zetu kazi wanayo...


  By PIUS RUGONZIBWA,

  21st May 2010

  THE government will borrow 250 million US dollars (about 350bn/-) from a foreign bank to offset a deficit in its 2010/2011 budget, but declared that it is not going to create a heavier burdern to taxpayers.

  Finance and Economic Affairs Minister Mustafa Mkulo said the move follows the decision by some donors to slash their contribution to the General Budget Support (GBS) by 220 million US dollars in the next financial year.


  He told a news conference in Dar es Salaam yesterday that the government was in final talks with the Stanbic Financial Group that has agreed to issue a loan to be repaid in five years.


  The minister also hinted that the government was likely to spend 9 trillion/- on its 2010/2011 budget, but could not give much detail on local and external sources of revenue as well as sectoral allocation.


  He further said that there would be insignificant increases of tax in 2010/2011, reassuring traders and investors stability and prudence of the Fourth Phase government fiscal policies.


  "We are not going to draw more blood from the already over-burderned taxpayers," he stressed.


  Traditionally the government depends on external sources including grants, loans and aid to finance its about 30 per cent budget deficit.


  The minister was reacting to reports that GBS donors have slashed over 220 US dollars contribution in 2010/2011 financial year, demanding speedy implementation of some reforms, in a move that brought fears that various social and development programmes could be frustrated.


  The development partners agreed to give the government 534 million US dollars in GBS in 2010/2011 financial year. But the minister said more funds were expected from the African Development Bank (AfDB).


  "It is true, Development Partners are not happy with how we are working on some reforms for them to continue supporting our budget. But I wish to assure that things are now under control and the deficit won't be felt any more," he said.


  The minister said the donors had earlier committed themselves to give the country over 220 million US dollars for 2008/2009 and 2009/2010 financial years to mitigate effects of the global financial crisis.


  "Technically, we have already spent the money that we are supposed to be given during the next financial year (2010/2011) in the wake of economic recession..and for that reason we are now sourcing the funds elsewhere," he said.


  He admitted that there were several areas that called for reforms in line with the donors' requests that includes cost of doing business, public finance management, legal sector reforms and the investment climate.


  Mr Mkulo said the government plans to move in the National Assembly bills seeking changes on the Investment Act and provision of a legal framework on Private Public Partnership (PPP).


  He, however, said reforms in various areas have already been carried out in public finance management, local government finance and establishment of the post of internal auditor general at the Treasury.
   
 12. p

  pareto 8020 Member

  #12
  May 22, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna maswali mengi ya kujiuliza juu ya majibu ya Mkulo.

  1) Hivi kama ni kweli ilifahamika toka awali kwamba wafadhili watapunguza msaada wao mwaka huu, kwanini imemchukua zaidi ya wiki moja Mkulo kutoa msimamo huo.....na kwanini his initial reaction iliyokuwa reported kwenye media alionekana kustuka? Hili linaleta walakini juu ya majibu ya Bw Mkulo (unless kama alikuwa hajui hizo latest info.....ndio amekuwa briefed....na if that is the case then ameonyesha kukosa umakini...itakuwaje mtu mwenye dhamana ya masuala ya pesa asiwe informed kwenye jambo nyeti kama hilo?

  2) Hio altenative measure waliyochukua ya kukopa kwenye Commercial bank....terms zake ni zipi? Serikali italipa riba kiasi gani? Kwa kawaida, serikali haikopi from commericial banks.....kwasababu riba zake zipo juu na pia ni mara chache commercial banks kutoa long term soft loans - kama matumizi yake ni kwa ajili ya kugharamia recurrent expenditure...

  3) Hivi hakuna altenative ways za serikali ku raise hizo fedha? Je ile option ya kuuza treasury bonds haifai kutumika kwa hapa? Kwa kuwa Mkulo anasema uchumi ni imara na sasa nchi inaheshimika na imetoka kwenye kundi la nchi masikini sana....kwanini wasi issue bonds zikanunuliwa kwenye soko.....nikiri wazi mie sio mchumi hivyo pengine sielewi vizuri mfumo huu...

  4) KWanini maelezo ya Mkulo yanatofautiana na maelezo ya donors...? who is not telling the truth? Donors wanasema wamesitisha kwasababu serikali haijaweza kutekeleza makubaliano kadhaa.....Mkulo anasema walishakubaliana na Donors kwamba mwaka huu watapunguza pesa za msaada kwakuwa waliikopesha serikali wakati wa economic crisis mwaka jana? Statment hiii ya Mkulo ni mpya....donors waulizwe kama ni kweli haya ndio yalikuwa ni makubaliano....

  5) Nilitegemea katika statment yake Mkulo angeweza kuelezea kwamba serikali ina mkakati wa ku cut costs ili kukabiliana na upungufu huo wa fedha, na pia kukabiliana na hali mbaya ya uchumi kwa ujumla inayoikumba dunia na haswa nchi za ulaya ambazo ndio wafadhili wakuu wa Tanzania.

  Nadhani waandishi wetu wa habari wanahitaji kuuliza maswali haya ya msingi kwa Mkulo na Donors ili ukweli halisi ufahamike
   
 13. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Kama Jakaya anaipenda nchi hii asione aibu aseme tu jamani kazi imenishinda ; atafutwe ntu mwingine na yeye astaafu na pension ya Urais atapata, lakini atakuwa ameiokoa nchi kutoka kwenye njia ya kuangamia!! kwa mtindo huu tulionao,kama atapata miaka mingine mitano tujuwe wazi huko mbele hakuna salama!!
   
 14. Lighondi

  Lighondi JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 585
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Ayaaaaaaaa!!!! Lol!!! Imeshakula kwetu tena. kazi tunayo kizazi hiki. Enewei labda tutaanza kupata akili kichwani!
   
 15. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2010
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Twafaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ilo sio deni la serikali bali letu wananji. Mayoooooooo, maweeeeeeee, mai wasuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Haya maswali nimeyauliza katika thread nyengine na kuelezea hatari ya Tanzania kukopa ndani ya nchi kwani terms and conditions zake zinaweza kuwa kubwa kiasi kwamba nchi ikashindwa kulipa na matokeo yake nchi ikaingia katika malimbikizo ya madeni ambayo wajukuu zetu ndio watatulaumu.

  Na kumbuka unapokaa na deni linazidi kuongezeka na vilevile na ugumu wa deni unapozidi sijui sasa hawa jamaa wanaliona hilo au wanatafuta solution ya haraka kufidia shortage ya liquidity katika hazina ili mzee azidi kutanua!!!
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  May 22, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Hivi kwa nini CCM isijiuzulu na kutengeneza serikali ya MSETO iliyo na viongozi bora?

  Ngoja yaje ya GREECE ndiyo watafahamu hasira za wananchi.

  Hapo lazima ufahamu kuwa NUSU ya hizo hela ni hela ya TAKRIMA na Rushwa za uchaguzi.
   
 18. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #18
  May 22, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Kwa upande wangu naona ni bora wafadhili waache kabisa kutoa misaada kwani wananchi wa kawaida hawafaidiki na misaada hiyo. Na pia tuweze kujifunza kutumia vizuri kipato chetu.

  Tanzania kama nchi tuna vyanzo vingi sana vya kujiingizia kipato, lakini hatuko makini katika kutumia vyanzo hivyo na kibaya zaidi hata kile kidogo tunachopata hatujui kukitumia kwa busara.

  Tulikuwa hatuna haja ya kupungukiwa pesa kama hiyo kwenye bajeti ya nchi laiti kama tungeweza kusimamia na kulinda vyema makusanyo ya mapato yetu. Tunahitaji kuwa na vipaumbele muhimu katika matumizi ya pesa.

  Tunahitaji kupunguza maisha ya hanasa ya viongozi wetu kwani bila kuficha maisha ya waziri ama mbunge wa Tanzania ni ya hanasa zaidi kuliko maisha ya waziri ama mbunge wa Uingereza. Tunahitaji kupunguza safari na semina za viongozi zisizo na faida ama umuhimu.
   
 19. K

  Kinombo JF-Expert Member

  #19
  May 22, 2010
  Joined: Feb 24, 2007
  Messages: 332
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dhahabu bado hiko juu usd 1241.00/ounce na TZ ni nchi ya Tatu kwa uzalishaji Africa....
   
 20. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #20
  May 22, 2010
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,450
  Likes Received: 782
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha ajabu gabbage in gabbage out,wakubwa wa nchi wanapokula bila kunawa mpaka wakavimbia hawawezi wakatunza ankala. Wanakulupuka tu hii ndio staili ya Bongo.Hawakujua kuwa bila kupunguza matumizi haramu ya pesa za umma,wafadhili watakata mirija yao?Kwani pesa ya Wafadhili inatokana na kodi za wananchi wao.
   
Loading...