Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,569
- 9,429
Serikali imepanga kufanya marekebisho makubwa katika taasisi ya elimu nchini ili kuweza kutengeneza vitabu vitakavyoendana na matakwa ya mitaala ya masomo husika vitakavyotumika mashuleni.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo kwa hapo Bungeni dodoma ambapo amesema watatumia wasomi mbalimbali nchini waliojikita kwenye fani ili kutengeneza vitabu bora na kuondokana na makosa yaliyotokea katika vitabu vilivyopita
Akijibu swali kuhusu zoezi la utolewaji wa vitambulisho vya taifa Waziri Mkuu amesema taasisi ya vitambulisho vya taifa “Nida” inaendelea na zoezi la uandikishaji wananchi ili kutoa vitambulisho hivyo ambavyo mpaka sasa vimekwishatolewa katika mikoa zaidi ya tisa nchini
Amesema serikali kupitia taasisi ya Nida imejipanga kufanya kazi hiyo ya uandikishaji kwa umakini mkubwa ili kuepuka kutoa vitambulisho hivyo kwa watu wasio watanzania hasa wananchi wanaoishi katika mikoa ya Pembezoni hivyo isionekane kuwa zoezi hilo linachelewa.
Chanzo; ITV