Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 3,119
- 1,428
SERIKALI KUANZA KUNUNUA MAHINDI YA NGARA
π14/04/2025
NGARA
ββββββββββββββββββββββββββββββββββ
Serikali imeahidi kuanza kununua mahindi ya Wakulima wa Wilaya ya Ngara kuanzia mwezi wa tano mwaka huu wa 2025.
Hatua hii itaimarisha bei ya soko la mahindi ambayo imekuwa ikibadirika badirika na hivyo kuathiri wakulima.
Ni mara ya kwanza Serikali kununua mahindi ya Ngara na hatua hii inaenda kuwezekana kutokana na juhudi za Mbunge wa Ngara MH NDAISABA G RUHORO ambaye amekuwa akiwapigania wananchi wake kuhakikisha wananufaishwa na kilimo ambacho ndicho tegemeo kubwa la Wananchi wa Ngara.
Sera ya bei nzuri ya mazao, kuongeza uzalishaji na thamani ya mazao ni sehemu ya mkakati wa Mh Ruhoro wa PESA KWA WOTE 2025-2030. Mkakati huu unalenga kugawa miche milion 10 ya kahawa, miche milioni mbili ya Parachichi, kuimarisha masoko na kuchochea ongezeko la thamani na uhai wa bidhaa za kilimo za Kahawa, Parachichi, Ndizi pamoja na nafaka nyinginezo.
Watu wengi wanamuombea Mh RUHORO afya njema ili aendelee kutekeleza mipango hii yenye lengo la kukuza kipato na kuondoa umasikini na kufanya maisha yawe bora kwa wananchi wa Ngara.
Fedha itakayo letwa kununua mahindi ya Ngara itatolewa na Rais Wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. Samia Suluhu Hassan na hii na kwa sababu Rais Samia anawapenda wananchi wa Ngara na watanzania kwa ujumla. Kila mtu anamuombea Afya tele Rais wetu na hakika tunakwenda kumpa mi 5 tena.
Wenu
Ernest Ruhugu
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Ngara.