Serikali: Kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi itakuwa Siku ya kufanya Usafi nchini!

tena wewe unatakiwa uwahi kutoka huko mbagala rangi nne unapokaa kwenda kufanya usafi pale kariakoo shimoni! ole wako uchelewa achilia mbali kutokwenda kabisa!

Kuna makampuni ya usafi mijini na wanalipwa na wameajiri watu.mimi siwezi kwenda mjini kufanya usafi wakati kodi yangu ndo kazi yake.
 
Nimesikia agizo lililotolewa na Waziri kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku ya Usafi kitaifa na kila raia wa nchi hii ni lazima ashiriki shughuli hiyo ili kuweka mazingira yetu safi.
Wapo ndugu zetu Wasabato ambao kwa imani yao siku hiyo ya jumamosi hakifanyiki chochote hata kuingia jikoni kujipikia bali ni kusali na kuomba tuu. Jee kwa agizo hili itakuwaje? Hapo hapatatokea mgogoro wa kiimani?
 
Nina maana watafanya usafi ijumaa jioni kabla ya saa sita usiku kuamkia jumamosi.

Hili jambo nina hakika litaleta mgongano katika jamii. Mtu wa dini nyingine mtaani utakapomlazimisha afanye kazi ya kusafisha mtaa wake wakati jirani yake hataki kwani imani haimruhusu hapo ndio kasheshe.
 
Serikali imetangaza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya kufanya usafi nchi nzima!

Mh Luhaga Mpina pia amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanikisha jambo hili na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kila siku!

Tunaipongeza serikali kwa juhudi hizi za kuhakikisha miji inakuwa misafi na kutunza mazingira..ni vyema watanzania tukaunga mkono juhudi hizi.!

Chanzo: EATV
Hii ni njema kwa afya zetu.Ni matumaini yetu yule mzee aliyekuja kupanda daladala Gongo la mboto na kununua muhogo wa mama lishe atakuwa akija kutuhamasisha na kusaidiana nasi kwenye zoezi hili la kizalendo,au ndo mpaka OCTOBER 2020?
 
Back
Top Bottom