Suala la usafi Kila mwisho wa mwezi maduka yasifunguliwe mpaka muda fulani

Kaka yake shetani

JF-Expert Member
Feb 1, 2023
3,611
8,746
Mnaweza kuniita mkorofi ila upande mwingine tutabaki kutatua matatizo ya tanesco umeme masaa mawili usikatike.

Kwanza na mlaumu aliyeanzisha Ili la kujiwekea taratibu Kila mwisho wa mwezi ufanyike usafi shuguli zisifanyike.

Kuna watu hapa JF mtatoa mapovu ila kujiuliza kama mijini na masokoni Kuna Kila aina ya ushuru mfano pesa ya takataka,pesa za mazingira tena wale wenye viwanda n.k zote hizi zikilenga swala la usafi.

Kwa wale mliopo mijini mnaafahamu wanao husika na kusafisha Jiji Kila mda wa jioni.

La kujiuliza kazi zao ni nini mpaka mwisho wa mwezi Yani tunapoteza pesa za nyingi Kila mwisho wa mwezi.
Kwa sifa za viongozi wasio na akili
 
Raia yeyote anawajibika kulisafisha eneo lake, Yani mita tano kutoka mpakani mwa eneo lake.

Ushuru upo masokoni. Na huko masokoni Sheria zinaelekeza kwamba ni jukumu la mfanyabiashara kulisafisha eneo lake na kuweka taka sehemu MAALUM, ambapo kazi ya kuzoa taka ni ya Manispaa.

Ushuru unaolipwa si kwa ajili ya kufagia bali ni kwa kazi ya kuzoa taka na kufanya maendeleo.

Sheria inaelekeza adhabu ya papo kwa papo iwapo itabainika kwamba ndani ya eneo la mita tano za mtu husika Kuna uchafu.

Hivyo jukumu la usafi wa mazingira la raia yeyote. Viongozi wanafanya usafi ili kutoa hamasa japo Bado Sheria inambana raia afanye usafi.

Maeneo mengine ya umma hufanyiwa usafi na Manispaa husika mfano kuondoa mchanga Barabarani na taka kwenye mitaro mikubwa, japo kisheria ikibainika Kuna watu au mtu anachafua maeneo tajwa naye ataadhibiwa.
 
Mnaweza kuniita mkorofi ila upande mwingine tutabaki kutatua matatizo ya tanesco umeme masaa mawili usikatike.

Kwanza na mlaumu aliyeanzisha Ili la kujiwekea taratibu Kila mwisho wa mwezi ufanyike usafi shuguli zisifanyike.

Kuna watu hapa JF mtatoa mapovu ila kujiuliza kama mijini na masokoni Kuna Kila aina ya ushuru mfano pesa ya takataka,pesa za mazingira tena wale wenye viwanda n.k zote hizi zikilenga swala la usafi.
Kwa wale mliopo mijini mnaafahamu wanao husika na kusafisha Jiji Kila mda wa jioni.

La kujiuliza kazi zao ni nini mpaka mwisho wa mwezi Yani tunapoteza pesa za nyingi Kila mwisho wa mwezi.
Kwa sifa za viongozi wasio na akili
Tena ni ujinga sana swala la usafi ni la kila mtu kila mtu anatakiwa kuwajibika mazingira yake ya kazi au ofisi yawe masafi kila siku sio mpaka mwisho wa mwezi.

Viongozi wanatakiwa kuwa wabunifu ili kuhakikisha haya yanawezekana uzuri almashauri zinamamlaka ya kutengeneza bylaws sijui wanafeli wapi..

Wanatakiwa waCreate bylaws ila make sure wana jihatached na wananchi mbona mambo yangekuwa rahisi.
 
Mnaweza kuniita mkorofi ila upande mwingine tutabaki kutatua matatizo ya tanesco umeme masaa mawili usikatike.

Kwanza na mlaumu aliyeanzisha Ili la kujiwekea taratibu Kila mwisho wa mwezi ufanyike usafi shuguli zisifanyike.

Kuna watu hapa JF mtatoa mapovu ila kujiuliza kama mijini na masokoni Kuna Kila aina ya ushuru mfano pesa ya takataka,pesa za mazingira tena wale wenye viwanda n.k zote hizi zikilenga swala la usafi.
Kwa wale mliopo mijini mnaafahamu wanao husika na kusafisha Jiji Kila mda wa jioni.

La kujiuliza kazi zao ni nini mpaka mwisho wa mwezi Yani tunapoteza pesa za nyingi Kila mwisho wa mwezi.
Kwa sifa za viongozi wasio na akili
Ni ujinga wa viongozi wetu wasio thamini muda wa kazi. Hata ukiwauliza faida na hasara ya uamuzi huo jibu watakupa la kisiasa. Wafanya biashara kila siku asubuhi kabla ya kuanza biashara hufanya usafi na wengine baada ya kufunga biashara. Unaweza toa ajira mtu afanye usafi wakati biashara inaendelea.
 
Back
Top Bottom