Serikali: Kila Jumamosi ya Mwisho wa Mwezi itakuwa Siku ya kufanya Usafi nchini!

Hahahaaaaa hii serikali sasa inatuona wote ni mabwira.
Watanzania tunalipishwa kodi nyingi sana,haki ya nani mimi wanangu watasafisha maeneo ya nyumba yangu tu!
kama wameshindwa ku provide essential services (Merits) tools na equipments kwenye serikali za mitaa na kuhakikishajMajiji yanapewa fungu la kujazia kwenye budget ya usafi basi sioni maana ya kuiita hiyo ni serikali makini.
Kumfanyisha mtu kazi bila malipo hata mungu wa Wasabato atawalaani.
Tumieni pesa zetu kwa busara sio kufanya mashindano ya kufyatuka.
Very sad people
 
Sisi wasabatho jeee

Vigezo gani vimetumika kutenga siku ya Jumamosi

Mambo ya imani hayaingiliwi......Rwanda wanachofanya wasabato wanafanya usafi J2 .........kwani nao wanautaratibu kama huo.....ila kama msabato mwenyewe atapenda kufanya jumamosi hamna shida......wanyarwanda tupeni shule kwani hii ni copy and paste kutoka kwenu......
 
Kweli Mungu hawezi akakupa vyote. Ningeshangaa sana, eti Mungu atupatie rasilimali na wakati huo huo atupatie viongozi wenye akili, never.
 
Serikali imetangaza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya kufanya usafi nchi nzima!

Mh Luhaga Mpina pia amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanikisha jambo hili na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kila siku!

Tunaipongeza serikali kwa juhudi hizi za kuhakikisha miji inakuwa misafi na kutunza mazingira..ni vyema watanzania tukaunga mkono juhudi hizi.!

Chanzo: EATV

Mkuu niliweka uzi huu hapa JF naona serikali leo imelifanyia maamuzi: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...wa-mwezi-iwe-sikukuu-ya-usafi-nchi-nzima.html
 
Na amesema hii ni lazima kwa kila mtu.....

yaani hata kugusia tu kodi na ushuru wote wanaokusanya unafanyia nini hakugusa
na hii ya 'lazima' ni kwa mujibu wa sheria zipi hawasemi...
eti naibu waziri anasema kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na waziri wake January Makamba....dah
Nyani Ngabu platozoom Dark City Nguruvi3 ...

Tanga tulifanya sana enzi za Said Kalembo ila alipoondoka kila kitu kikaenda naye. Hata elimu ya kujitegemea iliondoka na ujamaa.

Tungejifunza kushawishi ingesaidia.
 
hii safi sana, lazima tuwe na utamaduni kitaifa wa kufanya usafi
 
...hii kitu ni muhimu; hata kama hakuna sheria inayomtaka mtu kufanya usafi kwa lazima,lakini kwa sababu usafi ni muhimu kwa afya zetu,sioni sababu ya kuanza kulalamika kuhusu hili.
Natumai huu ndio mwanzo wa maeneo yetu kubadilika sasa, uchafu hautakuwepo,na hata ukiwepo utakua kwa kiwango kidogo.
Muhimu,ni vyema waweke dustbin za kutosha ili watu wapate pa kuhifadhia uchafu,na yale magari ya kusomba uchafu yafike kwa wakati,ili kuondoa uchafu uliokusanywa karibu na makazi ya watu.Isitokee tena uchafu kukaa muda mrefu kabla haujazolewa,kama ilivyotokea siku ya uhuru.
 
Mkuu kama wazo ni zuri....kwa nini utafuti ufumbuzi wa tatizo la kuzoa taka...badala yake unakuja na kauli/maswali ya kikebehi. Mimi nilitengemea utoe wazo la namna ya kupata pesa ama mchango wa kuondoa taka mtaani baada ya kusafisha mitaa.
Mfano: Kwa kukuwa tatizo la uzoaji taka umekuwa tatizo maeneo ya mijini na miji inayokuwa basi kila kato la EWURA, na REA kwenye ununuzi wa units za umeme zikatwe sent hamsini (jumla shilingi moja) kwa ajili ya kukodi magari ya ziada ya kuzole taka wakati huo tukiomba wamimiliki wa magari hayo kijitolea kuzoa taka walau trip mbili na kila atakayejitolea atunukiwe cheti chenye saini ya rais. Kwa maeno ya mashambani tuhimize matumizi ya taka kwa uzalishaji wa nishati na mbolea....!!

Mchango wa nini tena mkuu wakati Kila nyumba inatozwa Shs 1000 kwa mwez kwa ajili Ya kubeba takataka.
 
Boxing Day hii itahusika? Naona huu mwaka umeanza na sarakazi lukuki.
Na isipohusika, kwa nini? Ili hali tarehe 9 ilihusika.
 
Serikali imetangaza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya kufanya usafi nchi nzima!

Mh Luhaga Mpina pia amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa kuhakikisha wanafanikisha jambo hili na kuhakikisha mazingira yanakuwa safi kila siku!

Tunaipongeza serikali kwa juhudi hizi za kuhakikisha miji inakuwa misafi na kutunza mazingira..ni vyema watanzania tukaunga mkono juhudi hizi.!

Chanzo: EATV
MIMI NITAKUWA NAENDA KANISANI......Nitakua nafanya jpil....au usafi kwanza kwa Mungu baadae?....
 
Back
Top Bottom