Serikali Izuie Watu Kuja Dar...

Ukitazama miji mingi duniani wenyewe huwa wanawapisha wakuja..wanahama wanaenda kwingine na wakuja hupenda kujifanya ndo wenyewe..it happens a lot..wenyeji hadi mnakuwa kama wageni..watu wanaona maduka kariakoo kumbe zamani tulifunga mitaa kwa mpira..Sasa wao wanapaki magari na kulipia parking hawajui watoto waliifunga hiyo mitaa kwa mpira tu..
 

Du jamaa unaumimi sana nini maana kuwa watanzania watu hawajaenda kenya wako nchini kwao nadhani wewe ulikuja kwa mbio za mwenge umezoea sasa unajifanya dar yako
 
Ukisema wa mikoani tusije Dar au tuje dar kwa vitambulisho,je na sisi wa mikoani tukiamua na nye mje kwa vitambulisho ndugu mtawatembeleaje?

Kwani hujui maendeleo yanatokana na uwingi wa watu?mnategemea kila kitu toka mikoani kwanza dar hamna mashamba au mtaishi kwa kula biskuti za Azam
 

First time I stepped into NYC, an old gentleman told me the same thing.

Mzee aliniambia kuna New Yorkers old school ambao wamekuwa hapa mjini for generations na generations, hawa hawana tabu, kuna watu poa sana.

Halafu kuna hawa wamekuja juzikutoka South Carolina, Montana na Jamaica.

Hawa ndio wanajifanya New York kwao kuliko original New Yorkers wenyewe.

Ndicho kinachotokea hapa.

Watu wa Dar wenyewe hata hawana matatizo, mji ukiizidi vurugu wanaenda Mkuranga, Kisarawe na Mbwamaji.

Sasa usiombe hawa waliokuja Dar baada ya kuzaliwa kwa chama kipyaa, tarehe tano mwezi wa pili sabini na sabaaa eee mungu ipe barakaaa.

Utakomaa.
 
Kiranga ikifika Jumamosi utashangaa ukienda soko la,kariakoo...magari tele watu wanatoka tabata kuja kununua nyanya na vitunguu kariakoo kumbe masoko waliyoyapita huko bugurun na ilala yanauza way cheaper..so now soko la kariakoo limekuwa sehemu ya 'kuwabamiza' wakuja..very funny kwa wenyeji
 

Sasa wanatoka Tabata kwenda Kariakoo Buguruni kote huku hamna masoko?

Tabata pale relini ukikata ukachepuka kidogo ilikuwa unatokea SUKITA, enzi hizo tukienda kununua mayai pale.

Baadaye kupata umri kidogo vibaa baa vya Mandela Road fujo sana. Kuna UKIMWI si mchezo. Nilikuwa na kitoto kimoja.ki.mixer cha Sri Lanka kinakaa mitaa ile kwa nyuma kule. Hatari tupu.

Kuna party moja walifanya mchanganyiko watoto wa kishua Bima kule kina Willy, na watoto wa uswahilini

Basi mie nimekuja ki soap soap mwenyewe, nina thin rimmed glasses, basi nimejiegesha vipi sijui, washashi wakaidaka.

Basi mwenyewe nikawa nimeshatoa sadaka kwa.watoto wa kihuni.

Basi pale kulikuwa na boda la kutambaa na wigo wa Msimbazi unatokea Tabata unakatika Kigogo, Kigogo unatokea Mchikichini, unatokea Migomigo, ukipandisha umetokea Jangwani mara uko Muhimbili ukishusha uko town.

Pale dampo kwa juu kulikuwa kuna mchizi anaweza kukuchongea chata ya Bima kwa 30,00 hata trafiki mwenyewe akiiangalia haishtukii.

Chata la Mwaikambo and all.
 

Hahaha wenye Dar yenu mnaringaa, jamaa alipofika Tábora akitokea.kigoma akasema "aisee acha tu, kigoma ni muji.lakini tabora ni daaslam"
 
Hahaha wenye Dar yenu mnaringaa, jamaa alipofika Tábora akitokea.kigoma akasema "aisee acha tu, kigoma ni muji.lakini tabora ni daaslam"

Tabora hapo kuna mtoto mmoja miksa la Kitusi na kinyamwezi basi ndo kwao.

Mshua wake alikuwa RPC mkoa fulani.

Miksa za kitusi si unazijua mwenyewe.

Mpaka masista duu ambao walikuwa hawakusemeshi wananza kukuomba urafiki, mara tu wanaanza kukushauri uvae hivi na vile ukiwa nae, duh.

We acha tu, bado kidogo mjanja mzima nitangaze ndoa.

Ila hapo hapo nikakipa Oslo.

Juzi nimerudi nakuta watu washazalisha kwa saana tu.
 
una hoja ya msingi,ila hujaiweka vyema. Hapa shida yako nafikiri population pressure na hakika dar sasa imezidiwa.
Nakutafutia takwimu.
 
bakini kwenu mnatujazia mji wetu, kwan si mna mikoa yenu kwanin msiishi huko.!? aarggghhh

Mji mmeshindwa kuuendesha,achen wakuja tuwaonyeshe.siku hizi umepanga au bado unaishi kwa ndugu zako?rudi bagamoyo mkaendeleze mji wenu.
 

Waambie bana.. Watu wamekimbia makwao huko hata kurudi hawataki leo wanadai Dar ni kwao na wanataka wengine wasije na wanadai wapewe vitanbulisho....Sawa vitambulisho vitulewe lakini lazima wazingatie Origin za watu...na wale wazamiaji pia wapewe vitambulisho vya kuonyesha wao ni wazamiaji.
 

Nenda na wewe mkoani then tuone kama utakuja kutamba na thread kama hii tena
 

Wasizuie watu tu bali na mapato ya madini yalipiwe mikoa inayochimba madini ili mikoa iwe na nguvu ya kiuchumi,pia hata maamuzi ya kisera ziachiwe manispaa kwani kuna mikoa kama Shinyanga yenye migodi mikubwa mitatu inauwezo wa kujenga hospitali kubwa kuliko Muhimbili na kununua ndege zake yenyewe.Dar nini bhana watu wengi wenye uwezo siku hizi wanaruka abroad kupitia Nairobi na mizigo yao inapitia Mombasa.Dar magumashi tu na kama si wizi mnaotufanyia watu wa mikoani kupitia serikali hilo jiji lenu lingekuwa kama Tanga tu

Sent from my BlackBerry 9220 using JamiiForums
 
Nyie wageni mnaanza kugombania jiji, Sisi tuliokuwa na mashamba SINZA,TABATA tusemeje? Nyie njooni tuwatume.
 
Nshaenda kuangalia "Bedroom Eyes" hapo ndani ya Empress, na "Never Say Never Again" ndani ya Empire.

Huku nna John Rupia, huku nna Jeshi.

Mkavirondo anayekataza watu wasije mjini alikuwa tarafa gani enzi hiyo?
atakua alikua tarafa ya ntuzu enzi hizo,kipindi hicho hata kuiona Land lover 109 kwa mwaka labda mara moja,au mpaka upite msafara wa nyerere ama waziri mkuu salimu ahmed salimu.
 
Wakazi wote wa Dar tupewe vitambulisho special.., hakuna kuingia Dar kama huna hicho kitambulisho.., unless uwe umepata kazi huku au unamwaliko maalumu kutoka kwa mwana Dar.., na hiyo shughuli iliyokuleta ikiisha unarudi ulikotoka.., TUMEJAAA...!!

ukisema hivyo ni kuwekeana vikwazo na utengano mkuu. watu wa dar hawawezi kuishi bila kutegemea mikoani.. vivyo hivyo watu wa mikoani hawawezi kuishi bila dar. sasa ndugu yangu unavyosema mwiko kuja dar, chakula 90% kinachokuja dsm kinatokea mikoani, ukiwazuia watu wa mikoani kuja dar watu wa dar watakula nini???? vivyo hivyo watu wa mikoani hutegemea vitu kama bandari ya dar na mengine mengi.. ukizuia itakuaje?? ni ushauri tu mkuu. let us live together as one. as a nation...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…