Serikali iwasaidie wananchi wanaopukutika kwa Radi huko Mbeya, Rukwa, Katavi na kwingineko

Takwimu za kizamani bado zinaonyesha kwamba Chanzo kikuu cha vifo vya wanadamu ni maradhi , kwamba Wengi wanaopoteza maisha ni wale kwanza waliumwa na baada ya jitihada za madaktari kushindikana hufariki .

Lakini kwa maeneo mengine takwimu mpya zinaonyesha kwamba kumeibuka chanzo kipya cha vifo kinachoitwa Radi , sasa hivi si ajabu tena kila inyeshapo mvua kusikia radi imeua watu kadhaa eneo fulani , Radi imeibuka kuwa chanzo madhubuti cha vifo huko nyanda za Juu kusini, Mbeya, Katavi, Rukwa na sasa Kigoma na Tabora , kwa Mfano sasa hivi kule Kyela , na hasa maeneo ya boda ya Kasumulu , kijiji cha Isaki , Njisi , Lubele na Mbako ni maeneo hatari mno kwa radi , watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya sana kwa kipindi kifupi cha miaka mitano hivi iliyopita.

Naiomba sana serikali ichukulie janga hili jipya la radi kama chanzo kipya cha vifo vya halaiki kwa binadamu na wanyama , hatua za kisayansi za kulinda maisha na uhai wa watu zichukuliwe haraka , kama tulichukua hatua kwenye Kipindupindu na Corona basi hatuna budi kufanya hivyo kuikabili radi pia .

Kazi Iendelee .
KATAVI...Mwese na Lugonesi ni kama simba na yanga RADI KAMA huko rashiya na yukreni
 
Kipo kifaa kinafungwa kwa ajili ya kupoteza radi Nchi zilizoendelea kwenye majengo marefu wamefunga hiyo kwa yale majengo bila kuwa na hicho kifaa kila kukicha majengo marefu yangepigwa na radi hata kwenye minara ya makampuni ya simu wamefunga sema haina nguvu ya kupoteza radi kwa eneo kubwa..
 
Takwimu za kizamani bado zinaonyesha kwamba Chanzo kikuu cha vifo vya wanadamu ni maradhi , kwamba Wengi wanaopoteza maisha ni wale kwanza waliumwa na baada ya jitihada za madaktari kushindikana hufariki .

Lakini kwa maeneo mengine takwimu mpya zinaonyesha kwamba kumeibuka chanzo kipya cha vifo kinachoitwa Radi , sasa hivi si ajabu tena kila inyeshapo mvua kusikia radi imeua watu kadhaa eneo fulani , Radi imeibuka kuwa chanzo madhubuti cha vifo huko nyanda za Juu kusini, Mbeya, Katavi, Rukwa na sasa Kigoma na Tabora , kwa Mfano sasa hivi kule Kyela , na hasa maeneo ya boda ya Kasumulu , kijiji cha Isaki , Njisi , Lubele na Mbako ni maeneo hatari mno kwa radi , watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya sana kwa kipindi kifupi cha miaka mitano hivi iliyopita.

Naiomba sana serikali ichukulie janga hili jipya la radi kama chanzo kipya cha vifo vya halaiki kwa binadamu na wanyama , hatua za kisayansi za kulinda maisha na uhai wa watu zichukuliwe haraka , kama tulichukua hatua kwenye Kipindupindu na Corona basi hatuna budi kufanya hivyo kuikabili radi pia .

Kazi Iendelee .
Hizo takwimu ziko wapi?
 
Mkuu mbona unanishambulia bila kosa lolote ? mimi siwezi kusemea ya Tukuyu ambayo siyajui , nimeeleza ya Kyela ambako ni nyumbani na ninao ushahidi .

Umenishambulia kwa kunionea sana , tena nimeikumbusha serikali kusaidia raia wote bila kujali waliko .
Msamehe Ako na stress, trust me kapigwa tukio na dada wa kinyaki basi anachukia kila mtu
 
Back
Top Bottom