Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,548
- 217,818
Takwimu za kizamani bado zinaonyesha kwamba Chanzo kikuu cha vifo vya wanadamu ni maradhi , kwamba Wengi wanaopoteza maisha ni wale kwanza waliumwa na baada ya jitihada za madaktari kushindikana hufariki .
Lakini kwa maeneo mengine takwimu mpya zinaonyesha kwamba kumeibuka chanzo kipya cha vifo kinachoitwa Radi , sasa hivi si ajabu tena kila inyeshapo mvua kusikia radi imeua watu kadhaa eneo fulani , Radi imeibuka kuwa chanzo madhubuti cha vifo huko nyanda za Juu kusini, Mbeya, Katavi, Rukwa na sasa Kigoma na Tabora , kwa Mfano sasa hivi kule Kyela , na hasa maeneo ya boda ya Kasumulu , kijiji cha Isaki , Njisi , Lubele na Mbako ni maeneo hatari mno kwa radi , watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine kujeruhiwa vibaya sana kwa kipindi kifupi cha miaka mitano hivi iliyopita.
Naiomba sana serikali ichukulie janga hili jipya la radi kama chanzo kipya cha vifo vya halaiki kwa binadamu na wanyama , hatua za kisayansi za kulinda maisha na uhai wa watu zichukuliwe haraka , kama tulichukua hatua kwenye Kipindupindu na Corona basi hatuna budi kufanya hivyo kuikabili radi pia .
Kazi Iendelee .