Wananchi wenyewe tunachangia miundombinu ya serikali kuharibika,mfano mvua zinapokua zinanyesha wananchi wamekua na tabia ya kumiminia taka taka kwenye mitaro eti isombwe na maji,kitu kinacho changia mitaro na makaruvati kuziba.Hivyo pengine kupelekea mafuriko yasiyo na ulazima kwa watu waishio mabondeni,lakini pia barabara zingine hua zinaharibiwa na haya maji yanayo chepuka kutokana na mitaro na makaruvati kuziba.
Hivyo basi mimi nashauri serikali itunge sheria kali kwa yeyote ambae katika eneo la uwanja wake,nyumba yake,eneo la kazi aidha kibanda,duka n,k kukikutwa mtaro umejaa takataka,karuvati limeziba,au mtaro haujasafishwa kwa muda sahihi basi achukuliwe hatua kali za kisheria.Yani hiyo iwe ni lazima kila mwananchi kusafisha eneo la mtaro wake na kuhakikisha mtaro haujai mchanga ambao utapelekea kizuizi maji kupita.Ni wajibu wetu kuitunza miundombinu iliyopo.