Serikali isiyagawe mashamba makubwa kwa wananchi wa jembe la mkono

kavulata

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
12,313
12,613
Hiwezi kuanzisha kiwanda kinachotegemea wakulima wanaolima kwa kutumia jembe la mkono.

Kama kuna yaliyokuwa mashamba makubwa, plantations ya wanyama, nafaka, kahawa, zabibu, machungwa, mkonge au mpira ambayo yalikuwa yanamilikiwa na serikali au wafanyabishara ni makosa makubwa kuyafuta na kuyarudisha kwa wakulima wadogo. Kufanya havyo sio tu kwamba kunaua uchumi lakini kunaua pia viwanda na uchumi na ajira kwa vijana wengi.

Tutafute wawekezaji waendeleze na sio kumshawishi rais afute umiliki ili wapewe watakaolima kwa mkono kwa kutegemea mvua.

Unahitaji mashamba makubwa ya alizeti yanayolimwa kisasa na kupandwa mbegu bora na kutunzwa na kuvunwa kitaalamu ili kupanda mafuta yanayoweza kulisaidia taifa.

Tuache mawazo ya kijamaa tutafute wawekezaji wataotoa ajira kwenye kilimo kwakuwa kulima, kupanda, kupalilia, kuvuna, kubeba, kusindika, kulinda na kusafirisha mazao kutahitaji vibarua wa moja kwa moja na wasiokuwa wa moja kwa moja kama mama lishe, bodaboda, tigopesa, wauza mchele na nyanya, nk.
 
Inawekana wale wanakijiji wanaozunguka hayo mashamba hawana ardhi ya kulima.
 
Back
Top Bottom