Serikali isitishe hili zoezi la bomoabomoa

Serikali isitishe hili zoezi la bomoabomoa

SELFISH

Senior Member
Joined
Feb 25, 2014
Posts
133
Reaction score
61
Mh rais, sitisha hili zoezi la bomoa bomoa kwa wakazi wa mabondeni. Tunajua kua kuna baadhi walipewa viwanja na wengine hawakupewa kabisa, Ijulikane kwamba hakuna mtu anaependa kuishi kwa tabu kiasi kile kwenye mvua hua hawana amani ila ni shida tu!

Nafiki tunazalisha kizazi cha kuichukia serikali. Angalia watoto wanavyolia pamoja na wazazi wao. Ni heri kama ingetumika busara ya kuwapa fidia ya kodi ya japo mwaka mmoja kwa kila mmoja. Ikumbukwe serikali nayo inamakosa kwanini wasinge wazuia wakati wanajenga?

Hebu angalia watoto wanavyo teseka

facebook.com/itvtz
 
Si Mlijifanya Kumuunga Mkono Yule... Sasa Mtaisoma Namba KISAWASAWA Hadi MTANYOOKA Tu. Na Bahati Nzuri Hata SHERIA Itawamaliza Tu Hivyo TIINI Tu Maamuzi Ya MAMLAKA au Kama Vipi Mwambieni Huyo Mtu Wenu Kuwa Hizo HELA au Hiyo Bajeti Anayotaka Kuitumia Kuzunguka Nchi Nzima Kuwashukuru Angeimega Tu Kidogo Ili Awapeni Mjenge Nyumba ILA Kwa Upande Wetu Mziki Ni Ule Ule Tu Wa HAPA KAZI TU!
 
Si Mlijifanya Kumuunga Mkono Yule Mpuuzi Wenu Sasa Mtaisoma Namba KISAWASAWA Hadi MTANYOOKA Tu. Na Bahati Nzuri Hata SHERIA Itawamaliza Tu Hivyo TIINI Tu Maamuzi Ya MAMLAKA au Kama Vipi Mwambieni Huyo Mtu Wenu Kuwa Hizo HELA au Hiyo Bajeti Anayotaka Kuitumia Kuzunguka Nchi Nzima Kuwashukuru NYUMBU Angeimega Tu Kidogo Ili Awapeni Mjenge Nyumba ILA Kwa Upande Wetu Mziki Ni Ule Ule Tu Wa HAPA KAZI TU!

Haya bwana, Mungu akubariki mkuu
 
Wanaoichukia serikali ni wachache kuliko wanaompenda Magufuli, hizi huruma huruma ndo Kikwete alikuwa nazo leo mnasema ndo rais mbovu kuliko waliomtangulia, nyumba zibomolewe tu! Nchi irudi ktk mstari, hawa wakibomolewa, wengine watajifunza kuwa endapo watakaidi agizo la kujenga pasio ruhusiwa yatawakita nao!
 
Wapewe viwanja vilivyopimwa maeneo mengine kabla hawajavunjiwa. Pia watafutiwe makazi ya muda yenye huduma zote za kijamii. Hili jipu ni chungu Sana, linauma hadi kwa watoto
 
Mods naona ifike wakati tukubaliane kutumia utambulisho wa kweli tu maana huyu Gentamycine amezidi. Yeye anasema ni Mnyarwanda ila ameishi TZ bali kwa sasa yuko kwao yapata miaka 11. Sasa kama ni hivyo mambo ya Bongo mbona yanamgusa sana? Ana maslahi gani na nchi hii wakati sio kwake?
 
Kwa maelezo yake ana roots za Butiama kama sio Mara!
 
Suala la kujenga mabondeni halina mjadala kwa sababu tunazuia mikondo ya maji. Mvua za siku hizi ni nyingi sana ndani ya muda mfupi sasa maji yanakosa njia yanavamia nyumba za watu. Waathirika hawa walishapewa viwanja Mabwepande na walipewa muda wa kuhama kwa hiyo hili zoezi ni endelevu.
Wasisahau nyumba ya mch Getrude Lwakatare aliyeziba njia mto kwa gabions ili kupanua kiwanja chake huko Mbezi Beach.
Na wale Stone Blocks pale mto Mbezi darajani sijui kama wameshahama.
 
Zoezi hili midhali limeanza na limalizwe! kuna matajiri WANAJULIKANA wamejenga maeneno hatarishi kama haya kuna wapo SELANDER Bridge hapo! kuna wapo Bonde la Mpunga! HAKUNA KUSITISHA ! liendee mpaka huko! kama watu wa hali ya chini wamevunjiwa basi haki itendeke kote kuvunjwe! ili maji yapite kirahisi!

Chini ya Mh Magufuli tunataraji kuona haki inatendeka kote kote kuanzia watu wa chini kati mpaka mabwanyenye! waionewe wa JAngwani tu mpaka huko maji yanapokaribia kufika!
 
Uongozi na kutumia busara. Mvua zinanyesha, watu wazima na watoto wanavunjiwa nyumba wakati huu, huu si uongozi. Uongozi huenda na hekima na busara. Sheria zipo, lakini hekima na busara huzidi sheria. Subirini basi muwavunjie wakati wa kiangazi, unyama gani huu mnaowafanyia raia wenu?
 
Inahuzunisha na kusikitisha sana lakini pia wanasheria wanasema, ignorance of the law is no excuse.

Kwa sababu katika awamu hii tumeamua kuishi ndani ya sheria, hatuna budi kukubali athari zake.

Ikumbukwe kuna watu walikufa na wengine walipata athari za kimaisha ili tupate uhuru kwa faida ya Watanganyika wote. Vile vile itabidi baadhi ya watu wapate misukosuko kwa faida ya watanzania wengi kuishi ndani ya sheria za nchi.

Hata hivyo, ninawalaani pia watu wanaosimamia sheria kwa kushindwa kufanya kazi zao properly mpaka watu wanafikia hatua ya kuvuta maji na umeme katika nyumba zao bila kuwapiga stop.
 
Mimi kwa mtazamo wangu naona kama hao wakaazi wa mabondeni wanataka tu huruma ya umma kuhararisha upumbavu wao wa kukaa huko maeneo hatarishi......suala la wao kutakiwa kuhama huko mabondeni halikuanza leo wala jana.......ni suala la takribani miaka zaidi ya kumi iliyopita......katika kipindi chote hicho tumekuwa tukishuhudia maafa baada ya mafuriko kutokea na kuingiza serikali katika gharama za kipumbavu kwa ubishi wao wenyewe......
Ule muda wa kuchekeana na kubembelezana umekwisha sasa ni muda wa kuishi kwa kufuata sheria........ninachowaomba serikali kuwa wasiishie tu kuwaondoa tu hao wakazi wa jangwani zoezi liendelee kwa wote waliojenga katika maeneo yasiyo ruhusiwa kisheria.......
 
Si Mlijifanya Kumuunga Mkono Yule Mpuuzi Wenu Sasa Mtaisoma Namba KISAWASAWA Hadi MTANYOOKA Tu. Na Bahati Nzuri Hata SHERIA Itawamaliza Tu Hivyo TIINI Tu Maamuzi Ya MAMLAKA au Kama Vipi Mwambieni Huyo Mtu Wenu Kuwa Hizo HELA au Hiyo Bajeti Anayotaka Kuitumia Kuzunguka Nchi Nzima Kuwashukuru NYUMBU Angeimega Tu Kidogo Ili Awapeni Mjenge Nyumba ILA Kwa Upande Wetu Mziki Ni Ule Ule Tu Wa HAPA KAZI TU!

Beware of the way you consider yourself someone in the ruling class, hakuna dhuluma inayochekesha.

Believe me ignorant boy, mkurugenzi wa manispaa ya nyumba zinakovunjwa was once proud than you feel now.

Kwa namna yako ya maongezi, you are nothing more a stupid pathetic fool on the street, nyumba hazivunjwi sbb ya watu kuunga mkono upinzani, zilipaswa kuvunjwa long time ago ila wewe kwa upumbavu wako unaona ni wkt wa kuchochea hisia mbaya kwenye mioyo ya watu.

Umelelewa vibaya sana wewe
 
Mh rais, sitisha hili zoezi la bomoa bomoa kwa wakazi wa mabondeni. Tunajua kua kuna baadhi walipewa viwanja na wengine hawakupewa kabisa, Ijulikane kwamba hakuna mtu anaependa kuishi kwa tabu kiasi kile kwenye mvua hua hawana amani ila ni shida tu!

Nafiki tunazalisha kizazi cha kuichukia serikali. Angalia watoto wanavyolia pamoja na wazazi wao. Ni heri kama ingetumika busara ya kuwapa fidia ya kodi ya japo mwaka mmoja kwa kila mmoja. Ikumbukwe serikali nayo inamakosa kwanini wasinge wazuia wakati wanajenga?

Hebu angalia watoto wanavyo teseka

facebook.com/itvtz
Si waliwapigia kura ukawa wezi, ccm ya sasa hapindishi sheria, pole zao.
 
Linahitaji busara kabla ya kukurupuka kuvunja nyumba za watu!
 
% kubwa ya watu wanaotaka mageuzi ni watu wanaotambua haki zao na wasomi na tafiti zinaonyesha mwenye elimu duni wengi wao ndio wapiga kura Wa Ccm nahisi ndio wanaisoma namba na kunyooka ila utu Wa mtu ni muhimu hueshimiwe na serikali japo kuwapa hifadhi ya muda au kuwalipia kodi walau ya mwaka wakati hili zoezi linaendelea ili wawezekujipanga upya kwa maisha ya mtu wa hali ya chini ni magumu sana.GENTAMYCINE kumbuka hata wakimbizi upewa hifadhi vipi mzawa ndani ya inchi yake.Mheshimiwa rais watazame wanainchi wako kwa jicho la pili. ndio wanamakosa ila mtoto akinyea mkono usiukate
 
Viwanja walivyopewa ni offer tu. Bomoa bila kupepesa macho. Kila mafuriko yanaleta madhara na emergency fund inatumika ambayo ingefanya kazi nyingine. Ukifurahi mwenzako kufukuzwa kazi kwa uzembe au rushwa jua hana tofauti na wewe unaejenga kwenye njia za maji. Bomoa, ushaambiwa sheria msumeno. Bomooooooaaaaaaa
 
Si Mlijifanya Kumuunga Mkono Yule Mpuuzi Wenu Sasa Mtaisoma Namba KISAWASAWA Hadi MTANYOOKA Tu. Na Bahati Nzuri Hata SHERIA Itawamaliza Tu Hivyo TIINI Tu Maamuzi Ya MAMLAKA au Kama Vipi Mwambieni Huyo Mtu Wenu Kuwa Hizo HELA au Hiyo Bajeti Anayotaka Kuitumia Kuzunguka Nchi Nzima Kuwashukuru NYUMBU Angeimega Tu Kidogo Ili Awapeni Mjenge Nyumba ILA Kwa Upande Wetu Mziki Ni Ule Ule Tu Wa HAPA KAZI TU!
Cjakuelewa unataka kutuaminisha kuwa utawala wa magufuri ni wakulipa kisasi kwa wale wasio mpigia kura??????? Usimtwishe dhambi magufuri si mtu wa mawazo kama yako, madhan usiaminishe watu hisia zako potofu.
 
Back
Top Bottom