Kuna walioko nyuma ya Rugimbana au ni jeshi la mtu mmoja?

Nafwachii

Senior Member
Aug 1, 2016
162
43
mnamo July 18, 2013 Habari Leo iliandika haya kumhusu huyu bwana

DC Rugimbana ashtakiwa CCM

KAMATI iliyoundwa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, (CCM) Abdulrahman Kinana kuchunguza sababu zinazokwamisha utekelezaji wa ilani ya chama hicho katika maeneo mbalimbali nchini, imekabidhiwa tuhuma nzito zinazomuhusisha Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana.

Tuhuma hizo zinahusu Taasisi anayoiongoza ya Umoja wa Vijana wa Kikristo Tanzania (UVIKIUTA) kudaiwa kutumia polisi na mgambo kupiga wananchi, kuwavunjia nyumba, kufyeka bustani za wajasiriamali na adhabu za kuwarusha kichura wanawake.

Katika Mkutano wa hadhara wa wanachama wa CCM na wakazi wa Mtaa wa Mkombozi Kata ya Kivule wilayani Ilala mkoani Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, wananchi waliiambia Kamati hiyo kuwa Rugimbana amesababisha watoto wao kutokwenda shule na wao kuishi chini ya mikorosho kwa zaidi ya miezi 10 sasa.

Kamati hiyo kutoka Makao Makuu ya CCM Dodoma ilioongozwa na Hussein Balyagati, ilipokea kero hizo kupitia kwa viongozi wa CCM wa eneo hilo wakiongozwa na Kamati ya siasa ya Kata ya Kivule.

Mmoja wa wananchi hao, Elia Mharagi alidai Oktoba mwaka jana, DC Rugimbana alisimamia uvunjwaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 700 uliofanywa na UVIKIUTA.

Naye Diwani wa kata hiyo, Nyansika Motena (CCM) alisema alichofanya Rugimbana ni matumizi mabaya ya madaraka kwa sababu sheria hairuhusu mtu mmoja kumiliki ardhi katika wilaya mbili tofauti na kuifanya kuwa moja.

Alipofuatwa, Rugimbana alisema yeye kama kiongozi wa Serikali hawezi kulizungumza kwenye vyombo vya habari kwa sababu bado halijafikia tamati ya sheria (mahakamani), lakini kuhusu kamati ya CCM kuchunguza suala hilo, atalizungumza kupitia vikao husika vya chama.

“Unajua mimi ni kiongozi wa Serikali kwa upande mmoja, lakini pia nafanya kazi zangu kwa kutekeleza ilani ya CCM hivyo siwezi… nikilisemea nitakuwa naingilia uhuru wa mahakama, na hili la kamati ya chama nitatumia mkondo wa vikao kulisemea huko” alisema Rugimbana.

Kesi ya mgogoro huo Na.32 ya mwaka 2012 ilifunguliwa na wananchi katika Mahakama Kuu ya Ardhi wakipinga uamuzi wa Baraza la Ardhi la Wilaya ya Temeke kuamuru wavunjiwe nyumba zao na UVIKIUTA wakidai haikuwa na mamlaka ya sheria kufanya hivyo.

UVIKIUTA nayo imefungua kesi mpya ya madai katika mahakama hiyo ikiwadai wananchi hao fidia ya zaidi ya Sh bilioni nne.


kifupi

huyu bwana ndiye anaye lalamikiwa na wananchi zaidi ya elf 3000 kuleta adha ya kubomolewa wananchi wa kivule lakini hakukuwa na suruhu yoyote iliyofanyika kwa jambo hili , awali kesi ya mgogoro huo kati ya wananchi na uvikuita(ikiongozwa na Rugimbana japo ofisi zake hazieleweki ziko wapi) iliyokuwa mahakama kuu no.32 ya mwaka 2013, inadaiwa wananchi walishinda kesi. uvikiuta walikata rufaa kwenda mahakama ya rufaa kitengo cha ardhi.

upload_2016-12-10_12-21-52.png



miaka 3 baadae (2016) baada ya bomoa bomoa ya kwanza na eneo hilohilo kesi ikiwa bado mahakamani

mnamo December mosi , mwananchi yaandika

By Muyonga Jumanne, Mwananchi mjumanne@mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamia ya wananchi wa eneo la Magole A, Kata ya Kivule wilayani Ilala wameachwa bila makazi baada ya nyumba zao kubomolewa bila taarifa kwa usimamizi wa askari wa Jeshi la Polisi, wakati mgogoro wa eneo hilo baina yao na Umoja wa Vijana wa Kikristo wa Usharika wa Kurasini (Uvikiuta) ukisubiri uamuzi wa mahakama.

Mgogoro huo pia una tatizo la mpaka kutokana na baadhi kuamini kuwa eneo hilo liko wilayani Temeke na wengine wilayani Ilala, huku mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akifuatilia wapigakura wake kwa siku ya tatu na mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala akisema liko chini ya mamlaka yake.

Bomoabomoa hiyo lilifanyika ikisimamiwa na polisi wa Temeke huku Waitara akidai eneo hilo lipo Ilala.

“Jumla ya nyumba 500 zimebomolewa hapa jana (juzi). Familia zote zimelala nje hawakuwa na mahala pa kujihifadhi pia haukutumika utaratibu wa kutoa taarifa mapema. Kisheria zinatolewa siku 14 kabla ya ubomoaji,” alisema Waitara.

Waitara alisema katika hati ya mahakama ya awali ilionyesha ni nyumba tano katika eneo hilo zilizotakiwa kubomolewa japo wahusika wa nyumba hizo hawakuwahi kuitwa mahakamani, ila katika utekelezaji nyumba 500 zimebomolewa.

Mgogoro wa eneo hilo ambalo lipo kwenye mpaka wa Temeke na Ilala uliingia katika ushindani wa mahakama baina ya Uvikiuta na wakazi hao, ukirindima katika mahakama tatu kisha Mahakama Kuu kuwapa uhalali wakazi hao kuendelea kuishi.

Mwaka 2013 Uvikiuta walikata rufaa Mahakama Kuu na shauri lao litasikilizwa leo ili kujua uhalali wa eneo hilo, wakati nyumba zikiwa zimeshabomolewa.

Waitara, ambaye pia ni mwenyekiti wa mtaa wa eneo hilo, alisema alipopata taarifa za bomoabomoa juzi, alifika eneo la tukio na kuhoji sababu za ubomoaji huo, lakini badala yake alitakiwa aende kituo cha polisi cha Chang’ombe kupata maelezo zaidi kutoka kwa Kamanda wa Temeke, Gilles Muroto.

Lakini alipofika kituoni, alitakiwa kutoa maelezo ya sababu za kuhoji ubomoaji huo na akawaeleza na akadai kuwa baadaye alishikiliwa kwa saa tisa mpaka alipopata dhamana saa 12:00 jioni kisha kuachiwa na kutakiwa kuripoti polisi jana saa 2:00 asubuhi.

“Leo nimefika ila nimepewa hati ya mahakama iliyo tofauti na ile ya juzi. Hii ya sasa inaonyesha Mahakama ya Ardhi ilitoa hukumu Juni 22 mwaka huu ila utashangaa bomoabomoa imefanyika. Huku ni kuwaonea wananchi,” alisema Waitara. Mmoja wa wakazi walioathirika na ubomoaji huo, Elizabeth Wilunge alisema alikuwa eneo la tukio wakati wa bomoabomoa, lakini hakuweza kuokoa kitu chochote.

“Kinachoniumiza ni fedha nilizokuwa nimehifadhi, kiasi cha Sh900,000, kwa ajili ya kikundi cha akina mama wanaoishi na virusi vya Ukimwi,” alisema Wilunge.

Wilunge alisema hata nyumba hiyo iliyobomolewa imetokana na mkopo, hivyo atalazimika kulipa wakati analala nje bila makazi.

“Mimi ndiye nilikuwa mweka hazina wa hicho kikundi na fedha zote ambazo zilikuwa zinatusaidia kuhakikisha tunazingatia tiba zimechukuliwa. Sasa tumerudishwa nyuma tena, hatujui tutafanyaje,” alisema Wilunge.

Zawadi Jacob, aliyehamia eneo hilo miaka minne iliyopita na ana watoto wanne ambao wote wanasoma, alilazimika kulala nje usiku wa kuamkia jana huku watoto wake wakishindwa kwenda shule baada ya nyumba yao kubomolewa na hawakufanikiwa kuokoa mali zao zilizokuwa ndani.

“Hatuna chakula, maji wala sehemu ya kulala. Tunaiomba Serikali itusaidie maana hatujui tutaenda wapi. Tangu tuhamie, hatukuwahi kuambiwa kama tutakuja kuhamishwa eneo ili ila sasa tunakuja kubomolewa,” alisema Jacob.

Felista Damasi. ambaye alihamia Julai, 2010 akiwa amejenga nyumba na duka la vifaa vya ujenzi, pia hakufanikiwa kuokoa bidhaa zilizokuwa dukani ambavyo vimeharibiwa na vingine kutupwa nje wakati akiwa hayupo eneo hilo.

“Kuna watu walinifuata wakaniambia niwape Sh40,000 lakini nilikataa kuwapa na wakaendelea na zoezi lao la kubomoa. Mpaka sasa mimi, mama yangu na watoto wangu mapacha tunaishi katika mazingira magumu maana mume wangu amesafiri,” alisema Damasi.

Diwani wa Kivule, Wilson Molel alisema polisi waliofanikisha ubomoaji huo wanatoka Temeke na waliagizwa na Kamanda Muroto, ila hawakupewa ushirikiano wa kutosha katika yale waliyohoji. Hivyo aliwataka wananchi hao kujitokeza mahakamani leo kusikiliza hukumu yao.

“Hatukupewa ushirikiano na polisi wa hapa, Walituambia twende polisi Chang’ombe. Ila kesho haki itapatikana maana hawa wananchi wametuchagua kwa upande wa Ilala tutawatumikia kuhakikisha haki yao inapatikana,” alisema Molel. mwisho


Rugimbana alipotafutwa na ITV kuongerea hili kwa mara nyingine alichomoa na kudai amemsindikiza raisi hayuko kwenye nafasi nzuri ya kuliongelea hilo
anaria report ya sam mahera wa ITV hapa




tafakari yangu
kwanini viongozi wote hawajaonekana kwenye eneo la tukio au kusema chochote licha ya wananchi kwenda mpaka kwenye baadhi ya ofisi zao? mfano RC,DC n.k isipokuwa mbunge wao
Huyu bwana si mkono mmoja, lazima kuna mikono mirefu zaid nyuma yake

nini maoni yako?
karibuni wana jamvi
 
Huyo ni kada wa CCM, na hao ni wanaCCM wenzake, hivyo hakuna jipya litakalofanyika.
Kada wa CCM hawezi kuadhibiwa ovyo ovyo.
 
Wakati mwingine mnachosha watu, kwa akili ya kawaida unadhani miaka yote na siku zote na kila siku ambapo ccm wamekua wakitesa wananchi wake leo ndo wawe na uchungu nao?
 
kwan kwa CCM kipaumbele ni makada kwanza si wananchi kama ilan inavyodai?
Sera ya CCM ni CCM kwanza mambo mengine baadaye. Usitegemee CCM inaweza kumtosa kada wake ili kuwafurahisha wananchi.
Ukitaka kuwa salama katika nchi hii wewe kuwa kada wa CCM tu, utalindwa hadi na vikosi vya jeshi.
 
Sera ya CCM ni CCM kwanza mambo mengine baadaye. Usitegemee CCM inaweza kumtosa kada wake ili kuwafurahisha wananchi.
Ukitaka kuwa salama katika nchi hii wewe kuwa kada wa CCM tu, utalindwa hadi na vikosi vya jeshi.
Nakuelewa sana mkuu kwan tumeona makada wengi wakivunja sheria na vyombo husika vikizibwa midomo
 
Back
Top Bottom