nzahaksm
Member
- Dec 2, 2018
- 14
- 29
Hii njia sasa imeshakuwa kero kwa wananchi. Haipiti siku bila kutokea ajali eneo la mzinga darajani mpaka kongowe. Wiki iliyopita lori lilifeli breki na kusomba wapita njia na kuwaingiza mtoni. Zaidi ya watu 5 walifariki hapo hapo. Wiki iliyopita nyuma yake lori liliangukia bajaji na wakapotea abiria watatu na dereva papo hapo.
Leo lori tena limefeli na kuingia kwenye mtaro na kufunga njia kabisa zaidi ya masaa magari yapo kwenye foleni
Changamoto ni njia nyembamba na kuna mlima. Lakini pia kwa chini kuna daraja ambalo linafanya hata service road isiweze kufanya kazi mpaka labda daraja litanuliwe.
Niiombe Serikali kuitupia jicho hii njia na kuipanua walau kuanzia mbagala mpaka kisemvule kwa hatua ya mwanzo . Wakianza na utanuzi wa daraja liruhusu service road ziweze kuunganisga kupita darajani itasaidia sana .
Wananchi wameshachoshwa na kero hii kuna sku wataonesha hisia zao kwa pamoja na itakuwa too late kwa kuwa madhara mengi yameshatokea. Serikali inahitaji vifo vingapi ili kulifanyia kazi hili??