Ni muda sasa serikali ifikirie upanuzi wa Barabara ya Mandela

mozeh

JF-Expert Member
Mar 13, 2022
494
952
Wasalam wana jukwaa

Moja kwa moja niende kwenye mada.. aisee hii barabara kwa watumiaji tunaoitumia ni kero kubwa sana haswa foleni zisizo na mpango.

Suluhisho ni serikali kufanya upanuzi wa njia nne kwenda Ubungo na njia nne kutoka Ubungo to Tazara haya maflyover sijui interchange hayatokuja kutatua shida ya foleni kwenye barabara hii zaidi ya sifa tu za kisiasa..

Kingine barabara hii ni moja ya kitovu cha uchumi maana inaunganisha malori yanayotoka bandari kuelekea mikoani so ili tuchocheee maendeleo hakuna budi zaidi ya kupanua barabara.

Nawasilisha.
 
Hii Nchi mipango yake ni zero kabisa,angalia hata Morogoro Road muda watu wanaopoteza.
Acha tu mkuu.. sitaki kuamin nchii hatuna watu smart wa kufanya mambo kiubora ila ndo ivo mifumo haiwataki watu ambao wako smart
 
Wasalam wana jukwaa

Moja kwa moja niende kwenye mada.. aisee hii barabara kwa watumiaji tunaoitumia ni kero kubwa sana haswa foleni zisizo na mpango.

Suluhisho ni serikali kufanya upanuzi wa njia nne kwenda Ubungo na njia nne kutoka Ubungo to Tazara haya maflyover sijui interchange hayatokuja kutatua shida ya foleni kwenye barabara hii zaidi ya sifa tu za kisiasa..

Kingine barabara hii ni moja ya kitovu cha uchumi maana inaunganisha malori yanayotoka bandari kuelekea mikoani so ili tuchocheee maendeleo hakuna budi zaidi ya kupanua barabara.

Nawasilisha.
Barabara ya Mandela Road
 
Kituo cha daladala pale Reverside imekuacha Chanzo cha Tatizo Hilo

Daladala ndio wanaleta msongamano wote pale

Solution ni kurudizsha kituo pembeni na pawepo na faini

Manzese pia daladala ndio chanzo cha foleni isiyo na ulazima
 
Kulikuwa na plan ya kujenga barabara kutoka bandarini ya njia sita ya kupitia maeneo ya Kitunda kuelekea Pugu na kiwanja changu kilikuwa marked ili kupunguza foleni ya Mandela road. Mpaka leo sijasikia chochote na hakuna mtu aliyetusemesha tena.
 
Back
Top Bottom