Serikali isikwepe uwajibikaji kwenye ajali za majini; chanzo cha ajali hizi ni uzembe wa watendaji wake!!!

Tarehe 21.05.1996, MV Bukoba ilizima ikiwa takribani kilomita 53 kutoka nchi kavu. Watanzania 894 walipoteza maisha. Ripoti zinaonesha kuwa, meli hiyo ilikuwa imezidisha shehena kuliko kiwango stahiki cha meli yenyewe.

Tarehe 30.5.2009, boti iliyokuwa inamilikiwa na kampuni la Seagul, MV Fatih, ilipinduka punde ilipokuwa ikijiandaa kutia nanga bandari ya Malindi. Watu sita walikufa. The Citizen liliwahi kutaarifu kuwa, boti hiyo ilikuwa na mzigo mkubwa kuliko uwezo halisi wa boti hiyo.

Tarehe 10 ya Septemba, 2011, MV Spice Islanders I, iliyokuwa ikifanya safari yake kutokea Unguja kwenda Pemba, ilibinuka. Taarifa rasmi zinasema, abiria 200 walikufa maji, ingawa taarifa za kiuchunguzi zinadai, zaidi ya watu 1500 walipoteza maisha. Chanzo cha ajali hiyo kilikuwa ni. "overloading", meli ile ilikuwa imebeba abiria zaidi ya 2,000 kuliko uwezo wa meli yenyewe ambao inadaiwa ulikuwa ni watu 1,000. Pia kulikuwamo tani kadhaa za mizigo zenye uzito kuliko uwezo wa meli yenyewe.

Tarehe 18 Julai, 2012, MV Skagit ilibinuka karibu kabisa na kisiwa cha Chumbe. Chanzo cha ajali ile ni upepo na " mzigo mkubwa". Inaelezwa, meli ile ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 250, lakini siku ya ajali ilikuwa na abiria zaidi ya 290. Abiria 136, kwa mujibu wa taarifa rasmi, walipoteza maisha.

Januari 9, 3017, watu 30 walipoteza maisha kwenye boti Bahari ya Hindi, iliyokuwa ikifanya safari yake kutokea Tanga kwenda Pemba. Boti ile ilikuwa na uwezo wa kubeba abiria 25, lakini siku ya ajali, boti ile ilikuwa na abiria 50.

Tarehe 23 ya Disemba 2017, watu 22 walipoteza maisha Ziwani Tanganyika, wakisafiri kwa boti. Uwezo wa boti ile ulikuwa ni watu 30, lakini siku ya ajali, boti ile ilikuwa na watu 65.

Septemba 20, 2018, MV Nyerere, inayofanya safari zake kwenye visiwa vya Ukerewe na Ukala, ziwani Victoria, ilizama. Abiria, hadi kufikia muda huu, 196 wamepoteza maisha. Chanzo cha ajali hii ni ujazo mkubwa kuliko uwezo wa meli. Uwezo wa meli ni abiria 101, lakini siku ya ajali, meli ilikuwa na watu zaidi ya 400. Cha kuchekesha zaidi, hata kitabu cha abiria alisafiri nacho mkatisha tikiti, kwa hiyo hakijukikani kilipo. Wakati shughuli za uokoaji, mkuu wa mkoa, mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa wa Mwanza, John Mongela, akasitisha shughuli hizo kutokana na kinachodaiwa kukosekana kwa taa. "Resume" ya uopoaji miili ya wafa maji imefanikiwa kumuokoa fundi mkuu wa meli ile, ambaye amekaa ndani ya maji kwa zaidi ya masaa 30.

Serikali inakwepaje kuwajibika kwa hili?

Mosi, mlolongo wote wa ajali za maji (marine accidents) zinaonesha chanzo kikubwa kuwa ni ujazo wa mizigo na abiria kuliko uwezo wa chombo chenyewe. Tunao SUMATRA, tafsiri yake haiwajibiki, kwa hiyo serikali imeshindwa kutimiza wajibu wake.

Pili, kwa miaka 22 leo, serikali imeshindwa kabisa kujifunza kitu toka ajali ya MV Bukoba. Ujazo wa abiria na mizigo ni ishara kuwa, kuna uhaba wa vyombo vya majini, na hata hivyo vilivyopo ni vibovu, kwani siku nyingi havifnyiwi ukarabati. Wawakilishi wa wananchi wakidai ukarabati, serikali inawapuuza kwa kuwa ni waumini wa siasa za *mrengo wa kushoto*, na hivyo kwa makusudi kabisa kuwanyima fedha za maendeleo.

Tatu, serikali, kwa miaka 22 toka ajali ya MV Bukoba, imeshindwa kabisa kutimiza wajibu wake wa kujali haki ya watu kuishi, ambayo ni wajibu wake namba moja, yaani "fulfillment". Karibu ajali zote, uokoaji umekuwa ni msaada kutoka nje. Nimeshuhudia MV Spice Islanders I na MV Skagit, ambapo wataalamu wa majini kutoka A. Kusini walitoa msaada kwa kiwango cha hali ya juu sana.

Leo inasikitisha sana kuwa, inafikia hatua shughuli za uokoaji zinasimama kwa kukosa *taa*, hii ni fedheha kubwa kwenye haki ya watu kuishi. Usafiri wa majini ni muhimu kuliko bombardier, dreamliner na madege mengine, kwani usafiri huu hutumiwa na wananchi wengi wa kipato cha chini kuliko hayo madege.

Nne, itikadi za kuwapuuza wanasiasa wa mrengo wa kushoto ni kuhatarisha haki ya watu kuishi, kuwanyima haki yao ya maendeleo, kuwadhulumu haki yao ya msingi ya kugawana kwa usawa rasimali za nchi. Ingawa tunaombwa tusilifanye tukio hili kuwa la kisiasa, lakini tunasahau kuwa siasa ni maisha. Mbunge aliomba kwa lugha nzuri kabisa fedha za ukarabati wa MV Nyerere, akapuuzwa tu kwa kuwa ni wa chama fulani kinachobishana na chama cha mrengo wa kulia.

Tano, serikali kuanza kulaumu " day worker" aliyekuwa nahodha wa meli hiyo ni kukwepa uwajibikaji wake. Chanzo yawezekana siyo "day worker", ila " overload" ambayo ilitakiwa kudhibitiwa na serikali kwa;
(a) vyombo vyake na wizara yake kuwajibika ipasavyo, na;
(b) kuwaongezea wananchi wale meli nyingine ambayo zingekuwa zinapishana, ili kuwahakikisha usafiri muda wote.

Watanzania tunaumia. Kwa kuwa ni utamaduni wetu kushikana mkono kwenye misiba kama hii, na kwa kuwa serikali ilishindwa kuwajibika kabla ya uhai wa abiria hawa, watanzania, haujaondoka, basi hakuna haja ya serikali kuonesha wajibu wake kwenye rambirambi. Sisi ni watanzania. Tuende mmojammoja ama kwa makundi kuwafuta wenzetu machozi, moja kwa moja, kuliko kuwafuta machozi kupitia mikono ya serikali.

Serikali isikwepe kabisa wajibu wake kwa kujificha kwenye rambirambi, achilia mbali kuwa rambirambi zenyewe huwa ngumu kufika sehemu husika kama ilivyokuwa kwa watoto wa Lucky Vincent na Tetemeko la Kagera; ione namna kabambe ya kuwajibika moja kwa moja. It should not be sympathetic; it must be empathetic. It has to strictly nag the irresponsibles central to the accident! Irekebishe iliposhindwa kurekebika kwa miaka 22 toka ajali ya MV Bukoba!
Nakuomba siku uje pale Kimara asubuhi kama saa moja kuelekea saa mbili uone mwendokasi inabeba watu 300+ kwa gari moja ila hakuna cha SUMATRA wala askari ambao wapo pale hivyo sikio la kufa halisikii dawa

Bahati mbaya ikitokea Mwendokasi (na vile vi njia vyao vyembamba na huduma za EXPRESS) ika fail basi itakuwa wote wale tunaosimama tutakuwa wa kwanza kwanza kuumia kama sio kufa au kuwa vilema

Tatizo kubwa ni kuwa hakuna magari ya kutosha na hakuna namna itabidi kupanda tu magari yaliuojaa ndo mfumo uliopo
 
Ni wakati sasa wa kuhakikisha ,Abiria wote kabla ya kuingia kwenye hivi vyombo vya majini wavae Life Jackets ajili ya usalama wao.

Itasaidia kupunguza vifo pindi ajali zinapotokea.
 
saizi anatafutwa mbuzi wa kafara wa kubeba lawama yote na kutumbuliwa,na tume ya kuchunguza tukio,eidha inaandaliwa ama ipo tayari.hii ndio bongo,reactive instead of active.
 
Hapana mkuu hii inatoksna na mbunge kushinikiza kufunga engene kubwa kuongeza speed. Mwanzoni ilikuwa inatumia saa moja sasa hivi ilikuwa ikitumia robo saa mara nne ya manufacture design. Yaani TATA kufungwa engene ya scania.

Pili ni hili la daiwaka kuchati na simu wakati akiendesha chombo angalia kiliko angukia ni mbali kabisa na gati.

Kusema mizigo ilizidi hili sikubaliano nalo chombo kina uwezo wa kubeba tani 28. Hao watu mia nne hawawezi kuwa na zaidi ya tani 28 hata iweje

Kwahiyo unataka kusema kilo moja ya mawe sio sawa na kilo moja ya manyoya ya kuku
 
Hapana mkuu hii inatoksna na mbunge kushinikiza kufunga engene kubwa kuongeza speed. Mwanzoni ilikuwa inatumia saa moja sasa hivi ilikuwa ikitumia robo saa mara nne ya manufacture design. Yaani TATA kufungwa engene ya scania.

Pili ni hili la daiwaka kuchati na simu wakati akiendesha chombo angalia kiliko angukia ni mbali kabisa na gati.

Kusema mizigo ilizidi hili sikubaliano nalo chombo kina uwezo wa kubeba tani 28. Hao watu mia nne hawawezi kuwa na zaidi ya tani 28 hata iweje
Hilo la kuchat na simu,!!!kivuko /meli hakiendeshwi kama gari kuwa muda wote wewe na sukani na gia, kuhusu kuwa eti kilikuwa mbali na gati huo ni mtizamo wako, kwani kuna njia zake sio kuwa kama gari, kuhusu ku overload, inawezekana ndio sababu kubwa kwani, kilikuwa na uwezo wa kubeba tani25, za mizigo na abiria 101!! Hapo kuna kama abiria 260!!hadi sasa, na kilikuwa kinatoka gulioni inawezekana ka mtu alikuwa na mzigo, kulikuwa na magunia ya mahindi, kulikuwa na canter imejaa mizigo kulikuwa kuna nguzo za umeme!!!
 
Naamini matukio haya yote yaliundiwa tumebau Kamati za ucgunguzi na taarifa kutolea kwa serikali kupitia taasisi husika. Lakini matokeo ya Kazi hayawekwi bayana hata kwa mihtasari. Watu wangependa kujua kiini au kisababishi cha ajali na mapendekezo kudhibiti aina ya ajali hizo



Hivi ndivyo wenzetu wanavyofanya. Taarifa zinatayarishwa na wataalam na zinawekwa wazi ili watu wajifunze na wachangie. Lengo si kutafuta mchawi bali kama ilivyosemwa hapo juu ni kutafuta kiini ili hatua zichukuliwe kuzuia ajali kama hiyo kutokea tena.

Amandla.............
 
MV nyerere haikuanza leo kubeba abiria wengi zaid ya kiwango chake. Mimi nmetumia sana hiki kivuko abiria wamekuwa wakijaa na hata wakati mwingine ukiangalia kwa macho ni zaid ya watu mia 4.

Serikal imekuwa ikipokea mapato kupitia kivuko hiki na wanajua kabisa kimekuwa kikilazimika kubeba zaid ya uwezo wake.

Mfano leo ukiangalia Mwendo kasi zinavyoshona watu utadhan mahindi kwenye gunia, siku likipata ajal na kuuwa watu wa kutosha ndyo utasikia serkal inasema ilibeba zaid ya kiwango chake. Dreva ataftwe.
 
Hapana mkuu hii inatoksna na mbunge kushinikiza kufunga engene kubwa kuongeza speed. Mwanzoni ilikuwa inatumia saa moja sasa hivi ilikuwa ikitumia robo saa mara nne ya manufacture design. Yaani TATA kufungwa engene ya scania.

Pili ni hili la daiwaka kuchati na simu wakati akiendesha chombo angalia kiliko angukia ni mbali kabisa na gati.

Kusema mizigo ilizidi hili sikubaliano nalo chombo kina uwezo wa kubeba tani 28. Hao watu mia nne hawawezi kuwa na zaidi ya tani 28 hata iweje
Uzito wa watu 400 kwa wastani wa kg 70 kila mtu ni:
70x100= kg 7,000
7,000×4= kg 28,000
Kwahiyo Idadi ya abiria tu ilikuwa sawa na uwezo wa chombo tani 28,000!
Lakini meli ilikuwa na mizigo ya abiria na shehena ya mahindi na nyanya na magari kadhaa. Vitu hivyo hukuvitaja makusudi.
Mmeanza kupotosha mambo!
 
Sio kila kitu lawama ziende serikalini. Na sisi abiria tunapaswa kubadilika, watu wakiona meli imekaribia kufika pwani, wanaanza kusogea mbele pasipo utaratibu.

Uzito ukihamia upande mmoja ni rahisi sana meli kupinduka. Watu wakitulia hata kama meli imejaa kupita uwezo, upo uwezekano wa abiria kufika salama mwisho wa safari.
 
Uzito wa watu 400 kwa wastani wa kg 70 kila mtu ni:
70x100= kg 7,000
7,000×4= kg 28,000
Kwahiyo Idadi ya abiria tu ilikuwa sawa na uwezo wa chombo tani 28,000!
Lakini meli ilikuwa na mizigo ya abiria na shehena ya mahindi na nyanya na magari kadhaa. Vitu hivyo hukuvitaja makusudi.
Mmeanza kupotosha mambo!
Jamani acheni porojo hicho kisiwa masikini hakina gari hata moja usafiri wa huko ni toyo tu. Hiyo shehena gani ya kupelekwa ukara? Tangu lini mkara akala ugali hebu wacheni porojo
 
Sio kila kitu lawama ziende serikalini. Na sisi abiria tunapaswa kubadilika, watu wakiona meli imekaribia kufika pwani, wanaanza kusogea mbele pasipo utaratibu.

Uzito ukihamia upande mmoja ni rahisi sana meli kupinduka. Watu wakitulia hata kama meli imejaa kupita uwezo, upo uwezekano wa abiria kufika salama mwisho wa safari.
Wanatakiwa wawe wanatoa Elimu hiyo, Mbn kwenye Ndogo elimu ya kujiokoa inatolewa kabla ya Safari


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom