Serikali isambaratishe vijiwe vyote Mwanza ni chanzo cha umaskini

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,902
51,995
Mkoa wa Mwanza umeripotiwa kuwa mmoja wa mikoa inayoongoza Tanzania yenye umaskini uliotopea.Na mojawapo ya chanzo ni vijiwe vilivyozagaa mjini Mwanza ambako watu hukaa bila kufanya kazi.

Serikali kupitia Jeshi la polisi isambaratishe vijiwe vyote kwani vinaletelea umaskini wa huo mkoa.

Zoezi hilo si geni hata majiji mengine limeshafanyika huwezi kukuta watu wako tu vijiweni.Nenda mkoa wa Kilimanjaro huwezi kukuta watu wamezagaa tu vijiweni hakuna kitu kama hicho.

Defender za polisi zifanye hilo zoezi kwa kushirikiana na manispaa.

Zoezi hilo lifanyike haraka ili kuendana na spidi ya Raisi ya hapa kazi tu ili Mwanza nayo kama ilivyo Kilimanjaro kusiwe na vijiwe.
 
Swala sio kusambaratisha vijiwe bali ni kuhamasisha watu wachape kazi, vijiwe ni muhimu baada ya kazi kwakuwa watu wanapata kubadilisha mawazo.
 
Nadhani mtoa mada umeishia mwanza tu na kilimanjaro ndo ukaona bora ulinganisha mikoa hiyo miwili, lakini umewahi kufika Tanga na mikoa mingine ya pwani!!? kuna sehemu yenye vijiwe kama maeneo ya huko? kila baada ya hatua 15 utakutana na kijiwe iwe cha kahawa na kashata au bao. ila mbona hairipotiwi kama kuna umasikini? nadhani kuna kitu kingine kinachosababisha umasikini na sio vijiwe.
 
Swala sio kusambaratisha vijiwe bali ni kuhamasisha watu wachape kazi, vijiwe ni muhimu baada ya kazi kwakuwa watu wanapata kubadilisha mawazo.

Unanichekesha.Ni kama jirani yangu akiaga nyumbani kwake kwenda baa anasema naondoka kidogo nikatoe mawazo.Mtu akitoa mawazo anabakiwa na nini si anakuwa mwehu tu.Na mtu kusingizia anaenda kubadilishana mawazo na wenzie baa si kweli.Kubadilishana mawazo mtu anatakiwa kuwa ana akili timamu sio kakolea kiroba ndio anaanza kubadilishana mawazo na wengine.Watu wakilewa kila mtu hujiita Kivyake kutegemea pombe inakompeleka utawakuta wanaojiita kazi zao washauri wa Magufuli au UKAWA,NK utapata ID FAKE kibao na zikiongea kwa kujiamini wakati sio.

Kijiweni pia si sehemu salama ya kubadilishana mawazo.

Ukitaka kupata mawazo mazuri hudhuria semina ,warsha,nk zinazohusu kitu unachotaka kukijua au soma au badilishana mawazo ukiwa kazini nk sio vijiweni
 
Mkoa wa Mwanza umeripotiwa kuwa mmoja wa mikoa inayoongoza Tanzania yenye umaskini uliotopea.Na mojawapo ya chanzo ni vijiwe vilivyozagaa mjini Mwanza ambako watu hukaa bila kufanya kazi.

Serikali kupitia Jeshi la polisi isambaratishe vijiwe vyote kwani vinaletelea umaskini wa huo mkoa.

Zoezi hilo si geni hata majiji mengine limeshafanyika huwezi kukuta watu wako tu vijiweni.Nenda mkoa wa Kilimanjaro huwezi kukuta watu wamezagaa tu vijiweni hakuna kitu kama hicho.

Defender za polisi zifanye hilo zoezi kwa kushirikiana na manispaa.

Zoezi hilo lifanyike haraka ili kuendana na spidi ya Raisi ya hapa kazi tu ili Mwanza nayo kama ilivyo Kilimanjaro kusiwe na vijiwe.
MUONGO mkubwa! nani amekueleza umaskini ulioripotiwa kwa mkoa wa Mwanza unasababishwa na vijiwe vilivyozagaa mjini Mwanza? Kwani mikoa ya Dar, Kilimanjaro, Arusha, Pwani na Manyara ambayo imetajwa kuwa na maskini wachache hakuna vijiwe? Huu umaskini unaolezwa is not justifiable maana umaskini wa kipato unapimwa kwa mapato ya mwaka mzima ambapo unakuta wananchi wengi wa mikoa iliyotajwa kuwa na umaskini zaidi ikiwemo Mwanza wako chini ya dola moja kwa siku kimapato.

Sasa unahusishaje mtu kuwa kijiweni na kuwa maskini? Wewe hujui kama kuna watu wanamiliki mikokoteni labda kumi kwa mfano lakini anakuwa kijiweni huku mikokoteni yake inaingiza pesa. Au mtu anakuwa kijiweni lakini ana bodaboda zake tano zinapiga mzigo?

Kwanini usiishauri serikali ya "Hapa Kazi Tu" kupeleka wataalamu wa kutosha vijijini kuwafundisha/kuwashauri wakulima kuendesha kilimo kinachoweza kuwa na manufaa kwao kama vile "green house". Tatizo la mkoa wa Mwanza sio vijiwe bali ni kukosekana kwa mazao yanaingiza fedha kwa wingi kama ilivyo kwa ngano, ufuta na kahawa kwa mikoa ya Arusha, Kilimanjaro na Manyara. Sababu nyingine ni wakulima kutegemea mvua wakati kumekuwepo na mabadiliko makubwa ya hali ya hewa kiasi cha kuathiri misimu ya mvua.

Najua andiko lako linalenga kuishauri serikali iondoe vijiwe kama njia ya kusaidia kufurusha vijana waliojikatia tamaa kutokana na mifumo mibovu ya elimu inayowafanya wengi kukosa maarifa na mitaji ya kuwa na shughuli za uzalishaji mali na hivyo kujikuta wanaunga mkono siasa za upinzani. (Rejea kukamatwa kwa Mbowe na viongozi wengine wa Chadema huko Mwanza jana).
 
Mkoa wa Mwanza umeripotiwa kuwa mmoja wa mikoa inayoongoza Tanzania yenye umaskini uliotopea.Na mojawapo ya chanzo ni vijiwe vilivyozagaa mjini Mwanza ambako watu hukaa bila kufanya kazi.

Serikali kupitia Jeshi la polisi isambaratishe vijiwe vyote kwani vinaletelea umaskini wa huo mkoa.

Zoezi hilo si geni hata majiji mengine limeshafanyika huwezi kukuta watu wako tu vijiweni.Nenda mkoa wa Ki.
Kwa hiyo wewe upeo wako unakomea hapo?! Umeshindwa kuona matatizo ya usalama, ukosefu wa ajira, biashara kuganda (bidhaa kutonunuliwa kutokana na watu kukosa uwezo wa kununua), mapato ya nchi kushuka kiasi cha serikali kutaka kupora mapato ya serikali za mitaa ili kulinda shoo ya takwimu za ukusanyaji mapato kila mwezi, udikteta ukishika kasi (wengine mkiendelea kushangilia mtego wa panya), uhaba wa sukari na matokeo yake, uongo kuwa elimu ni bure, nk. Hayo yote akili yako haijayaona?!! Pole sana.
 
Unaonaje uanzishe thread yako Uyachambue hayo yako lukuki? Mimi nimechukua moja tu la kijiweni wewe anzisha yako uyajadili na kuyachambua hayo mengine
 
Acheni watu wake kijiweni wakisubiri ajira za viwandani, mnataka vijana wakae jikoni na mama zao? Haa huu tena si uoga bali ccm inajiaibisha.
 
Mkoa wa Mwanza umeripotiwa kuwa mmoja wa mikoa inayoongoza Tanzania yenye umaskini uliotopea.Na mojawapo ya chanzo ni vijiwe vilivyozagaa mjini Mwanza ambako watu hukaa bila kufanya kazi.

Serikali kupitia Jeshi la polisi isambaratishe vijiwe vyote kwani vinaletelea umaskini wa huo mkoa.

Zoezi hilo si geni hata majiji mengine limeshafanyika huwezi kukuta watu wako tu vijiweni.Nenda mkoa wa Kilimanjaro huwezi kukuta watu wamezagaa tu vijiweni hakuna kitu kama hicho.

Defender za polisi zifanye hilo zoezi kwa kushirikiana na manispaa.

Zoezi hilo lifanyike haraka ili kuendana na spidi ya Raisi ya hapa kazi tu ili Mwanza nayo kama ilivyo Kilimanjaro kusiwe na vijiwe.
Wewe unajua zilikotoka kura za akina Mabula mwanza ?
 
Vijiwe kwa kweli kwa asilimia kubwa huchangia umaskini japo wapo wachache washindao Vijiweni wakiwa na mishe za maana kwingineko.
 
Tulizoeshwa kuitegemea serikali kwa kila kitu iwe ajira au shughuli nyingine. Sasa itachukua muda mrefu kubadilisha your mind set probably a generation
 
Tatizo sio vijiwe, bali ni
1.Njia kuu za uzalishaji mali kumilikiwa na watu wachache.
2.Kuongozeka kwa idadi ya watu kuliko uwezo wa rasilimali zilizopo (Ardhi, Kazi /Ajira, Miundombinu)
3.Idadi kubwa ya wakazi kufanya biashara aina moja.
4.Kukosekana kwa miundombinu ya barabara inayoliunganisha jiji lote kimanispaa.
5.Geographia ya jiji kuhitaji miundombinu yenye kughalimu fedha nyingi (makazi).
6.Jamii nyingi bado zinaishi kijamaa/nzengo hivyo kusababisha utegemezi uliokithili.
7.Karibu 75 per cent ya makazi kutokupimwa hivyo kuwafanya wananchi wasikopesheke kwenye taasisi za fedha.
8.Uvivu wa baadhi ya watu kutokufanya kazi kwa kuwategemea ndugu, jamaa na rafiki.
9.Dhuluma na ubabe kwa baadhi ya watu wanaojifanya miungu watu.
10.Kukosekana kwa maadili na nguvukazi inayopotea kutokana na dawa za kulevya, pombe na ngono zembe.
11.Idadi kubwa ya wakazi kuathiliwa na siasa za visasi.
12.Kuongezeka kwa wakazi hasa wale wa wanaotoka nchi jirani (Ukanda wa Maziwa Makuu) kutokana na athali za vita na mapigano ya mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom