Serikali irudishe Annual Increment na ipandishe madaraja Kwa wakati, iachane na nyongeza ya mishahara kwani haiwezi

Retina

JF-Expert Member
Mar 6, 2015
1,038
1,154
Moja ya malalamiko ya wafanyakazi wa umma ni hili la kuondolewa Kwa annual increment na serikali, ambayo ipo kisheria huku huku ikishindwa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma, inayokidhi hali ya sasa.

Uwepo wa increment kwenye mishahara imetoa uzoefu kazini, nikiwa na maana kuwa hakuna senior na junior kazini, mtu anaweza kuwa ameanza kazin zaidi ya miaka mitatu ya mwingine lakini wote wana mshahara sawa.

Lakin pia, serikali iachane na nyongeza ya mishahara kama inaona haiwezi au inaogopa mfumuko wa bei, basi iwapandishe madaraja watumishi wake mapema kwani hii huwa ni Siri kati ya mwajiriwa na mwajiri, haiitaji kutangaza sana kama nyongeza inavyotangazwa hivyo kusababisha mfumuko wa bei n.k.
 
Pamoja na uwepo wa annual increment nyongeza ya mshahara ya Mei Mosi ilikuwepo pia.
 
Ila watumishi mna viterminology vingi mara annual increment mara malimbikizo!Mwaka huu mwanzoni mliimba sana suala la madaraja ya mserereko ajabu imesomwa bajeti ya utumishi na utawala bora waziri wala naibu waziri hajagusia popote kuhusu kuserereka kwa watumishi mnaosema walinyang'anywa madaraja yao mwaka 2016 ukweli mchungu hakuna kitu kama hicho ingekuwa kweli waziri angesema kwenye mpango wake wa budget ya 2023/2024
 
Moja ya malalamiko ya wafanyakazi wa umma ni hili la kuondolewa Kwa annual increment na serikali, ambayo ipo kisheria huku huku ikishindwa kuwaongezea mishahara watumishi wa umma, inayokidhi hali ya sasa.

Uwepo wa increment kwenye mishahara imetoa uzoefu kazini, nikiwa na maana kuwa hakuna senior na junior kazini, mtu anaweza kuwa ameanza kazin zaidi ya miaka mitatu ya mwingine lakini wote wana mshahara sawa.

Lakin pia, serikali iachane na nyongeza ya mishahara kama inaona haiwezi au inaogopa mfumuko wa bei, basi iwapandishe madaraja watumishi wake mapema kwani hii huwa ni Siri kati ya mwajiriwa na mwajiri, haiitaji kutangaza sana kama nyongeza inavyotangazwa hivyo kusababisha mfumuko wa bei n.k.
Aliyeondoa annual increment kama alivunja sheria awajibike kulipa wote waliostahili kupata hizo nyongeza ikibidi hata mali zake ziuzwe
 
Pesa nyingi ambazo zingeenda kulipa stahiki za watumishi zikiwemo annual incements na kupanda madaraja zinapigwa na majizi kupitia miradi ya serikali na manunuzi, serikali iangalie uwezekano wa kujikita kulipa stahiki za watumishi kwanza kabla ya kutoa pesa kwenda kutekeleza miradi na kufanya manunuzi ambayo kimsingi inaonekana ni wizi mtupu unaofanyika huko.​
 
Back
Top Bottom