Serikali ipunguze muda wa kazi kwa watumishi wa umma kutoka saa 8 mpaka saa 6

roadmaster

JF-Expert Member
Mar 21, 2023
1,484
2,573
Hali ya mtumishi Tanzania kuanzia wakati kutoka awamu iliyopita mpaka Sasa ni Tete!! Serikali ya Magufuli ilishindwa kuongeza mishahara Kwa kipindi cha uhai wake akiwa kama Rais wa nchi!!

Tatizo hili linajirudia tena na tena, ambapo hata kanachoitwa annual increment ambayo ni haki ya msingi haipo tena!!!

Niishauri serikali ni muda muafaka Sasa ipunguze muda wa kufanya kazi ili watumishi wanalalama wapate muda wa kuingia mtaana na kuisaka shilingi Kwa udi na uvumba!! Badala ya masaa nane Sasa yapungue na yabaki matano tuu!!

Watumishi wengi wanashughuli mbalimbali kama udereva Noah, udereva pikpiki, mashine za kusaga,sheli bubu,saloon,kukaanga vihepe,aka chips,nk!! Niwazi kama watatia nguvu kwenye usimamizi wataongeza vipato hivyo kupunguza ukali wa maisha uliosababishwa na serikali kujishindwa!!
 
Tatizo la binadamu ni kujiangalia yeye....

Ili ufahamu uzuri au ubaya wa kuwa mtumishi acha kazi uone wangapi wataitaka kazi yako !!!, Kuna kipindi ualimu, uaskari uanajeshi watu walikuwa wakipangiwa hawaendi; sasa hivi mpaka wanahonga...

Kwahio ili kuondoa mzizi wa tatizo its about time serikali iache kukaa likizo na kupiga udalali na kuja na sera ambazo zitaleta ajira zenye ujira wa kutosha kwa majority ya watu...

Sisemi watu wawe matajiri.., bali middle income iongezeke sasa hivi kuna watu wa kula na kuzaza wengine hata makombo hawana....., Extreme Poverty anywhere is a threat to to Human Security Everywhere....
 
Ikiwezekana serikali iongeze masaa hadi kumi. Na kuna mamlaka zinatakiwa zisifunge ofisi kabisa wafanye kazi masaa 24, kama TRA, UHAMIAJI ,RITA, NIDA na nyinginezo zinazo hudumia raia moja kwa moja

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Halmashauri masaa 9 kuwachosha tu mwisho wa siku majungu,wizi na umbea unatamalaki,watumishi wa halmashauri wapewe masaa ma4 tu yanatosha wakapambane na familia zao mana hata mshahara wanaolipwa unatia huruma,hao watumishi ni kama watumwa ndio wanotusumbua humu jf na mitaani.
 
Tatizo la binadamu ni kujiangalia yeye....

Ili ufahamu uzuri au ubaya wa kuwa mtumishi acha kazi uone wangapi wataitaka kazi yako !!!, Kuna kipindi ualimu, uaskari uanajeshi watu walikuwa wakipangiwa hawaendi; sasa hivi mpaka wanaonga...

Kwahio ili kuondoa mzizi wa tatizo its about time serikali iache kukaa likizo na kupiga udalali na kuja na sera ambazo zitaleta ajira zenye ujira wa kutosha kwa majority ya watu...

Sisemi watu wawe matajiri.., bali middle income iongezeke sasa hivi kuna watu wa kula na kuzaza wengine hata makombo hawana....., Extreme Poverty anywhere is a threat to to Human Security Everywhere....
Umeelewa kilichoandikwa!? Au ndio walewale!?
 
Tatizo sio masaa tatizo ni nidhamu,sisi watanzania hatuthamini kabisa tunachokifanya hasa kwenye taasisi hizi za serikali.
Magufuli alijitahidi kiasi kuileta nidhamu,now tumerudi nyumba kabisa.

Ukiipenda kazi yako utawathamini na unao wahudumia,tuzipende kazi zetu.
 
Umeelewa kilichoandikwa!? Au ndio walewale!?
Huenda wewe ndio haujaelewa ulichokiandika ngoja ni-break it down....

Achana na hayo masaa nane hata wakisema masaa 12 bado watu watafanya ili kujua kwamba mtaani pagumu acha hio kazi uone wangapi wataitafuta...; Unaongelea masaa yapunguzwe hivi hizi kazi zipo ili watu wapate pesa au wapate huduma ? Kama ni huduma hayo masaa yakipungua nani afanye hizo extras ? Watafute wengine wa kuzipa pengo la masaa mawili ?

Ndio hapo nikakupa mzizi wa fitina sio masaa wala walio kwenye ajira mtaani ni pagumu hata hao wenye security ya kazi wana nafuu (proof ya hili ni ikitokea nafasi moja ya kazi wanakwenda watu mia moja)
 
Hali ya mtumishi Tanzania kuanzia wakati kutoka awamu iliyopita mpaka Sasa ni Tete!! Serikali ya magufuli ilishindwa kuongeza mishahara Kwa kipindi cha uhai wake akiwa kama Rais wa nchi!!

Tatizo hili linajirudia tena na tena,ambapo hata ikanachoitwa annual increment ambayo ni haki ya msingi haipo tena!!!

Niishauri serikali ni muda muafaka Sasa ipunguze muda wa kufanya kazi ili watumishi wanalalama wapate muda wa kuingia mtaana na kuisaka shilingi Kwa udi na uvumba!! Badala ya masaa nane Sasa yapungue na yabaki matano tuu!!

Watumishi wengi wanashughuli mbalimbali kama udereva Noah, udereva pikpiki, mashine za kusaga,sheli bubu,saloon,kukaanga vihepe,aka chips,nk!! Niwazi kama watatia nguvu kwenye usimamizi wataongeza vipato hivyo kupunguza ukali wa maisha uliosababishwa na serikali kujishindwa!!
Kama mmechoka kazi.tokeni.

Tuongie wengine msitutishe.

Sent from my SO-01L using JamiiForums mobile app
 
Wenye akili timamu wameshajipunguzia wenyewe muda wa kazi.

Kuna mmoja mwaka 2012 aliwahi kuniambia mshahara wa serikali ni wa saa 4 tu kwa siku.
 
Tatizo sio masaa tatizo ni nidhamu,sisi watanzania hatuthamini kabisa tunachokifanya hasa kwenye taasisi hizi za serikali.
Magufuli alijitahidi kiasi kuileta nidhamu,now tumerudi nyumba kabisa.

Ukiipenda kazi yako utawathamini na unao wahudumia,tuzipende kazi zetu.
Huelewi kilichoandikwa na Sana ya fasihi
 
Huenda wewe ndio haujaelewa ulichokiandika ngoja ni-break it down....

Achana na hayo masaa nane hata wakisema masaa 12 bado watu watafanya ili kujua kwamba mtaani pagumu acha hio kazi uone wangapi wataitafuta...; Unaongelea masaa yapunguzwe hivi hizi kazi zipo ili watu wapate pesa au wapate huduma ? Kama ni huduma hayo masaa yakipungua nani afanye hizo extras ? Watafute wengine wa kuzipa pengo la masaa mawili ?

Ndio hapo nikakupa mzizi wa fitina sio masaa wala walio kwenye ajira mtaani ni pagumu hata hao wenye security ya kazi wana nafuu (proof ya hili ni ikitokea nafasi moja ya kazi wanakwenda watu mia moja)
Unakichwa kigumu Sana hakika ulimzeesha mwalimu wako
 
Masaa yangeweza punguzwa kazi zikaongezwa pia
Au nasema uongo ndugu zangu
 
We unafanya kazi sekta gani? Siku nyingi watumishi walishapunguza masaa ya kazi kivyao. Mfano, walimu, mwalimu anapiga pindi moja la asubuhi kisha anaenda shambani kwake kupiga jembe kisha anarudi kusaini muda wa kutoka kazini. Mkuu wa shule hana noma kwa kuwa naye ni doja wa vipindi, wengine wanaenda kupiga boda vichwa viwili vitatu wanarudi shuleni. Wale wakaanga chipsi na saluni nao wana staili yao ya kutoka ofisini. Wakaguzi wenyewe ni walimu hawana cha kuwafanya wakija wataambiwa wana udhuru. Huko kwenye sekta zingine mtindo ni huu huu, ukikagua daftari la mahudhuri wamejaa tele kumbe kuna makidamakida yanafanyika ili watumishi kujiongezea kipato ndani ya muda wa kazi
 
Back
Top Bottom