Serikali ipongezwe kwa hili la jambo la Bima

Hizi hospitali zilikuwa zinatupiga bei za kibwanyenye.

Kidonge cha shilingi 50 unauziwa shilingi 1000 hata zaidi, kutegemea wewe mwenyewe umekujaje.

Huo ndo ulikuwa utaratibu wa siku zote wa hizi hospitali.

Zinatia faida kwenye shida ya kiafya ya mtu!

Sasa Serikali imeshtuka na kuwashukia jumlajumla.

Sasa wamepewa bei halisi wanazostahili kuzipata.

Wanaanza kupiga mayowe.

Wanaona wamenyang'anywa tonge tamu mdomoni.

Maana walishazoea.

Tuwe nyuma ya Serikali tuitie moyo na kuipongeza Serikali kwa hatua hii.

Maana itaokoa wengi hasa huko vijijini maana hata kupata hiyo hela ya matibabu ni mtihani.
Uko serious mkuu.
 
Sidhani kama ulisoma madudu ya NHIF kwenye ripoti ya CAG, mfuko umechezewa sana, pesa zetu za michango zimetumika kuhonga mahawara, mfuko unapumulia mirija ili kuunusuru serikali inakuja na solution za kisiasa, huu ni ujinga. BTW next time unapoingia msalani jitahidi usitoke na haja kubwa kichwani then ukaja kuanzisha mada hapa. Siasa kwenye afya ya mwananchi sio jambo jema.
 
mrizike na mlichokipata kwa muda wote huo mliokamua watu mabei ya kibwanyenye kunenepesha matumbo yenu

msitake kujilimbikizia nyinyi tu

huo nao ni ufisadi mwingine tu
Jifunze kwanza kusoma na kuandika.

Ujinga una gharama kubwa sana.

Maana unajenga chuki kwa mambo yasiyokuwepo.

Ninyi ndio wale wazee ambayo wamepewa NHIF na watoto wao, halafu hawaendi nazo hospital kwasababu eti zikitumika hospital watoto wao watakatwa pesa.

Uzuzu ni mzigo mzito
 
Hospital binafsi wanatumia gharama zao kutoa huduma, kununua madawa, kodi kibao wanatoa, kulipa wafanyakazi.

Kwa mfano, wamesitisha huduma nani anapata madhara? Hii mifuko mnachota pesa za wachungiaji mpaka inakuwa empty kabisa, then mnaleta siasa za hovyo.

Kila mfumo, mnataka kupata pesa very soon mtaenda kule Utt amis, mchote pesa mkafanye kampeni, mwishoe watu wakitaka kutoa pesa zao muanze kuwazungusha.
mkuu hapo kwenye utt amis umegonga penyewe. Kwa serikali hii kuna siku watu wataamka na kilio!
 
Hakuna mtu anayefanya biashara Ili hasipate Faida. private Hospital zipo sahihi.. Kwani wanalipa Kodi kubwa wanalipa salary Kwa wafanya Kazi na gharama nyingine za uendeshaji. Mapato ya nchi hii yanawanufaisha watu wachache asa wana siasa wa kubwa tu
 
Jifunze kwanza kusoma na kuandika.

Ujinga una gharama kubwa sana.

Maana unajenga chuki kwa mambo yasiyokuwepo.

Ninyi ndio wale wazee ambayo wamepewa NHIF na watoto wao, halafu hawaendi nazo hospital kwasababu eti zikitumika hospital watoto wao watakatwa pesa.

Uzuzu ni mzigo mzito
lete hoja kiongozi
sio unapiga blaah blaah
 
Hakuna mtu anayefanya biashara Ili hasipate Faida. private Hospital zipo sahihi.. Kwani wanalipa Kodi kubwa wanalipa salary Kwa wafanya Kazi na gharama nyingine za uendeshaji. Mapato ya nchi hii yanawanufaisha watu wachache asa wana siasa wa kubwa tu
ueleweki unatetea nini mkuu

kodi wanayolipa ni halali sio halali? kwamba hawatakiwi kulipa kodi au?

mishahara? kwamba hawatakiwi kulipa au?

sawa tufanye wanalipa, nini kinachojustify waihamishie kwa wateja wao? tena wateja masikini?

crappie!!
 
Hizi hospitali zilikuwa zinatupiga bei za kibwanyenye.

Kidonge cha shilingi 50 unauziwa shilingi 1000 hata zaidi, kutegemea wewe mwenyewe umekujaje.

Huo ndo ulikuwa utaratibu wa siku zote wa hizi hospitali.

Zinatia faida kwenye shida ya kiafya ya mtu!

Sasa Serikali imeshtuka na kuwashukia jumlajumla.

Sasa wamepewa bei halisi wanazostahili kuzipata.

Wanaanza kupiga mayowe.

Wanaona wamenyang'anywa tonge tamu mdomoni.

Maana walishazoea.

Tuwe nyuma ya Serikali tuitie moyo na kuipongeza Serikali kwa hatua hii.

Maana itaokoa wengi hasa huko vijijini maana hata kupata hiyo hela ya matibabu ni mtihani.
Na kesho serikali ikikubali matakwa ya APTHA utakuja kupongeza hapa
 
Kuna wagonjwa wengi wako kwenye dialysis three times a week. Si watakufa tu!
Ndio hapo sasa na mtu anakuambia Serikali ipongezwe. Trumph alikua sahihi sana kuwa tunapaswa kutawaliwa tena. Kama wasomi wetu ndio wenye mawazo kama haya.
 
Ila tuache unafiki hospitali binafsi hasa hizi zinazojiita polyclinic na zile kubwa zinaibia sana mfuko wa bima ( NHIF) hili nimelishuhudia mwenyewe kwa macho yangu, yaani unakuta mtu anapewa maelezo kabisa jinsi ya kuchakata form sijui hata NHIF wafanye vipi kukabiliana na hili suala maana ishakuwa kama fashion sasa.
Miongoni mwa vitu wanavyokosea Serikali hususani NHIF ni huduma za ki dgitali.
Mtu unakwenda Hospitali unaambiwa saini hapa unasaini wakati huo wewe unachosaini haukioni. Anaona anaye operate mfumo (computer) unamaliza matibabu unasaini unaondoka.
Ilipaswa ukishasaini kile chote kilichojazwa kuwa ni huduma uliyopewa kije kwenye simu yako (msg) au upewe ripoti ili ujue umesaini nini.
Nje ya hapo watapigwa sana maana inabaki kiwa siri ya hospitali tu mgonjwa hajui chochote.
 
Sawa.

Hawataki tena hiyo faida kubwa waliyokuwa wanaipata kwa NHIF.

Sasa hivi ukienda na hicho kikadi chako cha NHIF hawapokei, utalipa cash.

Huu upoyoyo ndio CCM wanaufurahia.
Kwanini wasiende kwenye hospital za serikali?
Serikali ingetoa kodi na tozo kwenye hospitali za private kama kweli wanajali afya za wananchi
 
Miongoni mwa vitu wanavyokosea Serikali hususani NHIF ni huduma za ki dgitali.
Mtu unakwenda Hospitali unaambiwa saini hapa unasaini wakati huo wewe unachosaini haukioni. Anaona anaye operate mfumo (computer) unamaliza matibabu unasaini unaondoka.
Ilipaswa ukishasaini kile chote kilichojazwa kuwa ni huduma uliyopewa kije kwenye simu yako (msg) au upewe ripoti ili ujue umesaini nini.
Nje ya hapo watapigwa sana maana inabaki kiwa siri ya hospitali tu mgonjwa hajui chochote.
Mbaya zaid unasainishwa kabla hata hayo matibabu yenyewe hujayapata, ukishasaini unaingia kwa Dr pengine shida Yako inahitaji ushauri nasaha tu ukishaondoka Ile form inajazwa dawa na mavipimo wakat hukupata hizo huduma
 
Back
Top Bottom