From Sir With Love
JF-Expert Member
- Sep 13, 2010
- 2,076
- 3,797
Heri ya mwaka mpya.
Kama mzazi, nawiwa kukinzana na ulazima wa mzazi kununua uniform za shule kwenye shule ambayo mtoto amepata nafasi tena kwa bei kubwa.
Kwa wale wazazi au walezi ambao hawasomeshi watoto shule za private, mchezo upo hivi!
Mwanao ukimpeleka shule ya private na akatahiniwa na kufaulu, shule husika huwa inamlazimu mzazi anunue uniform na vikorombwezo vyake pale pale. Kwa udadisi wangu, bei za uniform kwenye shule husika huwa ni kubwa kuliko maduka ya kawaida.
Kibaya zaidi, mzazi analazimika anunue uniform kwenye shule husika kwa sababu ya MUHURI wa shule. Shule nyingi za private zina mihuri kwenye masweta, koti, kaptula, au shati za shule husika.
Kununua uniform shuleni, kunafanya wafanyabiashara wenye maduka ya nguo kutopata biashara kwa sababu ya kutokua na mihuri husika, hivyo nguo zao kukosa soko japo zinafanana na shule husika.
Ninaomba serikali yetu sikivu, ipige marufuku shule kuwauzia uniform wazazi kwa ulazima, lakini pia iweke bei elekezi za uniform ili wazazi wapate value for money, kama walivyoweka bei elekezi kwenye vitabu vya shule.
Sent using Jamii Forums mobile app