Serikali ipige marufuku matamasha ya fiesta

Serikali ipige marufuku matamasha ya fiesta

Mkuu naona hoja ya mleta mada ni sahihi...inatakiwa iundwe tume ya kijasusi ichunguze haya matamasha walete evidence ya videos na audios ya kinachofanyika humo..

Pia whatever the case,kwa walio na watoto teenagers hasa wa kike,aisee haya matamasha na media za Shigongo na Clouds hazifai kabisa....kwa wote wenye watoto,kwa uchungu uliopo wa malezi haya matamasha na hizi media ni za kufuta kabisa...

Zimeharibu akili za watoto 100%,kila mtoto anaabudu hawa watu na haya matamasha,hii ni hatari,mind control ni kubwa
UPO SAHIHI SANA

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Usitokwe jasho bure nenda Dodoma ndani uone wamama wa kiafrika na akina baba wa kiafrika wanavaaje. Wewe kama umezaliwa mjini shauri yako. Huko vijijini akina mama matiti nje, watoto midudu nje, akina baba ni kale ka nguo ka kufunika otherwise kila kitu free.
Nenda umang'ati unakutana na yale yale, umasaini, uhadsambe je. Hata wabantu wengine toa wagogo, kuna mahali wasicha wanatembea na magome ya miti kuficha sehemu nyeti. Tatizo hamtembei mnadhani maisha ni mjini tu. Wa mjini wanajitahidi kumodify maisha waliyiacha vijijini. Kama unataka uafrika nenda makumbusho kwanza ujifunze maisha ya waafrika na siyo hayo ya Dar sababu hayana mengi tembelea mikoa yote yenye makumbusho ndo urudi na story yako. Tusichanganye dini na uhalisia. Dini zililetwa utamaduni tulirithi chagua cha kuletewa au chakurithi.
Wewe ni SHETANI kweli, utamuachia mtoto wako wa kike kila siku awe anatembea kalio nje eti kisa mwanadamu hakuzaliwa na nguo? Wewe mbona hutembei KALIO NJE??? Hata huyo mtoto wako labda umtafutie shule ya peke yake msituni huko awe anaingia darasani huku KALIO likiwa limetokeza kwa nje? Wewe ni MJINGA kweli, au umekua kwenye aina ya maisha mama yako mzazi akiwa anavaa zile nguo za kulidondosha KALIO nje?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
 
Wewe ni SHETANI kweli, utamuachia mtoto wako wa kike kila siku awe anatembea kalio nje eti kisa mwanadamu hakuzaliwa na nguo? Wewe mbona hutembei KALIO NJE??? Hata huyo mtoto wako labda umtafutie shule ya peke yake msituni huko awe anaingia darasani huku KALIO likiwa limetokeza kwa nje? Wewe ni MJINGA kweli, au umekua kwenye aina ya maisha mama yako mzazi akiwa anavaa zile nguo za kulidondosha KALIO nje?

Sent from my SM-J700F using JamiiForums mobile app
Si shetani kidogo ni kichaa muulize yeye anarembea makalio nje?
 
Serikali waifute tu,fiesta ni ujinga na ufirauni ndio unaofanyika,wanahamasisha uzinzi,uasherati na ufirauni,ni uchafu wa kupitiliza unaofanyika,wafute tu,haina maana zaidi ya kuvunja maadili kwa vijana.
 
Ha ha haaa fikra pevu my .... na bado unani quote ei mie mwenye akili fupi zisizo kupita zako.

Lia ulie wivu tu umekujaa kea kuleta uzi huu, au unataka kukatiwa pesa zinazoingia sema tu, omba omba utapewa piga kelele lia

Mfwyuuuuu
Uchiuchi tyuuu[emoji37] [emoji37] [emoji37] [emoji37]
 
*SERIKALI IPIGE MARUFUKU MATAMASHA YA FIESTA NA MATAMASHA MENGINE YOTE YANAYOZIDI KUMOMONYOA MAADILI YA VIJANA WA KITANZANIA KWA KUENEZA, KUHALARISHA NA KURASIMISHA UHUNI NCHINI*

Na Emphraim Makamba

Kwa hakika Muheshimiwa angejua mambo ambayo huwa yanatokea kwenye matamasha ya Fiesta, ninaamini angeomba siku zirudi nyuma ili abadilishe maneno yake aliyoyaongea kwenye mkutano wake na waandishi wa habari ikulu.

SABABU kuu ya mimi kuandika waraka huu ni hofu kubwa inayo niandama baada ya kuona matamasha haya yameachiwa kuendelea kutamalaki nchi nzima kwa kuvuka mipaka ya majiji na sasa kuanza kuzitafuna mpaka halmashauri za miji midogo midogo ya Tanzania. Kwa hakika majiji kama Dar es salaam, Mwanza, Arusha na Mbeya, mambo ya kihuni na ya hovyo hovyo imekuwa sasa ni kama moja ya mambo muhimu katika maisha ya watu wahuni ila sasa ninapoona uhuni huu unapelekwa mpaka vijijini siwezi kuendelea kuwa mnafki na kunyamaza kimya. Ninaomba mnisaidie kupaza sauti yangu iwafikie wale wenye mamlaka waliopo kule juu.

Fiesta ni tamasha kubwa la KIHUNI nchini. Mahali popote ambapo tamasha hili linapokuwa likifanyika ni wazi kabisa mambo mbali mbali ya kihuni huwa yanakuwa yakifanyika sambamba na tamasha hilo kabla, wakati na baada ya tamasha.

NUSU UCHI ndio namna ya kuvaa mavazi kwa dada zetu na binti zetu wakati tamasha hili linapofanyika. UKAHABA na UFUSKA ndio mahala pake na hufanyika wazi wazi katika viwanja hivyo na biashara ya ukahaba na madawa ya kulevya hufanyika kupendezesha matamasha haya. Wasanii wanaoimba MATUSI MATUSI katika nyimbo zao ndio hupata nafasi kubwa ya kusherehesha matamasha haya na husafirishwa kwenda kusambaza UCHAFU huo mpaka mikoa ambayo haina hatia na uchafu wa mijini. Fiesta Rukwa, Tabora, Singida, Lindi, Manyara na mikoa midogo midogo mingi mpaka kufikia hali ya kusikitisha sana. Wasanii kama Snura wa chura, ManFongo wa hainaga ushemeji, Shilore na Kanga moko na wasanii wengine wengi wanaosifika kwa mashairi ya kihuni kihuni na kutumbwiza kwa kucheza nusu uchi ndio hupata nafasi kubwa sana ya kusafiri kwenda kusambaza huu UPUUZI katika mikoa yote midogo midogo nchini.

Mwaka 2005 baada ya Rais wa awamu ya nne ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuingia madarakani kwa mara ya kwanza kama mkuu wa nchi, nilipata nafasi ya kukutana na Chief of Staff kwa chakula cha mchana na alitaka kujua nini maoni yangu kuhusu swala la vijana hasa hasa nyanja za utamaduni na maadili. Tuliongea mengi ila nilimwambia kitu kimoja ambacho nilimuomba akichukue kama dira. Nilimwambia kwamba:

*Erick Shigongo* na *Joseph Kusaga* ni vijana wawili nchini wanaotakiwa kudhibitiwa haraka sana kupitia vyombo vyao vya habari vya Global Publishers Limited na Clouds Media Group kabla ya janga kuu la mmomonyoko wa maadili utakaoikumba taifa hili na isipatikane tiba ya haraka kwa muda mrefu. Wote tumeshuhudia namna magazeti ya udaku ya Global publishers yanavyoharibu kwa kasi jamii yetu. Wote tumeshuhudia na tunaendelea kuwa mashahidi wa namna jinsi CLOUDS MEDIA GROUP kupitia vyombo vyake vya habari vya Clouds Fm na Clouds TV vinavyojitahidi kila siku kubomoa kizazi hiki cha vijana wetu wa kitanzania kwa namna mbali mbali mpaka kufikia kuanza kuhamasisha USHOGA kwa kufanya mahojiano na shoga kupitia televisheni hiyo ambayo vijana wengi wanaiangalia na kuipenda. Juhudi na ushauri wangu uligonga mwamba baada ya kuona mkuu ndio kwanza anashikamana na hawa ambao kwangu mimi ninawaita Prime Suspects wa chanzo kikubwa cha kasi ya mmomonyoko wa maadili ya vijana wetu hapa nchini.

Wito wangu kwa serikali ni kwamba, *IT IS NOW OR NEVER* Kama tunataka kuokoa taifa hili la vijana wetu basi tuchukue hatua sasa lasivyo ifafikia mahali tutashindwa kuzuia upuuzi huu kama vile ilivyo kwa mataifa mengi ambayo ni wahanga wa upuuzi huu. Wazazi tutajitahidi kadri ya uwezo wetu kuwatunza na kuwalea vijana wetu katika maadili safi na bora ya kumcha mwenyezi Mungu lakini pia serikali nayo itusaidie kwa maswala ya kiujumla. Tusikubali UHUNI kuwa sehemu ya utamaduni wetu.

_Mungu ibariki Tanzania, Mungu bariki vijana wetu wote nchini._
Umezungumuzia mada muhimu sana kwa jami,ni mjinga tu atakayekupuuza.

Kwa haya yanayoendelea kwa taifa kupitia fiesta kama taifa tusipolia leo tutalia kesho,

Mda utaamua.
 
Huyu Joseph Nyanga inalekea haijui hii nchi pamoja na kujinasibu kwake kuwa ni mtanzania tena ana ukaribu na viongozi!
Awaachr vijana wapite na ujana wao hata enzi zao walikuwa Na majanga yao tu kwani Akina remmy na nyimbo zao za kwa soksi ziliwatia ukakasi lakini sasa ni ukweli tu kama mambo kwa soksi ndio yenyewe!
Pili serikali ipi hii ya kupiga kelele kuhusu vivazi vya vijana wakati mpaka sasa ile project ya vazi la taifa iliyo anzishwa kwa mbwembwe hatujui imeishia wapi!
Waache vijana wavae wapendeze hata mama zenu in the sixties na 70s walivaa vimini .
Na wakina baba walivaa provocative trouser so wide at the bottom and tight above in such a way muhogo wake uko outlined for all women to see!
Mzee tulia waache watu wajiburudishe!
 
Mleta mada uko sahihi kabisa, tunaua taifa kwa kujenga kizazi cha watoto wahuni wasio na maadili. Humo humo utegemee upate vijana wanaojielewa na wasomi kwa ajili ya kufikiri kuhusu maendeleo ya taifa. Ni vizuri serikali ikaangalia namna inavyoweza kulinda maadili ya vijana kwa ajili ya kizazi cha kesho
Badala ya kuhamasisha ubunifu wa vijana wenye na kuwashindanisha kuwaandalia zawadi na kuwapongeza wanaofanya vizuri .

Tumekazana kuwapelekea wacheza nusu uchi na kuhamasisha ngono kuwalazimisha kuimba imooo hata bila kujua maana yake

Ndio maana Trump.anasema tutawaliwe tena maana sijui ni lini tutajikwamua na kuwa na utamaduni wetu na kujitengenezea utaratibu wetu wa maisha kama taifa.
 
Bila shaka una chuki na
*Shigongo (Mzee wa kuikopesha ccm, na kulia lia na maandishi)
*Luge na Joseph kusaga
*Zamarad
Sasa unataka wadhibitiwe ili hawa wakale wapi? Hakuna anayelazimishwa kuhudhuria matamasha yao kama utawalea vyema wanao basi maadili yao yatabaki salama na huko fiesta hawatokanyaga kuuona ufuska, Jitahidi kuwaombea pia.
Yesu na Malia !!!! Mwizi nae akidhbitiwa unataka akale wap, ????
 
Fiesta ni tamasha la kuzimu/Free Mason/ na huwa ni ushetani,ajabu Kiongozi fulani anayesema tumuombee naye kalinariki akitaka tuende na yeye alitamani sema hana nafasi
 
Badala ya kuhamasisha ubunifu wa vijana wenye elimu tofauti tofauti na kuwashindanisha kuwaandalia zawadi na kuwapongeza wanaofanya vizuri .

Tumekazana kuwapelekea wacheza nusu uchi na kuhamasisha ngono kuwalazimisha kuimba imooo hata bila kujua maana yake

Sasa sijui hii Tanzania ya viwanda itajengwa na nani?

Ndio maana Trump.anasema tutawaliwe tena maana sijui ni lini tutajikwamua na kuwa na utamaduni wetu na kujitengenezea utaratibu wetu wa maisha kama taifa.
 
Back
Top Bottom