Serikali ipige marufuku kuuza mkaa nje ya nchi.....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,226
116,839
Ni vizuri serikali ikapiga marufuku kabisa uuzwaji wa mkaa nje ya nchi na iwe haramu kama ilivyo meno ya Tembo.

mkaa unao uzwa nje umewatajirisha wageni zaidi nilisoma gazeti la Sunday Nation walisema mkaa wa Tanzania kwa kupitia Kenya.Unakwenda Somali na ukifka Somalia unauzwa hadi Europe na Asia na kuna watu huko Somalia ni mamilionea.

Sasa mkaa huu kwa kweli unamaliza misitu yetu,,na vile vile kupandisha bei ya mkaa unaouzwa ndani.

nafikiri sasa serikali ipige marufuku uuzwaji wa mkaa kwenda nje ya nchi na mkaa unaokwenda Zanzibar utazamwe usiwe ndo upenyo wa mkaa kwenda Asia.

Hili ni muhimu kwa kulinda mazingira yetu mvua,umeme,na misitu na mazingira kwa ujumla.
 
Hadi mkaa ulikuwa unauzwa njee ya nchi??

Ngoja ninyamazee mana nitaambiwa mimi ni Ukawa!!
 
Ni vizuri serikali ikapiga marufuku kabisa uuzwaji wa mkaa nje ya nchi na iwe haramu kama ilivyo meno ya Tembo.

mkaa unao uzwa nje umewatajirisha wageni zaidi nilisoma gazeti la Sunday Nation walisema mkaa wa Tanzania kwa kupitia Kenya.Unakwenda Somali na ukifka Somalia unauzwa hadi Europe na Asia na kuna watu huko Somalia ni mamilionea.

Sasa mkaa huu kwa kweli unamaliza misitu yetu,,na vile vile kupandisha bei ya mkaa unaouzwa ndani.

nafikiri sasa serikali ipige marufuku uuzwaji wa mkaa kwenda nje ya nchi na mkaa unaokwenda Zanzibar utazamwe usiwe ndo upenyo wa mkaa kwenda Asia.

Hili ni muhimu kwa kulinda mazingira yetu mvua,umeme,na misitu na mazingira kwa ujumla.

Hilo gazeti linaweza kuwa limeficha kuogopa mambo ya kisiasa. kuna wasi pia kwamba mkaa mwingi unaingizwa Zbar na baadaye unapelekwa oman, komoro na visiwa vingine vya bahari ya hindi. tatizo ni zbar, wakiguswa tu wanakimbilia kusema wanaonewa.

Hata hivyo kila kitu kilikuwa kinafanyika nchi hii bora ujuane na jamaa, anayejuana na mtu fulani, anayejuana na waziri au kimada fulani naye anajuana na waziri fulani au mtoto wa waziri au rais.
 
mkaa mpaka ufike Oman au nchi nyingine si utakuwa na gharama kubwa.

kama wanautumia kwa matumizi haya haya ya kupikia si bora watumie gesi au umeme.
 
Mkuu The Boss taarifa yako imewafikia wahusika, natumai serikali hii ya mhe. Dr. J.P.Magufuri ni sikivu, hivyo itaifanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kupunguza kama sio kuzuia kabisa uharibifu wa mazingira.
 
Last edited by a moderator:
Hilo gazeti linaweza kuwa limeficha kuogopa mambo ya kisiasa. kuna wasi pia kwamba mkaa mwingi unaingizwa Zbar na baadaye unapelekwa oman, komoro na visiwa vingine vya bahari ya hindi. tatizo ni zbar, wakiguswa tu wanakimbilia kusema wanaonewa.

Hata hivyo kila kitu kilikuwa kinafanyika nchi hii bora ujuane na jamaa, anayejuana na mtu fulani, anayejuana na waziri au kimada fulani naye anajuana na waziri fulani au mtoto wa waziri au rais.

Zanzibar unaishia Comomoro
unaofika Oman unapitia Arusha hadi Kenya hadi Somalia....

Arusha ndio getaway ya mbao zetu...mkaa na nguzo zinazoenda Kenya
 
Duuhh!!! Hii ni hatari sana ndo maana joto limepanda sana,mvua hakuna kumbe misitu inazidi kumalizwa,mkaa wenyewe ndani unauzwa bei sana kwa watanzania kumbe wanaofaidi ni wengine,ni wakati sasa serikali kulisimamisha hili.
 
Hatari kupita maelezo
mvua hakuna na mabwawa ya umeme hayajai pia
so mara mgao wa umeme mara umeme wa gesi....wakati kumbe tatizo liko deep hivi
tunakata mno miti kutengeneza mkaa tunaouza hadi Europe...asilimia 80 ya mkaa wa Kenya unatoka kwetu
na Kenya ndie biggest exporter wa mkaa
 
Haswaaa hili janga la umeme na maji bila kuhifadhi vizuri mazingira tutaendelea kuteseka sana, tiba ni kutunza mazingira vizuri waswahili wanasema kitunze kigumu kikutunze.....

Na hawa Kenya duh !!..kama ameamua kutumbua majipu aliangalie na hili.....
 
Majipu yako mengi yakutumbua hadi Dr.atanuka usaha hili nalo jipu pia Makaa ya mawe pia tusije tukaagiza nje tena.
 
Ok ni makaa ya mawe mkuu ma truck yaliyosajiliwa kenya mengi yanapitia dodoma via mtera to iringa ile nadhani yanatoka songea nakumbuka nilipopita iyo barabara wiki iliypita nilikutana nayo mengi sana..
 
Ile mikakati ya kulinda mazingira iliyosomwa na VP mwanzoni mwa awamu ya nne iliendeleaje?

Achana na VP, rais mwenyewe wa ile awamu aliwahi kutangaza maamuzi magumu kama alivyoyaita. Akaishia kupiga marufuku mifuko ya plastiki kwa miezi 2 tu! Baadaye shoga zake wakaendelea na uchafu wao.

Hatukuwa na rais kwa miaka 10.
 
Mpaka Uingereza wananunua mkaa wa TZ...

Sijui umegunduaje kwamba ni mkaa wa TZ. Biashara ya kuuza mkaa kwa afrika inafanywa na Nigeria na Sudan. Wao wanauza nje kwa ruhusa kanisa ya serikali zao. Somalia ni biasahara yao haramu inayofanywa na Al shabaab. Hapa kwetu pia sehemu ya mkaa unapelekwa Rwanda ambao kwao hairuhusiwi kukata mti na wakati huo huo wanajidai wanatimiza mahitaji yao yote ya mkaa kwa kutumia miti ya kupandwa.
 
Back
Top Bottom