Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,811
Hawa watu jamii ya Wahdazabe na Wasandawe, Serikali iingilie na ipige marufuku kuishi kama wanavyoishi na badala yake wapelekewe Shule, wafundishwe Kiswahili na kuchanganywa na sisi, tuache kuwatumia ndugu zetu kama experiments, najua hapa mtakuja kutoa povu sijui Utamaduni blah blah wakati hapo ulipo umekaa kwenye computer au smart phone, umevaa Jeans na sneakers ukifika nyumbani unakula unawasha jiko la umeme au gesi kupika chakula na kula kijiko, lkn unataka wenzako ndiyo waendeleza huo unaouita Utamaduni, kwa faidia ya nani?
Hawa watu pmj na Wamasai bila ya kujua wanatumiwa na Wazungu kwa ajili ya experiments, (human experiments), Wazungu wakitaka kulinganisha tabia za Binadamu wa kale/ujima na wa sasa huenda kwa hawa watu, hivyo ndiyo maana ukitaka kuwapa nguo au kuwafundiosha Kiswahili na kuwachanganya na sisi Mzungu anakuja juu, kama sisi wote tulikuwa hivyo lkn leo hii hatuko hivyo kwa nini tunafikiri wenzetu ndiyo wanaopaswa kudumisha Utamaduni wao?
(Picha kwa hisani ya blogu ya Michuzi!)