Serikali ingeruhusu/Ingerahisisha sekta binafsi kuwekeza kwenye microhydropower dams na kuuza umeme locally

Red Giant

JF-Expert Member
Mar 9, 2012
15,658
20,890
Tanzania ina potential kubwa sana ya uzalishaji mdogo wa umeme wa maji. Hizi ni zile zinazoweza zalisha 5KW hadi 10MW.

Utafiti uliofanyika unaonyesha mikoa kama Ruvuma, Rukwa, Njombe, Mbeya, Songwe, Kagera na zingine kwa kiasi zina potential kubwa sana za micro hydro dam, ni kama inafika 500MW. Hii ni zaidi ya upungufu tuliotangaziwa.

Na hili litasaidia sana kwenye hili suala la REA, vijiji vinaweza tumia umeme unaozalishwa locally.

Uwekwe utaratibu mzuri ili watu waweze kuwekeza kwenye uzalishaji mdogo wa umeme wa maji na kuuza kwa urahisi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…