Serikali inavyowakomoa walimu

Serikali inavyowakomoa walimu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,769
Reaction score
288,283
Baada ya kuelezea 'scenario' ya jana rafiki yangu mmoja amenitafuta. Ni rafiki yangu wa muda mrefu, lakini sikuwahi kujua sana kuhusu upande wa pili wa maisha yake.

Yeye ni firstborn kwenye familia. Baba yake alifariki akiwa kidato cha 3, hivyo alipomaliza kidato cha 4 aliamua kusomea ualimu (grade III) ili asaidie wadogo zake. Pamoja na kufaulu vizuri lakini kwenda form five angeshindwa kulea wadogo zake.

Akasomea ualimu na kuhitimu. Akapangiwa shule ya kufundisha mkoani Arusha. Akaweza kujikimu na kusaidia wadogo zake kusoma. Baadae akaamua kujiendeleza kidato cha 5&6 kama Private Candidate. Akafanya mtihani na kupata division 2 ya points 10. Yani alama moja tu apatae division 1.

Akapata udahili chuo kikuu. Akaomba ruhusa kwa mwajiri wake akapewa. Akasoma shahada ya kwanza ya ualimu. Enzi hizo walimu wa shahada hawakua wengi kama sasa. Lakini aliporudi kwa mwajiri (DED) hakumpandisha daraja wala kumuongezea mshahara. Akaendelea kufundisha shule ya msingi na degree yake, kwa mshahara uleule wa mwalimu wa certificate.

Hakuvunjika moyo. Baada ya muda akajiunga tena chuo kikuu kusoma shahada ya uzamili ya usimamizi wa elimu (Master of Education - Planing &Administration). Akahitimu kwa ufaulu mzuri. Akarudi kwa mwajiri lakini hakumuongezea mshahara wala kumbadilisha daraja.

Wakati huo mambo ya uhakiki yalikua yakiendelea. Uhakiki ukamalizika lakini hakupandishwa daraja wala kuongezewa mshahara. Akaendelea kufundisha shule ya msingi kwa mshahara uleule wa "certificate" bila kujali elimu yake ya "masters degree"

Baadae akapata ufadhili chuo kimoja nje nchi, kusoma Stashahada ya uzamili ya Elimu maalumu (Postgraduate Diploma in Special Education). Akapewa ruhusa ya kwenda kusoma. Akahitimu na kurudi kwa mwajiri wake. Akarudishwa kulekule shule ya msingi, bila kubadilishwa daraja wala kuongezewa mshahara.

Kwahiyo nchi hii ina mwalimu wa shule ya msingi mwenye Certificate ya Ualimu, Bachelor Degree ya Ualimu, PGD ya elimu maalumu na Masters Degree ya usimamizi wa Elimu. Lakini serikali imeamua kumtumia kuimba "mabata madogo madogo" na watoto wa darasa la 3B. Just imagine.!

Halafu akipata kazi nje ya nchi mnasema si mzalendo. Au akipata kazi sekta binafsi akaondoka serikalini mnasema amekimbia sababu ya maslahi, mnaagiza akamatwe na huko alikoenda hiyo taasisi ifungiwe. Hivi serikali ikoje? Yani nyie mmeshindwa kumtumia na hamtaki wengine wamtumie. Roho ya kichawi hii.!

Mtu kama huyu alitakiwa awe mahali ambapo ataweza kutumia elimu, uzoefu na vipawa vyake kwa manufaa ya taifa, sio kufundisha MAGAZIJUTO darasa la 3B. Lakini amehangaika sana kupandishwa daraja bila mafanikio. Mbaya zaidi analipwa mshahara uleule kama mwalimu mwenye certificate.

Kinachoumiza zaidi ni analipwa mshahara wa cerificate halafu HESLB wanamkata 18% ya mshahara huo kufidia mkopo waliompa wakati akisoma Degree, wakati degree yenyewe haijamsaidia. Mlipeni basi mshahara wa degree ili mkimkata mkopo kuwe na logic. Sio mnamlipa mshahara wa certificate halafu manamkata mkoko wa degree. Ilogical.!

Naomba Mhe.Silinde Ernest David ulione hili na kulifanyia kazi ukiwa kama Naibu Waziri mwenye dhamana. Hali hii inavunja sana moyo watumishi. Mchukueni kijana huyu mtafutie mahali panapomfaa kulingana na elimu na uzoefu wake.

Kama mlikua hamtaki kutumia elimu yake kwanini mlikua mnampa ruhusa ya kwenda kusoma? Mmempa na mkopo ambao anateseka kuulipa lakini elimu aliyochukulia mkopo hamtaki kuitumia. Jamaa yuko very frustruted, kwa sababu ana familia inamtegemea na kipato hakitoshelezi. Tumuombee asije kufanya maamuzi magumu kama yule wa Pugu.

Mwalimu mwenye uzoefu wa miaka zaidi ya 15, msomi Cert, BA, MA, PGD mmeshindwa kabisa kumtumia kwa tija? Mpelekeni basi hata vyuo vya kati akafundishe, na mumlipe kwa hadhi ya elimu yake. Kumuacha shule ya msingi ni matumizi mabaya ya rasilimali, na kuendelea kumlipa mshahara wa Certificate ni UONEVU usiovumilika. Si ajabu amewazidi hata "maboss" zake elimu na uzoefu.

Tafadhali lifanyie kazi hili litakupa heshima wewe na serikali yenu. Weka alama kwenye maisha ya huyu Mwalimu. Wasiliana nami kwa maelezo zaidi. Namba yangu ni ileile, naamini ulipohama 'chama' hukuifuta.!

Malisa GJ
 
Binafsi nimeumia sana kwasababu ya kutopanda daraja kutokana na elimu yake lakini kuhusu nafasi yake katika kazi sijaona ubaya.

Labda nikupe mfano “ Nina mdogo wangu yupo ujerumani alipata chance kipindi cha Corona kutibu wagonjwa katika nchi ya ujerumani, yeye kajiongeze na kuendelea kujiendeleza kimasomo. Nikiwa nawasiliana nae ananiambia walimu wa awali katika nchi ya hiyo ni watu wenye elimu kubwa tu na tofauti na hapa Tanzania “

Binafsi natamani walimu wa awali wawe na elimu ya juu ili kuwapa knowledge kubwa vijana wetu.
 
Malisa acha uongo haiwezekani mwalimu ana miaka zaidi ya miaka kumi na tano akalipwa mshahara ule ule alioajiliwa nao

Watu ambao wanalipwa mishahara ilel ile kwa walimu ni kundi la ajira mwaka 2014 chini ya hapo hakuna hiyo moja

Pili serialini hakuna mshahara wa masters kuna mshahara wa degree hizo masters ni weredi upatapa maslahi yake endapo utapata position yenye posho ya ukuu wa hicho kitengo mfano masters yake nk inauwezo wakumpa nafasi ya uafisa elimu,

USHAURI
Kama ana phd na bado yupo darasani mwambie andike barua kwa katibu mkuu wizara ya elimu akijielezea wasifu wake na aombe nafasi anayoona anastahili kwa kusema anatuma maombi yake ikiwa nafasi itatokea basi yeye yupo

DOUBT
Uyo mwalimu achunguzwe atakuwa ana sifa ya elimu ila sifa ya kimaadili kama mtumishi wa umma anayestahili kupewa promition hana yani watu wa veting wakimpitia wanaona kasoro

ndio maana anasoma akimini kusoma kutamsaidia hawazi madili ya utumishi wa umma je anafaa

Kwa sababu kita halmashauri kila mwaka huwa zinachukua tarifa za watumishi kuhusu elimu nk tarifa hizo hzikai halmashauri tu zinaenda mpaka utumishi kwaiyo kwa elimu yake na mda aliokaa kazini lazima wangemuona wangeuliza uyu mtu tunamuitaji so mwambieni ajichunguze atakuwa na tatizo tusishie kulaaumu tu
 
Binafsi nimeumia sana kwasababu ya kutopanda daraja kutokana na elimu yake lakini kuhusu nafasi yake katika kazi sijaona ubaya....
Huko Ujerumani kuna maslahi .na walimu wanathaminiwa sio kama hapa.

Ndio maana akifundisha chekechea huko na kulipwa vizuri hana muda wa kuhangaika kutafuta maslahi.
 
Huko Ujerumani kuna maslahi .na walimu wanathaminiwa sio kama hapa.
Ndio maana akifundisha chekechea huko na kulipwa vizuri hana muda wa kuhangaika kutafuta maslahi.

Ndio nilitaka mhusika ajikite huko sio kusema nina elimu kubwa!
 
Malisa acha uongo haiwezekani mwalimu ana miaka zaidi ya miaka kumi na tano akalipwa mshahara ule ule alioajiliwa nao...
Kwasasa Nchi ina Changamoto ya upungufu wa Madarasa, upatikanaji wa maji upungufu wa Matundu ya vyoo na Changamoto hii ni yamiaka ming sanaa miaka60 ya Uhuru bado tunaongelea hizo changamoto Halafu Anatokea Mjinga Mmoja Anasema eti Rais aongezewe muda hata kama hatak Alazimishwe!
 
Hata maandamano ya nguvu, yasiyoisha

Nilikuwa nasema mambo haya kila siku lakini nikaona raia bado hawataki mabadiliko nimeamua kujikita zangu mtwara natekeleza taratibu, nasubiri watu wabadilike nitakuwa nao.
 
Binafsi nimeumia sana kwasababu ya kutopanda daraja kutokana na elimu yake lakini kuhusu nafasi yake katika kazi sijaona ubaya...
😬😬😬 Ujerumani wapo mbali sana kulinganisha na sisi. Wapi umewahi kusikia Hao walimu wa ujerumani wanalalamika kuhusu Maslahi yanayoendana na elimu yao au wapi ulisikia viongozi wakiwalalamikia hao walimu kuwa sio wazalendo kwa sababu ya maslahi atakayo mwalimu?

Kujiendeleza kielimu its like investment, Kuna faida na hasara zake. Lakini kwa hii case huyu mwalimu kapata hasara kwa sababu kajiendeleza wasting a lot of money and time alafu haongezewi mshahara.

Inakatisha tamaa! Kama wanafanya hivi, ni nani atakaethubutu kwenda kujiendeleza?
 
Ujerumani wapo mbali sana kulinganisha na sisi. Wapi umewahi kusikia Hao walimu wa ujerumani wanalalamika kuhusu Maslahi yanayoendana na elimu yao au wapi ulisikia viongozi wakiwalalamikia hao walimu kuwa sio wazalendo kwa sababu ya maslahi atakayo mwalimu?....

Baraka! Nimekuwa nikisema maslahi ya sekta ya elimu kuna hali mbaya kila siku lakini mimi nilikosoa mhusika kulalamika katika nafasi ya kazi yake kwa kusema yeye ana elimu kubwa.

So kuwa na elimu kubwa ni kutaka maslahi hiyo ni sawa lakini sio kusema nafasi aliyokuwa nayo.
 
Baraka! Nimekuwa nikisema maslahi ya sekta ya elimu kuna hali mbaya kila siku lakini mimi nilikosoa mhusika kulalamika katika nafasi ya kazi yake kwa kusema yeye ana elimu kubwa.

So kuwa na elimu kubwa ni kutaka maslahi hiyo ni sawa lakini sio kusema nafasi aliyokuwa nayo
Its ok lakini put yourself in position ya huyu mwalimu, Je, kwa elimu yake anastahili mshahara wa mwalimu wa grade III? Je, anastahili kufundisha primary?

Bora wangempandisha daraja kwa matumaini kwamba mshahara utapanda lakini hakuna hata kimoja walichomfanyia.
 
Its ok lakini put yourself in position ya huyu mwalimu, Je, kwa elimu yake anastahili mshahara wa mwalimu wa grade III? Je, anastahili kufundisha primary?

Bora wangempandisha daraja kwa matumaini kwamba mshahara utapanda lakini hakuna hata kimoja walichomfanyia
Kama ni kweli huyu mwalimu amepunjwa kwa Sheria za utumishi wa umma, alipaswa kufanyiwa kitu kiitwacho recategorization, ni haki yake.
 
Back
Top Bottom