Serikali inapokopa ili kulipa madeni, ni maendeleo?

Criterion

JF-Expert Member
Jan 8, 2008
11,798
11,881
Nimetekewa kidogo, na nimetindikiwa na amani kwa sehemu, lakini nimepata msukumo wa kulileta hili suala hapa kwa uchambuzi zaidi. Nitaweka mada yangu katika maswali ili katika kuyajibu, tupate muafaka wa kitaalam juu ya azimio la kukopa ili kulipa mikopo. Kama wewe si mtaalam, au hujui, au huna hakika, usiharibu mjadala badala yake kaa kimya soma mchezo upate maarifa.

Chanzo cha mada ni Rais aliposema hadharani kukoshwa na ushauri wa waziri wa fedha wa kukopa ili kulipa madeni, na akaenda mbele zaidi kwamba ataendelea kukopa mikopo nafuu ili alipe madeni yanayoiva.

1. Mikopo inayolipwa leo, ilikopwa kwa ajili ya kitu gani ambacho hakiwezi kuzalisha, wala kuwekewa mipango ya ulipwaji wake mapema, hadi kufika muda wa kulipwa bila mkakati na kuingia kwenye kulipwa kwa mkopo mwingine as if serikali hainaga long term plans za maturing financial obligations? Kama mikopo ilikopwa kwa mipango, iweje malipo yake yaonekane kama ni kitu cha dharura?

2. Kunaweza kuwa na mtazamo kwamba madeni haya mama kayakuta kwa hiyo hayamhusu analipa tu kwa fadhila. Ni kweli hii? Ina maana serikali huwa haina monitoring and evaluation plans, na ni vitu gani ambavyo huwa wanakabidhiana wanapobadilishana ofisi? Ina maana kila mtendaji akiondoka ofisini anaondoka na mipango na kazi zake? Au kazi za serikali hazinaga tracking systems?

3. Mama alisema kwa kumaanisha kwamba "Kama majumbani tunakopa ili kulipa madeni ya awali, tunaanza tena kulipa madeni mapya, kwani kuna ubaya gani Serikali tukafanya hivyo", hivi hii ni best practice? Kwa sasa serikali badala ya kuset mifano bora ya kuigwa, inaanza kuiga worst practices? Au ndiyo sababu hata ufanisi wa kazi na uwajibikaji inazidiwa na private sector? Nani ni role model wa mwingine? Wakopaji wasio na utaalam ni role model wa serikali au serikali inapashwa kuwa role model kwa Wananchi wake?

4. Mama anajua kwamba mikopo ni taaluma na siyo siasa? Anajua kwamba ukopaji wa kukopa ili kulipa madeni umedhoofisha Watanzania maskini kiasi wengine wameishia kufilisiwa na wakopeshaji wao? Anajua kwamba taasisi nyingi zimeingia katika matatizo kwa sababu ya trend ya kukopa ili kulipa madeni? Anajua kwamba wakopeshaji wako makini sana kuangalia matumizi ya mikopo inayoombwa kwa sababu wanajua matumizi yasiyosahihi hupelekea kumpoteza mteja na fedha zao?

5. Mama anajua moja ya matatizo yaliyopelekea kuyumba kwa shirika lililokuwa likiwakopesha wanawake mikopo nafuu la PRIDE Africa ilikuwa ni kukopa mikopo kusiko tija? Anajua kwamba juzi waziri Nchemba ametangaza kulifilisi shirika hilo, kwa kuogopa kulipa madeni, bila bila kujali athari za maamuzi hayo kwa wadau ama kutafuta namna ya kulisimamisha tena. (Naomba ku declare interest katika PRIDE Africa. Familia yangu watu wengi ni wakopaji kule, na mimi nimekuwa nikifuaatilia kwa karibu katika kutafuta haki na huduma kwa watu wa familia yangu, hivyo kwa sehemu, ninaelewa mambo kadha wa kadha). Kama Serikali inaua mashirika yake bila juhudi za kuyakomboa kwa ajili ya madeni yaliyokopwa bilautaalam, na serikali sasa ina declare kufuata nyayo za practices zile ambazo mimi naziita ni worst practises, kwa nini Watanzania wasiamini kwamba kuna siku watapigwa minada?

6. Kama Waziri anakosa utulivu wa kitaalam, na mkuu wa serikali ananunua kila ushauri akidhani ni ushauri sahihi kutoka kwa Waziri huyo ambaye, anaonekana kama laghai kwa kuwafanya Watanzania wapumbavu na kuwaambia "Hawatalipa madeni bali serikali italipa", bila kujali kwamba Watanzania wanaelewa serikali hulipa madeni kwa ktumia fedha zao. Hapa hakuna tatizo kweli? Nani washauri wa Sesrikali katika masuala ya uchumi? Wizara ya fedha walio wezi, laghai na wasiojli mateso ya Watz? Ni nini hii lakini?

Nini hatma ya kukopa huku kunakopigiliwa misumari kwamba tutakopa tu ili tulipe madeni mengine kwa mustakabari wa taifa letu, naomba tujadili.

Inaleta kizunguzungu.
 
  • Thanks
Reactions: Auz
Back
Top Bottom