IKIRIRI
JF-Expert Member
- Jan 14, 2018
- 2,734
- 3,017
Kiongozi wa dini ni mtu muhimu sana katika kuleta amani ya nchi. Nimesoma kupitia mitandao ambapo taarifa inasema:
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili na Kilutheri (KKKT), Askofu Fredrick Shoo amesema mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa usipotendeka kwa haki unaweza kusababisha fujo.
Kauli ya Shoo imekuja wakati serikali ikitangaza kuendelea na mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa huku wapinzani wakitangaza kujiondoa kwa kile wanachodai kutotendewa haki.
Askofu Shoo ambaye pia ni Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini amesema kuwa msimamizi mkuu wa uchaguzi huo anayo dhamana ya kuhakikisha uwepo wa ushindani sawa.
“Msimamizi mkuu wa uchaguzi anayo dhamana kubwa ya kuhakikisha kunakuwa na `fair play’ (usawa) kwa vyama vyote bila upendeleo.”
“Zoezi hili lisipofanyika kwa haki linaweza kusababisha fujo na uvunjifu wa amani. Wito wangu kwake na wasimamizi wengine wote wasimamie haki,” alisema Askofu Shoo.
Sasa kauli kama hizi ni za kichochezi sana mbona masheikh wametulia.
Askofu siasa zinamuhusu nini?
Tukifanya hayo sisi wa Allah utasikia kelele nyingi.