'Serikali inaiua ATCL', balozi Nyang'anyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Serikali inaiua ATCL', balozi Nyang'anyi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Apr 11, 2010.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 11, 2010
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,759
  Likes Received: 82,905
  Trophy Points: 280
  Date::4/10/2010'Serikali inaiua ATCL', balozi Nyang'anyiBoniface Meena
  Mwananchi  MWENYEKITI wa bodi ya Shirika la Ndege (ATCL), Balozi Mustafa Nyang'anyi amesema serikali ndiyo inayoliua shirika hilo.

  Balozi Nyang’anyi, ambaye juzi alikuwa katika ofisi ndogo za bunge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kuwasilisha ripoti ya shirika hilo kwa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, alisema kuwa bajeti ndogo wanayopewa imekuwa ni tatizo kubwa.


  Nyang'anyi aliwahi kukaririwa akisema kuwa itakuwa ni ndoto kwa ATCL kurudi kwenye shughuli zake za kawaida kama haitapewa Sh7.1 bilioni kwa ajili ya kulifufua shirika hilo ambalo mwaka jana lilipookonywa leseni ya kuruka angani.


  Nyang'anyi alisema wanatarajia kupewa Sh1 bilioni, fedha ambazo haziwezi kulinyanyua shirika hilo zaidi ya kulididimiza.

  Tatizo ni serikali ndiyo inayoua shirika... tunaomba fedha za kuweza kujikimu, wanatupa kidogo sasa shirika litaendeleaje?" alihoji Nyang'anyi.


  Alisema kuwa serikali iko tayari kupigia kifua shirika la ndege (jina tunalihifadhi) ili lipate fedha benki kwa ajili ya kununua ndege nyingine, lakini haifanyi hivyo kwa ATCL.


  “Nasema hivyo kwa kuwa shirika hilo linamilikiwa na watu ambao baadhi yao wako serikalini hivyo ni bora waiue ATCL ili wao waendelee kupata faida,” alisema.


  Alisema ATCL inasuasua na chanzo kikubwa ni serikali kutokana na kutokuwa makini katika kulinyanyua shirika.


  Wakati akiwasilisha ripoti yake kwenye kamati hiyo juzi, wabunge walishutshwa na deni la Sh39 bilioni pamoja na gharama ambazo ATCL inalilipa shirika la ndege la Air Bus.


  Deni hilo pamoja na gharama hizo linatokana na ndege ya ATCL iliyopata hitilafu ya bawa wakati ikitua mkoani Mwanza hivi karibuni.

  Kutokana na hali hiyo, kamati hiyo imeitaka bodi ya ATCL kuwasilisha vilelezo vya mikataba iliyongia na Airbus wakati wa vikao vya Bunge mwezi ujao.

  “Ni kweli ATCL inadaiwa Sh39 bilioni pamoja na kulipa gharama za ile ndege iliyopata itilafu Mwanza kwa kampuni ya ndege ya shirika la Airbus.

  Kutokana na hilo kamati imeiagiza bodi ya ATCL kuleta vielelezo vya mikataba iliyongia na shirika hilo katika Bunge la linaloanza Aprili mwaka huu, alisema mwenyekiti wa kamati hiyo, Mohamedi Misanga.


  Misanga alisema kamati yake itatangaza uamuzi wake kuhusu hali hiyo bungeni, mara baada kupitia vielelezo hivyo pamoja na kupata maelezo ya kina.

  Awali kamati hiyo ilikutana kwanza na wawikilishi wa wafanyakazi na kupokea mapendekezo yao.


  Baadaye ilikutana na bodi kwa ajili ya ufafanuzi wa mambo mbalimbali ya msingi.

  Baadhi ya wabunge waliozungumza na gazeti hili, wameapa kuibana ATCL hadi itoe taarifa za msingi kuhusu matatizo ya kimejimenti, tangu shirika hilo lilirejeshwe mikononi mwa wazalendo baada ya kuvunjwa mkataba na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA).
  "Tuliwabana hadi wamevunja mkataba na SAA, tumewapa wazalendo wenzetu mambo bado hayaendi kabisa, mara unasikia ndege iliyonunuliwa bawa moja lina hitilafu," alisema mbunge mmoja ambaye hakutaka jina lake litajwa.
   
 2. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #2
  Apr 11, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Gazeti la Nipashe la tarehe 10/04 limeandika kuwa waziri Shukuru Kawambwa ambae ndio waziri mwenye dhamana ya kuiangalia ATCL amekili mbele ya kamati ya bunge kuwa halisaidii shirika la ndege kupata mtaji toka serikalini kwasababu hana imani na BODI pamoja na MENEJIMENTI yake!! Hili ni jambo la kushangaza sana kuwa waziri mzima anaweza kukili kuwa yeye anahusika na kuliua shirika ambalo Rais aliyemteua aliwaahidi watanzania kuwa serikali ingejiliimalisha; kama tatizo la shirika ni utendaji mbovu wa menejimenti na bodi kwanini waziri huyu asiivunje bodi na kubadilisha menejimenti badala ya kuliacha shirika likidolola? Waziri huyu ameonyesha dhahili kuwa hamsaidii Kikwete katika kuleta maendeleo ya nchi hii na kusema kweli huyu waziri ni mzigo kwani mashirika yote anayoyaongoza hayana ufanisi hata kidogo, Miundombinu ni wizara nyeti inayohitaji waziri makini na sio mtu mbabaishaji!!
   
 3. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #3
  Apr 11, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  tutaendelea lini sasa? uimara wa ATC ungesaidia na sector nyingine hususani utalii, cgamsingi ni vema ATC mgefanya kazi badala ya kutafuta visingizio, achane kufanya kazi kwa mazoea,
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Apr 11, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,328
  Likes Received: 1,794
  Trophy Points: 280
  Hata mimi nina shaka sana na huyu mwenyekiti wa bodi. Hivi huyu si ndio aliyewahi kununua kivuko cha kigamboni miaka ile ya tisini ambacho hata sijui kilikwenda wapi maana ilionekana kama walinunua scrapers? Kama ndiye yeye kwanini aaminiwe sasa kwamba ni different person? Yale yaliyotokea wakati ule wa sakata la mahujaji la kuingilia kazi za moja kwa moja za ATCL lilikuwa ni ishara tosha ya kuwa something was wrong!
   
 5. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #5
  Apr 11, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Heri nyumba ibomolewe tugawane mbao.

  Mashuzi matupu!
   
 6. M

  Magezi JF-Expert Member

  #6
  Apr 11, 2010
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Akina mramba na wenzake walivyo ingia mkataba na SAA ilikuwa ni njia ya kuchota pesa na kuziingiza Precision air na sasa hawataki kabisa kuona ATCL inaendelea kwani itawazibia. Waziri kawambwa naye anaogopa kufanya maamuzi ya kuiwezesha ATCL kwa sababu awamu ijayo anahofiwa anaweza asipewe uwaziri kwa hiyo ni mashuzi tu kama jamaa alivyo sema hapo juu.
   
 7. Prodigal Son

  Prodigal Son JF-Expert Member

  #7
  Apr 11, 2010
  Joined: Dec 9, 2009
  Messages: 963
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 45
  ndugu Magezi
  HAPO UMEKOSEA KABISA

  SA na KQ wote walikuwa wanataka kununua ATC, KQ walishindwa na SA ndo wakakimbilia kununua stake ndani ya PW, Ikumbukwe SHIRIMA wa PW alitangaza kabisa kwenye vyombo vya habari nia ya kuuza hisa kwenye shirika lake,Interest kubwa ya KQ haikuwa PW ilikuwa ni ATC baada ya kushindwa ndo wakakimbilia kununua hisa PW, mramba katika hilo hakuhusika kabisa

  Kumbuka SA walikuwa na nia ya dhati kabisa kugeuza DSM kama Hub yao, kwa bahati mbaya hilo halikufikiwa kulitokea msuguano wa Management ndani ya SA yule CEO aliyekuwa na nia ya dhati kuifufua ATC akaachia ngazi aliyechukuwa nafasi yake hakuwa na interst kabisa na ATC ndo mwanzo wa kifo cha ATCL ulianza,,,Tuwe realistic kidogo katika kujadili swala hili tusiwe walalamishi saana kitakachotuokoa tuwe tunatekeleza tunayoyanena

  Nini cha kujifunza kwa KAKA ZETU Wakenya KQ ilipokuwa na khali mbaya walitafuta wabia wa uhakika KLM na air france hawakuwapa share zote waliwapa kidogo tu nyingine wakabakiza kwa gvnt na nyingine wakawauzia watu binafsi na taasisi, mchanganyiko huu ndo ulilolipa KQ uhai mpya

  Ufanisi wa PW nikutokana na uongozi dhabiti wa KQ japo maamuzi karibia yote yanatolewa Nairobi bora kila kukicha wananunua ndege mpya, wanaongeza njia mpya na la msingi usalama ATCL wao badala ya kuamka na kufanya kazi kwa akili maarifa wanaishia kulalamika, ndio pamoja na matatizo mliyonayo je nini mnachokifanya?????
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Apr 12, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  Bold ya pili....
  Kama kweli waziri alisema kitu kama hiki... kinachomzuia yeye/serikali isiivunje Bodi NI NINI?
   
 9. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,495
  Likes Received: 5,725
  Trophy Points: 280
  Huyu tapeli tu hana jipya kwanza asubiri sala za waislamu aliokul hela zake na mwenzie mattaka
  kuishia kulala airport,,ameshindwqa kujieleza alipata wapi namba za staff wa atc na kumegewa mkopo wa gari wakati yeye ni bodi cheaman
  hana jipya wameiiua atcl na mwenzie mataka david ona sasa wanaelekea kuomba ubunge hawa si wauwaji kabisa

  mattaka kugombea songea ubunge ,..nyanganyi anaenda singida uko kama si laana nini??
   
 10. w

  wa hapahapa JF-Expert Member

  #10
  Nov 19, 2015
  Joined: Aug 22, 2012
  Messages: 5,552
  Likes Received: 1,604
  Trophy Points: 280
  hii nchi kama kichwa cha mwendawazimu...

  ktk reli na ndege hakuna ufanisi, serikali imeshindwa kufanya biashara
   
Loading...