Serikali inachowafanyia Wanachuo sio kitu kizuri

MADABACHU

JF-Expert Member
Nov 24, 2020
325
379
Ipo hivi: unajua mtu mwaka wa kwanza na wapili ulipata allocation yako vizuri, sasa mwaka wa tatu huu unajiandaa kwenda chuo bado siku tatu unakuta ada imepunguzwa na hela za stationery nazo wamechukua, wanatarajia mtu atafanyaje kwa kipindi hiki kifupi hivi.

Na ukiangalia sioni sababu ya kupungua maana kama ni matokeo ni mazuri GPA ipo above 3.5 sasa tuseme hawana hela au ndio nini.

Wanajidai kusema kuwa wanaongeza kutoa mkopo kumbe kwa kupunguza zingine Ili wawape hao wanaoanza, daah! Hii hali sio nzuri, maisha utaona machungu na ukiangalia hamna unapotegemea zaidi ya hiyo boom nayo hata ukisema ulipie ada haitoshi kabisa.
 
Daah Pole mkuu najua inaumiza Sana unajiandaa kwenda Chuo alafu unakuta wamekupunguzia Allocation alafu mda umeisha. Hii ndio Serikali ya Wanyonge
 
Nina mdogo wangu aliniambia mkopo wake tokea kipindi cha corona umepunguzwa. Hili lina ukweli kwa wale mnaopata mkopo ?
 
Mimi mbona nikitaka kuangalia allocation projection sioni chochote?,nielekeze please
Ipo hivi unajua mtu mwaka wa kwanza na wapili ulipata Allocation Yako vizur sa mwaka wa tatu huu unajiandaa kwenda chuo BADO siku tatu unakuta Ada imepunguzwa na hela za stationary nazo wamechukua wanatarajia mtu atafanyaje kwa kipindi hiki kifupi hivi na ukiangalia sioni sababu ya kupungua maana Kama ni matokeo ni mazuri GPA IPO above 3.5 sasa tuseme hawana hela au Ndio nini .
wanajidai kusema kuwa wanaongeza kutoa mkopo kumbe kwa kupunguza zingine Ili wawape hao wanaoanza Daah hii Hali sio nzuri Maisha utaona machungu na ukiangalia hamna unapotegemea zaidi ya hiyo Boom nayo hata ukisema ulipie Ada haitoshi kabisa
 
jambo la kushukuru kidogo umewekewa .,, ila ni madahaifu ambayo yapo kwa mfumo wetu.. nakumbuka wakati namaliza diploma (ifm) matokeo yametoka na hela za kuomba mikopo tukalipishwa halafu majibu yakaja watu wote tulosoma diploma hakuna mikopo..wenzetu walotutangulia mbele yetu walibahatika na ndio walikuwa wa mwisho kupata mikopo tokea level ya diploma... tuliamua why walituruhusu tuombe na kuomba mkopo ni gharama?? ila tulivuka na tulisoma degree japo kwa nguvu nyingi na kuunga unga haswa sisi watoto wa familia za chini
 
Back
Top Bottom