Serikali Imewafanyia "Bait and Switch" Madaktari?

Serikali Imewafanyia "Bait and Switch" Madaktari?

Mi hii habari ya serikali haitoi ajira sababu haina ela siiamini, mbona ndege zinanunuliwa kwa mabilion ya pesa, mradi mingine inafanyika hizo pesa zinatoka wapi? Hebu nisaidieni,
 
Msomi Mwanakijiji!
1. MAT hawakupinga madaktari wa Tanzania kuajiriwa Kenya. Wamehojiwa Mara nyingi kwenye vyombo vya habari. Na wamekuwa wakitamka bayana kwamba hawapingi madaktari kuajiriwa Kenya, japokuwa wamekuwa na maelezo ya ziada ambayo mwisho wa yote yanaonyesha kuunga mkono madaktari kuajiriwa Kenya.
2. Kuuliza kwako kwamba madaktari watakuwa na ajira za mkataba gani kunaonyesha kutapatapa kwako sababu ajira za serikalini Tanzania zinaeleweka na nature ya mikataba yake inaeleweka.
3. Hawalazimishwi kupata ajira mpya serikalini. Serikali imewapa offer ya ajira ambayo kwa hakika ni upendeleo kutokana na uzalendo walioonyesha. Wana uhuru wa kukubali au kukataa.
 
Hutaki waajiriwe au
..sitaki waajiriwe kisiasa...kwamba baada ya siasa za majitaka za kujikomba kwa wakenya kugonga mwamba eti ndio wanaamua kuwaajiri!...kwanini tufike huku?.....kwamba leo ndio serikali imeona shida ya madaktari tz??...kwamba waliwahurumia wagonjwa wa kenya kuliko wazawa wa tz??.....hii kwangu ndio issue....hayo ya kutotaka waajiriwe ni mavi yako...
 
Monte.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

DAR-ES-SALAAM (ZAMAMPYA.COM) Katika hali ambayo inaonesha kufanyika kwa ‘cheupe chekundu’ au mchezo wa "karata tatu" Serikali ya Tanzania imeamua kuwabadilishia maombi madaktari waliojitokeza kuomba kazi Kenya baada ya kuamua madaktari hao waajiriwe katika Serikali hata kama hawakuomba ajira ndani ya Serikali.

Hilo limeelezwa katika taarifa iliyotolewa na Waziri wa Afya Bi. Ummy Mwalimu (pichani) katika taarifa yake kwa waandishi wa habari leo ambapo amesema kuwa Rais John Magufuli “ameamua” kuagiza madaktari waliokuwa wanasubiri kwenda Kenya kuitikia wito wa nchi hiyo kuomba madaktari wa ziada baada ya mgomo mkali wa madaktari uliofanyika nchini humo kuanzia mapema mwaka huu.

Taarifa ya Wizara imesema kuwa “tarehe 18 Machi, 2017 Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto ilitangaza nafasi hizo za ajira kwa Madaktari wa Tanzania kwenda kufanya kazi nchini Kenya. Maombi hayo yalipokelewa ambapo hadi tarehe 27 Machi, 2017 ambapo jumla ya maombi takribani 496 yaliwasilishwa. Baada ya kufanya uchambuzi wa maombi haya ilibainika kuwa, Madaktari 258 walikidhi vigezo vilivyotakiwa kwenda kufanya kazi nchini Kenya.”

Kwa mujibu wa taarifa ya Bi. Mwalimu “wakati Serikali ya Tanzania ikiendelea kukamilisha utaratibu wa ajira za Madaktari wake nchini Kenya ikiwa ni pamoja na kutangaza nafasi hizo za kazi na kufanya uchambuzi wa maombi ya kazi, kuandaa Hati ya Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Kenya kuhusu ajira hizo za Madaktari na Mkataba wa Ajira kwa Madaktari hao, wananchi (Madaktari) watano wa Kenya waliwasilisha pingamizi Mahakamani kuitaka Serikali ya nchi yao kusitisha kuajiri Madaktari kutoka Tanzania.”

Bi. Mwalimu alieleza kuwa “Kwa kuwa ratiba ya utekelezaji wa ajira hizi za Madaktari ilikubalika na pande zote mbili kuwa iwe imekamilika ifikapo tarehe 6 Aprili, 2017 na kuwa Madaktari hao wawe tayari kusafiri kwenda nchini Kenya kati ya tarehe 6-10 Aprili, 2017 na kwa kuwa hadi tarehe ya taarifa hii Mahakama nchini Kenya haijaondoa pingamizi lililofunguliwa kuhusu ajira za Madaktari wa Tanzania nchini Kenya.”

Kesi ya pingamizi lililotolewa na Mahakama ya Kenya kuzuia Serikali ya Kenya kuajiri madaktari wa kigeni inatarajiwa kuendelea huko Kenya siku ya Ijumaa wiki hii.

Tangazo la ajira za Kenya lilitolewa na Wizara kupitia Katibu Mkuu wake Dkt. Mpoki Ulusubisya ambapo lilieleza kuwa madaktari hao wanaotaka kwenda Kenya walikuwa waende kwa mkataba wa miaka miwili.

Hata hivyo Chama cha Madaktari Tanzania (MAT) kilipinga mpango huo na kudai kuwa kufanya hivyo ni kutowatendea haki madaktari wa Kitanzania na pia kutoitendea haki sekta ya afya Tanzania ambayo nayo ina upungufu wa madaktari. Katika tamko lao la kupinga mpango huo la tarehe 20/3/2017 chama hicho kilisema kuwa “Kwa kuwa MAT haikushirikishwa katika hatua yeyote na hivyo kukosa fursa yakufahamu lolote, Hivyo basi tungependa kupata ufafanuzi kuhusu masualayafuatayo ;Kwa nini Serikali ya Kenya imeshindwa kuajiri Madaktari wake na kuanza kutafuta Madaktari kutokaTanzania huku ikizingatiwa kwamba malipo ya Madaktari wa Tanzania yatakuwa makubwa zaidi ya wenyeji ?”

Uamuzi uliotangazwa leo na Waziri Mwalimu hata hivyo hausemi kama madaktari hao 254 ambao wataajiriwa Serikali wataajiriwa kwa mkataba wa aina gani na utakuwa na tofauti gani na madaktari ambao tayari wanafanya kazi nchini hasa ikizingatiwa kuwa wengi waliomba nafasi ya kwenda Kenya kwa sababu ya maslahi yao kwani walikuwa wanatarajiwa kulipwa kama wataalamu wa nje huku wakiahidiwa malipo manono na nyumba.

Hata hivyo, haijajulikana kama madaktari hawa ambao walikubaliwa kwenda Kenya na sasa wameamuliwa kufanya kazi Tanzania watakubali ajira hizi mpya ambao wao hawakuziomba au kama watalazimishwa hasa kwa vile Serikali katika taarifa yake imesema kuwa “majina ya Madaktari husika na vituo watakavyopangiwa kazi yatatangazwa katika tovuti ya Wizara www.ehealth.go.tz pamoja na wataalamu wengine wa Afya 11 walioleta maombi yao na kukidhi vigezo.”

Serikali imeendelea kuahidi kuwa itakuwa tayari kusaidia Kenya madaktari 500 baada ya mapingamizi yaliyowekwa kuondolewa lakini haijaeleza taarifa hiyo endapo nafasi hizo zitaanza tena hawa madaktari ambao watakuwa waajiriwa wa serikali ya Tanzania watapewa nafasi tena ya kwenda Kenya kutafuta maslahi zaidi au wakikubali ajira za serikali ndio nafasi ya kutafuta maslahi nje ya nchi zitakuwa zimepotea.
Ukiwa na wanasiasa wanaozunguka maeneo mengi na wasanii nao wanageuka wanakuwa wasanii.

Nchi imejaa VIHOJA in Tundu Lissu's voice
 
Hii serikali ni ngumu sana. Ni serikali inayoweza kuamka na kukurupuka na tamko lolote, kuna kukurupuka kuajiri na kuna kukurupuka kufukuza.

Bado sijaelewa mantiki nzima ya tangazo hilo la serikali la kuajiri, je, serikali ilikuwa ina mpango wa kuwaajiri madaktari au huo ulikuwa ni ujanja wa kutaka kuwaajiri madaktari wachache kwa 'gear' ya kusema wanatakiwa kwenda Kenya?
Hapa serikali imeonyesha inajali watu wake. Iliwatafutia ajira na kumetomea matatizo kule. Ili kuwaondolea msongo wa mawazo imeamua kuwachukua yenyewe. Shida iko wapi? Au ndiyo tunapinga kila kitu?
 
  • Thanks
Reactions: bdo
Tatizo langu ni hii impression inayojengekea kuwa Rais is everything: Ndiye mwajiri, ndiye anaamua kutoa madaktari waende nchi kwa jibu la papo kwa papo; ndiye anagawa hela, ndiye anazuia vyeo visipande, mishahara ipunguzwe, ajira zisitishwe, sherehe zifanyike, watu waende nje au wasiende; nani apelekwe hospitali nje na nani asiende; hspitali gani ipewe vitanda na jengo gani libadilishwe matumizi; nani anyang'anywe passport; shule gani itaifishwe na wanafuzi wake wote wabadilike na kuwa wa serikali; aamue kama kuna njaa au hakuna, shirika gani likatiwe umeme; n.k

Tukubali tuna tatizo kubwa kuliko linavyoonekana kwa juu
Kwani wewe hukuwahi kufahamu Rais ndiyo kila kitu nchini? Brother uko serious?
 
Tatizo langu ni hii impression inayojengekea kuwa Rais is everything: Ndiye mwajiri, ndiye anaamua kutoa madaktari waende nchi kwa jibu la papo kwa papo; ndiye anagawa hela, ndiye anazuia vyeo visipande, mishahara ipunguzwe, ajira zisitishwe, sherehe zifanyike, watu waende nje au wasiende; nani apelekwe hospitali nje na nani asiende; hspitali gani ipewe vitanda na jengo gani libadilishwe matumizi; nani anyang'anywe passport; shule gani itaifishwe na wanafuzi wake wote wabadilike na kuwa wa serikali; aamue kama kuna njaa au hakuna, shirika gani likatiwe umeme; n.k

Tukubali tuna tatizo kubwa kuliko linavyoonekana kwa juu
Hata watu wamekugongea like. Watanzania kweli kabisa IQ zetu ziko chini mnoooooo. Unaongea madudu watu wanakugongea likes. Rais hujui kama ndiyo namba 1 nchini? Au umetokea kuzimu Bro?
 
Hata watu wamekugongea like. Watanzania kweli kabisa IQ zetu ziko chini mnoooooo. Unaongea madudu watu wanakugongea likes. Rais hujui kama ndiyo namba 1 nchini? Au umetokea kuzimu Bro?
===

Nyangomboli kumradhi sikujua kama rais ndiye kila kitu. Alipoteua mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya, makatibu wakuu, wakurugenzi na wateule wengine, niliamini anagawa madaraka ili wengine wafanye kwa niaba yake!

Tulipounda serikali za mitaa (kugatua) nilidhani kuna mpaka unaotenganisha serikali hizo na serikali kuu!

Pia kabla sijaenda kuzimu kutembea, niliacha utaratibu wa rais wa kuwaagiza wateule wake unafanyika ofisini si lazima hadharani (kuagiza mtu anyang'anwe passport) au kubatilisha tangazo la waziri kuhusu ufungishaji wa ndoa kwa kutumia vyeti vya kuzaliwa! Nimerudi kutoka kuzimu nikakuta kuna mambo mapya na yanamchosha rais wetu kufanya kila kitu.

Hata wewe ukienda kuzimu leo na kurudi kesho, kuna mambo utayashagaa. Jaribu uone.
 
Msomi Mwanakijiji!
1. MAT hawakupinga madaktari wa Tanzania kuajiriwa Kenya. Wamehojiwa Mara nyingi kwenye vyombo vya habari. Na wamekuwa wakitamka bayana kwamba hawapingi madaktari kuajiriwa Kenya, japokuwa wamekuwa na maelezo ya ziada ambayo mwisho wa yote yanaonyesha kuunga mkono madaktari kuajiriwa Kenya.
2. Kuuliza kwako kwamba madaktari watakuwa na ajira za mkataba gani kunaonyesha kutapatapa kwako sababu ajira za serikalini Tanzania zinaeleweka na nature ya mikataba yake inaeleweka.
3. Hawalazimishwi kupata ajira mpya serikalini. Serikali imewapa offer ya ajira ambayo kwa hakika ni upendeleo kutokana na uzalendo walioonyesha. Wana uhuru wa kukubali au kukataa.

Hivi umesoma tangazo la Wizara au unafikiria umelisoma? Kuna mahali wamesema wamewapa ofa ya kukubali au kukataa?
 
Wengi wa hao madaktari watakataa hizo ajira za Serikali.Nani anataka kwenye kijijini kwenda kudhalilishwa na ma RC na ma DC wa mihemko.Wengi wataamua kuendelea na ajira zao AAR, Aghakani,TMJ, Hindu Mandal, Kairuki, Tabata General, Regency n.k
 
Mbona walimu Kenya hawagomi ili tz iombwe walimu 1000 ili walimu wetu waliozagaa mtaani wapate shavu
 
Back
Top Bottom